TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Vijana,Siasa za mihemko na Ukamanda.Mbowe anakula bata na Maisha yanaendelea.Mtatumika sana mpaka pale mtakapojitambua

Duniani kote kuna siasa na wanasiasa lazima wawepo no matter how utakavyotafsiri dhamira yao ila hili la kuua mtu kwasababu muuaji anaamini atalindwa na chama chenye dola linajenga chuki kwa level ambayo sio mwanasiasa tu atakayedhurika na chuki hii so chagueni lugha ya kujadili hichi kifo.
 
Siasa za ccm sasa zimefika pabaya

Sina cha ziada naomba niseme kwa masikitiko makubwa nimeumia sana na nimeumizwa zaid pale ambapo nmemuona mtu mzima akihojiwa hadi amelia kama mtoto mdogo, ubinadamu hakuna tena kwa sasa watu wamekuwa kama wanyama na nafikiri ule msemo wa kumuachia mungu kila jambo ufike mwisho
 
Yanahitajika maamuzi magumu badala ya kuendelea kudhalilishana hivi. Viongozi wa CDM mpo wapi???
 
Mhaini uso na utu wewe umelewa uGAMBA mpaka utu umeuweka pembeni
Muogope hata mungu
Changu, punguza jazba. Huu ni msiba. Sioni tatizo kwenye comment yangu iliyokufanya ufyatuke. Mwogope Mungu na mwombe akupe moyo wa ujasiri uache tabia ya kutoa mapovu hovyo mitandaoni.
 
Hamjishughulishi na kueleza chanzo cha tukio, mazingira ya hilo tukio, mnachoona ni sahihi kwenu ni kusema "wanaosadikiwa kuwa vijana wa ccm"

Kama siyo vijana wa ccm tuambie niakina nani walikuwepo wanasema vjana wa ccm alafu we unakataa.Tafadhali usija ni sababishia burn bure
 
Acha kuropoka ww,kuna uchaguz mdogo unafanyka wa diwan hiki n kpnd cha kampen

Huo ushahidi kuwa kauwawa na CCM unaweza kutuletea hapa na sisi Tuufahamu? Je kama kuna mtu anajaribu kuchochea vurugu na kutokuelewana kwa kupitia kifo cha mwanachama wa Ukawa ionekane ameuwawa kisiasa? Je kama alikosea watu ambao waliamua kulipa kisasi?
 
Naiombea Amani Tanzania yetu, atuepushe na siasa hizi tunazoanza kuzishuhudia... Wote tunashindana ili kujenga nyumba moja Tanzania.... Vijana acheni kutumika kwa watu wa maslahi binafsi,
Imagine wewe unamtoa uhai mwenzio kisa unamtetea mtu fulani apate nafasi fulani.
Je mnapopishana yeye akienda huko mjengoni na wewe gerezani, hapo umepata nini?????
Umewaachia shida wategemezi wako kisa posho ya kampeni au ukada wa Chama fulani, not fare walaaniwe Wote Wanaoharibu Jina la nchi yetu
R. I. P shupavu wa demokrasia ya kweli Alphonce mawazo (kama habari hii ni ya kweli)

Wakuu sio tetesi tena imetangazwa na ITV habari za saa mbili usiku huu kuwa ni kweli. Kavamiwa kwa mashoka na nondo na wanaosadikiwa ni green gurds wa ccm na kafia hospitali ya wilaya Geita muda mfupi baada ya kufikishwa hapo. Mashuhuda waliomfikisha hapo wanasema hawakupata msaada wa polisi.Nisichokielewa ni kama mikutano ya kata ambayo humchagua diwani nayo inaombewa kibali cha polisi wilayani. Ikiwa nayo inapewa kibali cha polisi ni wazi na ulinzi wa polisi utolewe. Uelewe huu ni mkusanyiko wa watu wengi na lolote kuweza kutokea k.m. vurugu na uvamizi wa mahasimu n.k. Je kwenye mkutano husika ulikuwa na ulinzi wa polisi wawe wa wilayani au wa kata? Hao green-guards wa ccm wanakaa kwenye kata au wanakuwepo makao makuu ya wilaya kusubiri kusambazwa inakofanyika mikutano ya ccm? Hapa inaonekana wazi kuwa Mawazo alifuatiliwa kwa lengo tu la kutolewa uhai na wahusika wa mpango huo sio watu wadogo. Ila la kufahamu ni kuwa damu ya Alphonce Mawazo inayoililia ardhi mungu hatachelewa kujibu na kuwaumbua wahusika wote kwani Mawazo analiliwa na watu wengi mno. Wala msitegemee kuwepo uchunguzi wowote.Ushauri wa bure ni kuwa endapo haya ndio matokeo ya siasa za vyama vingi kwa ushauri wangu ni bora kuwa na chama kimoja na kuokoa roho zinazoangamia bila sababu. R.I.P.KAMANDA MAWAZO.
 
Hili swala tunapolijadili tuondoe itikadi za kivyama..

Naamini hakuna chama kinachoruhusu mauaji... Wahuni wachache kwa maslahi yao.

Nimesoma toka mwanzo nashindwa kuelewa chanzo cha tukio kilikuwa nini ..

R.İ.P Aliphonce Mawazo.
 
Uchunguzi ufanyike,hatutaki kusikia jeshi la polisi likikimbilia kutoa matamko ya kipuuzi,uchunguzi wa kina first!Utashangaa issue ya Geita,kova anakimbilia kutoa tamko
 
Nashindwa kuelezea machungu niliyonayo kwa kufiwa na Mawazo. Najuta kuwa mwana CCM kabla sijaondoka mwaka huu chama hatari sana hasa kwenye madaraka. Mawazo aliweka pingamizi kwa huyu "sata" Laurencia Bukwimba na alikuwa na kila ushahidi wa kushinda kesi. Sasa njia aliyoona inafaa ni hiyo. Haiwezekani damu yake iende hivihivi kama ya kuku.

Uko sahihi kama ninavyowaza, ni matumaini yangu kesi itaendelezwa na chama.
 
Ni kweli nimesikia pia azam wakisema kulitokea kutoelewana na wafuasi wa ccm. Wamama wanapiga ukunga wanalalamiks maana ya vyama vingi nini sasa km hatueez kuvumiliana? Vifutwe basi. Inasikiyidha sana
 
Yanahitajika maamuzi magumu badala ya kuendelea kudhalilishana hivi. Viongozi wa CDM mpo wapi???

Mkuu mimi sijui labda Mbowe hatuamini,Labda haamini kama ana vijana tunaoweza. CCM wanatumaliza, tumeibiwa kura, watu wamewekwa ndani mpaka leo, watu wanakamatwa hovyo hovyo, watu wanauawa.Hakuna tangazo lingine la vita zaidi ya hili, Mbowe ananyamaza sisi tunageuka mbuzi wa sadaka!
 
Namlaumu sana Lowassa kwa udhaifu wa kuwanyamazia CCM. Haya yote yanafanywa kwa kuendelea kuwa kimya. Nimeongea na rafiki yangu akiwa Katoro inasikitisha sana. Wamemuua mchana kama wanaua mwizi (gari mbili zikiwa na hao watu). Tapata wapi silaha jamani!!!?
Nenda kawaulize IS wanazipata wapi
 
dah!!! hizi siasa zingine sio kabisa, imefikia hatua tunauana wenyewe kwa wenyewe kisa uongozi????? R.I.P kamanda
 
Imenisikitisha sana. Marehemu alikuwa mtu wangu wakaribu. Marehemu alikuwa MC kwenye Harusi yangu those days.

R.I.P Brother
 
Sitawasamehe ccm for the rest ofvmy life..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom