TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
RIP Mawazo kama mtanzania mwenzangu.

Kitendo kilichofanywa dhidi yako hakikubaliki na yoyote mpenda amani na utulivu.

Ni vizuri jeshi la polisi likawasaka na kuwakamata watu wote waliosababisha kifo chako. Hili ndugu zangu halina itikadi na tuuweke pembeni u CCM na u CHADEMA.

Waliofanya kitendo hicho ni wahuni na siamini kama wametunwa na chama chochote zaidi ya matakwa yao tu. Tuwe na amani na tusubiri ripoti kamili ya jeshi la polisi....tusiwe ns jazba na kukimbilia kusema tulipize kisasi kwa watu fulani bila ushahidi...
 
Na laani kwa Nguvu zote wote walioshiriki kukatisha uhai wa kamanda Mawazo.

Pumzika kwa amani kamanda Mawazo, umetuacha wanabadiliko na mawazo.

Daima nitakukumbuka katika harakati na ujasiri utadumu milele kwa wapenda haki.
 
Masikitiko kwenu yatoke wapi? si umesikia ni vijana wenu wa green guard ktk kutetea maslahi ya chama chenu?

Lakini yana mwisho!!

Kama ni kweli habari hii inasikitisha sana maana Mawazo nilimfahamu vzr kwakweli. Ila napingana na huu utamaduni wa kuhusisha siasa kwenye kila tukio na vyama vingine vya siasa. Tunakosea sana. RIP Mawazo
 
Nimelia kwa kweli, amenikumbusha Mohamedi Mtoi dah, ila mwisho wa haya mambo si mwema. Auwaye kwa upanga atakufa kwa upanga
 
Last edited by a moderator:
R I P Mawazo,uwanja ulibubujikwa na majonzi baada ya mw,kiti wa chadema Arusha kutoa taarifa za kifo cha Mawazo tulipokua kwnye mkutano wa kampen jimbo la Arusha mjini,wtu wte walidondosha chozi kwa ajili ya mawazo,lkn machozi haya hayatamwagika bure,yatarudi na majibu chanya.
 
Wanaojua wanasema ni vijana wa green guard,munaoamini munasema waliokula hela wote watakufa!! Basi mutaendelea kuua hadi muwamalize wote? Kwa kuamini tu?

Unawatambuaje green guard? Kama ni mavazi, mtu yeyote anao uwezo wa kuvaa uniform zisizomhusu kwa kusudio maalumu alilonalo. Kama waliwatambua kwa sura kwa kuwa wanawafahamu, kwanini hao wanaodai waliwatambua kuwa ni green guard wasiwataje wajulikane haraka? Kama ni magari, plate number si zipo? Mbona hili swala linaashiria kusudio la uchochezi wa wazi kabisa?
 
Walaaniwe waliofanya mauaji haya, wameua kwa upanga na watauawa kwa upanga. Kamanda Alfonce Mawazo ninakulilia, ninakulilia sana. Nina uchungu na maumivu moyoni mwangu.
 
Shujaa ameondoka, akiwa juu jukwaani,
Pambano la uhakika, likiwa bado matatani,
Majahili yenye shoka, mapanga na uhayawani,
Kweli umetokwa roho, Shujaa umelala chini!

Ulipotoka Arusha, Mwanza ukajikita,
Vijana uliwakosha, kwa semi zenye kumeta,
Ujasiri ukawasha, wakawa kama ukuta,
Kweli umetokwa roho, Shujaa umelala chini!

Nilipokuona kwanza, nilidhani ni Samora,
Mawazo yakaangaza, Ukombozi ulo bora,
Zama za mwangaza, Mapambano yenye sura,
Kweli umetokwa roho, Shujaa umelala chini!

Nashindwa kusema sana, rohoni nina huzuni,
Japo ulikwisha nena, tuchukue yako thamani,
Mapambano yenye kina, yatokemeze wahaini,
Wanaodhani Tanzania, ni mali ya vitukuu vyao.
 
Nakumbuka hata mgombea ubunge Geita mjini alishasema kuwa wana harakati wote wa upinzani kanda ya ziwa wanawindwa sana..ni kwamba kitengo wanataka kufuta kabisa upinzani mkoani Geita na kanda yote ya ziwa ambapo mkuu anatoka

Na inabidi viongozi na wagombea wote wa UKAWA kuwa na tahadhali kwa kila wanapokwenda maana "jini" lina hasira baada ya kuona linakosa wapiga kura vijana kadri siku zinavyokwenda. R.I.P Kamanda Mawazo.
 
Inaumiza Sana . Nakoswa hata neno la kusema hasira zimeujaza moyo wangu!
 
RIP Mawazo kama mtanzania mwenzangu.

Kitendo kilichofanywa dhidi yako hakikubaliki na yoyote mpenda amani na utulivu.

Ni vizuri jeshi la polisi likawasaka na kuwakamata watu wote waliosababisha kifo chako. Hili ndugu zangu halina itikadi na tuuweke pembeni u CCM na u CHADEMA.

Waliofanya kitendo hicho ni wahuni na siamini kama wametunwa na chama chochote zaidi ya matakwa yao tu. Tuwe na amani na tusubiri ripoti kamili ya jeshi la polisi....tusiwe ns jazba na kukimbilia kusema tulipize kisasi kwa watu fulani bila ushahidi...

Inapofika mahali inahitajika busara na uvumilivu ni upinzani.Mmetugeuza target ya kujifunzia.

Tupelekane kazi tu wanaume,sisi tupate nafasi ya kujitetea.Busara hapa haina nafasi.
 
Ikiwa tunahubiri AMANI bila kujua kiasi gani mioyo ya watz imechoka kusikia neno hilo bila ya kuwa na pacha wake HAKI ni sawa na kuchota maji kisimani na kuyamwagia baharini...hii nchi ni ya watz wote na endapo tunaweza kuwa na ujasiri wa kutamka neno 'amani' bila 'haki' ipo siku hata hilo neno amani itakuwa ni vigumu kulitamka.
 
Mawazo damu yako haitamwagika bure, Lazima nitaonyesha mfano, Watanzania wamezoea kila jambo linapita tu! Mimi nasema hili la kwako halitapita tu! Lazima tuionyeshe dunia kuwa tumechukizwa na ukatili huu! Niko tayari kuusalimisha uhai wangu, lakini dunia itajua tu! MAWAZO umekatiliwa maisha yako!!!
 
Rip ,
mh rais magufuli we ni mcha Mungu hakikisha haki inapatikana, tunakutazama, chukua kwanza hatua za makusudi kuonyesha kuwa hukubaliani na mauaji haya
 
Walaaniwe waliofanya mauaji haya, wameua kwa upanga na watauawa kwa upanga. Kamanda Alfonce Mawazo ninakulilia, ninakulilia sana. Nina uchungu na maumivu moyoni mwangu.

Acha kulia kamanda jiandae tu, huenda viongozi wetu wakatoa tamko la kudai haki.Kilio tuwaachie watoto!
 
Kwa msaada wa wananchi watuhumiwa 3 walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa mapoliccm cha ajabu ndani ya nusu saa wakaachiwa huru na kutokomea........!
 
Busara inahitajika katika kipindi hiki kigumu ndugu zangu.

Nyie mlioko nyuma ya keyboard mnahamasisha tusivumilie tulipize kisasi anzeni nyie kwa kutaja majina yenu halisi hapa ili tuwaone sio waoga mmechoka...

Tusubiri ripoti ya polisi...tusihukumu harakaharaka...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom