TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.
Kuwa Na roho ya utu wewe! Sidhani kama ukatili huu unafurahiwa Na mwanadamu yeyote awe ni wa itikadi gani. Huu ni unyama wa hali ya juu. Siasa zisitufikishe hata kiasi cha kugharimu damu za watanzania wenzetu. Hizi ni siasa tu. Leo upo ccm, kesho Act, baadae Cdm

diunal kuna watu hawajui siasa si uadui.wapo radhi kujitoa ufahamu kabisa tena kwa mambo makubwa yanayohusu uhai wa binadamu wenzao jambo ambalo hata mungu aliyetuumba hapendezwi
 
Last edited by a moderator:
Siku ya mazishi viongoz wa chadema washirik wote!tuiite mawazo day!nilifurah taifa starz kutoka suluhu,wakati mechi ikiendelea nikapata habar nikanywea mpaka mpira unaisha cjashangilia,nashukuru Mungu mashabik nao walinywea baada ya dk.90,tukaungana sote kwenye huzuni.Japo huzun yangu ilikuwa ya kumpoteza kamanda wangu Alphonce Mawazo.RIP kamanda sote tunakuja.

Retina inaumiza sana
 
Last edited by a moderator:
Kumbe zali walilianzisha wenyewe? Iko poa tu,nyie mnafikiria mkiamua kuwapiga watu mnawapiga tu,iko siku watu watachoka na haya ndio yanayotokea sasa. Katika uchaguzi kuna mgombea wa ubunge hukohuko Geita alikamatwa kwenye gari yake na nondo,silaha za jadi na pombe kali ya viroba,sijui ni huyuhuyu marehemu au mwingine?
 
Habari Watanzania wenzangu,

Nimesikitishwa saana na kifo cha ndugu yetu Alphonce Mawazo lakini nasikitishwa zaidi na uvumi unaosambazwa wahusika ni green guard wa CCM nashindwa kuamini moja kwa moja kutokana na maneno yaliopo hapa baada ya uchaguzi katika jimbo alilogombea Alophonce Mawazo.

Baada ya matokeo kutoka wafuasi wa CHADEMA katika jimbo hilo walishangazwa na matokeo yaliotoka kwamba kamanda Alphonce ameshindwa katika uchaguzi huo hali iliozusha sintofahamu kwa wafuasi wa chama hicho kutokana na kushindwa kwake na kutoonekana katika eneo la jimbo tangu siku ya mwisho ya kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo.

Kutokana na kutoonekana kwa ndugu Alphonce Mawazo katika jimbo kulileta sintofahamu kwa wafuasi wa CHADEMA ndipo zilipozuka fununu ndugu Alphonce Mawazo aliuza jimbo kwa chama tawala na kukubali kushindwa kirahisi, hali hiyo ilileta chuki kwa makamanda wa CHADEMA hali iliyosababisha waape kwa miungu yote kuwa atakapoonekana hadharani ama zao ama zake lazima wamdhuru, ikibidi hata kumuua.

Hivyo kutokana na hasira za wapenzi wa chama hicho nashindwa kuamini moja kwa moja upande mmoja tuu wa green guard wanahusika kwani kama kushindwa alikuwa ameshashindwa ubunge na hakua tishio tena kwa chama cha mapinduzi, kwangu mimi naweza sema kama angekua tishio kwa chama cha mapinduzi basi wangemdhuru wakati anatafuta jimbo lakini sio kwa sasa ambapo hakuwa mshindani hivyo napata ukakasi sana kuamini kama kuna nguvu yoyoye kutoka chama cha mapinduzi ilio nyuma ya kifo cha kamanda Alphonce Mawazo, lakini pia naona kuna watu wanataka kugeuza kifo cha kamanda Alphonce Mawazo mtaji wa kisiasa.

Naomba tutafakari pia hawa wapenzi wa CHADEMA walikuwa wakiapa kuwa lazima watamdhuru baada ya kuhongwa hela ili akubali kupoteza jimbo lakini pia tukiwa tunasubiri matamko ya police na uchunguzi wao ni vema tukawa watulivu kusubiri uchunguzi wa polisi maana yapo pia mambo nje ya siasa ambayo yanaweza pelekea mtu kuumizwa hata kuuwawa ikiwemo biashara, ugoni, imani za kishirikina, ujambazi. nk

Hivyo kabla hatujanyanyua vidole kunyoosheana kwa hisia na kupandikiza uhasama wa kisiasa ni vema tukatafakari upya na kusubiri vyombo vya dola kuleta ukweli. Nichukue nafasi hii kuwapa pole wafiwa na wapenzi wake MUNGU ALITOA MUNGU AMETWA JINA LA BWANA

Tusivutane sana tusubiri taarifa kutoka polise ndio yenye hatima na ukweli huo.
 
Kadri siku zinavyoyoyoma ndivyo amani inavyotoweka ndani ya mioyo ya wapenda haki wengi wa nchi hii.
Hapa nchini Kila Mara Uchungu unawekwa kwenye akiba ya UCHUNGU MKUU!
Usipokuja asubuhi basi utegemea jioni.

Jana maadui wa Amani wameongeza tena UCHUNGU kwenye account ya mioyo ya wengi kwa Mauaji ya Alfonce Mawazo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa Wa Geita.

NIMEKUWA NAJIULIZA SWALI HILI JADIDI,
Hivi kweli Dola hili kubwa limeridhika kabisa kuwa taifa la watekaji na wauaji?
Kama si hivyo naomba niambiwe,
Nani alimuua Daudi Mwangosi?
Nani walimuuwa Dr Mvungi
Nani walimteka na Kumpiga vile Dr Ulimboka
Vipi kuhusu Absalomu Kibanda; na wengine wengi walioteswa na kuuawa vilevile kama hawa!

Mpaka sasa ni hatua gani zilichukuliwa na vyombo husika ili haki itendeke, na ionekane wote kutendeka.

Hofu yangu hapa ambayo kwa kweli sijui kama wenzangu wanayo ni pale
Kikombe cha Uovu na Ubaya wa taifa kinapojaa na kumwagika sana!

Yaani ni kana kwamba foleni imesogea na zamu yetu imewadia!
Swali ni kuwa ili msambaratiko huu utimie je utapelekewa na mauaji ya nani, wapi, na lini?

Na je tokea sasa zimebaki hatua ngapi ili tuvuke mstali na kuvuna kile tulichokipanda wenyewe kwa gharama ya ujinga na ulevi wetu!

Napatata mashaka makubwa juu dhamira ya watesaji na wauaji hawa! Hivi kwani wao hawaoni kuwa wanalipeleka taifa hili kusiko?

Najua wakurupukaji watakuja na mengi lakini
Huu si Utabiri wa kiganga la!
Hii ni kanuni ya asili tu!
Mtu huzaliwa na baadaye hufa.
Taifa huundwa hatimae huparanganyika.

Mwisho kabisa,
Ukimwona mtu mzima juu ya mti, anaelekea kwenye tawi kavu; ukamwonya asikubali; akianguka chini, je ni wewe uliyemsababishia anguko lake? Hapana!
Ukivunja kanuni ya asili ni lazima upate stahili yako.
 
UTARATIBU ULIOWEKWA NA CHAMA KUHUSU MAZISHI YA
KAMANDA ALPHONCE CHEMU MAWAZO ALIYEKUA
MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA GEITA.....




Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kimetoa
hatua na utaratibu utakaofuatwa mpaka hatua za mazishi ya
kamanda Mwenzetu Alphonce Mawazo ....




Leo maiti yake itapelekwa katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando jijini Mwanza..Mwili huo utachukuliwa leo katika
hospitali ya wilaya ya Geita Na mheshimiwa Godbless Lema
na makamanda wengine kupelekwa hospitali ya Bugando jijini
Mwanza.......




Baada ya wabunge wote wa CHADEMA/UKAWA kuapishwa
bungeni siku ya tarehe 17/11/2015 ndipo watakuwa tayari
kuelekea katika mazishi wakiambatana na viongozi
waandamizi wa CHADEMA na UKAWA Kwa ujumla....



Kwa kheri kiongozi wangu Mawazo
Buriani Kamanda wangu Savimbi kama ulivyojiita kabla ya
mauti.....




CHADEMA itakukumbuka, UKAWA itakukumbuka na Tanzania
itakuheshimu Daima...



Bwana Ametoa,wanadamu wametwaa!!!!
Jina la bwana lihimidiwe..AMINA..
 
Mchokoo ni kweli kabisa hata mie machungu yanazidi sana! Ipo siku uvumilivu utafika mwisho.Kova unafurahia vitisho! Shukuru Mungu wadanganyika ni waoga sana!
 
hizi laana zinachosha toka
Dr mvungi
Dr Ulimboka
Kibanda
Mwangosi
Tukio la Soweto
Moses Machali na Kiwia
Mch.Mtikila
hizi laana zote hawa watu wangekuwa vichaa na watoto wao
kweli sisi tunamwachia Mungu kila kitu

Chacha wangwe.....
 
inashangaza utawala wa magufuli damu zinaanza kumwagika tunaomba rais toa tamko naona kuna watu wanataka kuchafua utawala wako
 
Mleta mada bora ungekaa kimya tu mbona sisi wengine tunatafakari kimya kimya bila kuchochea chochote? Bandiko lako halina afya kwa Taifa.
 
Wewe Shetani Mkuu unayejificha (camouflager) kwa kujiita Malaika Mkuu unataka kutuambia kwamba Kamanda Mawazo jana ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwake kuonekana hadharani tangu uchaguzi Mkuu upite? Hao aliokuwa anafanya nao kikao cha ndani walikuwa ni wanachama wa chama gani?
 
Last edited by a moderator:
Very Sad !! Jamani HAKI..HAKI... Haki...Haki ipo wapi?!!? (JUSTICE for all) Nimesikitika kusoma.....uzi huu!!
 
toka nchi yetu ijikomboe kutoka kwa wakoloni,tumekuwa tukisema tanzania ni nchi yenye amani,utulivu,haki,upendo..mimi hayo maneno sikubaliani nayo hata kidogo.

uko wapi uhuru wa kuzungumza?uko wapi uhuru wa kuhoji?uko wapi uhuru wa kushiriki au kushirikishwa?iko wapi haki?iko wapi democrasia?uko wapi upendo??..KAMA TU

-tukihoji utawala tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishiriki harakati tunakuwa maadui zao
-tukiunga mkono wapinzani tunauzwa kuwa maadui zao
-tukidai haki zetu tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukiandika habari zinazowagusa tunageuzwa kuwa maadui zao
-tukishinda tunanya'ganywa ushindi
-tukishinda uchaguzi unafutwa.

"iko wapi HAKI ndugu zangu?,iko wapi DEMOCRASIA ndugu zangu?"... hivi hii TANZANIA ni ya nani?????????hivi kuna mwenye hati miliki juu ya nchi hii..???

1.ikoo wapi HAKI juu ya kifo cha DR.MVUNGI aliyekuwa kamishna wa tume ya mabadiliko ya katiba baada ya kuvamiwa kwake kimara na kujeruhiwa na watu wasiojulikana na hatimaye mauti yakamkuta akiwa hospitali.

2.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa DK.ULIMBOKA aliyetekwa na kutolewa meno,kupigwa nondo,kukatwa na mapanga kisa tu kutetea haki za madaktari.

3.iko wapi HAKI juu ya umwagiwaji wa tindi kali kwa mwandishi na mtafiti mahiri SAED KUBENEA?

4.iko wapi HAKI juu ya utekwaji wa KAMANDA MAWAZO na hitimaye kukatwa katwa mapinga na baada ya siku moja akafariki...???

IKO WAPI HAKI,UKO WAPI UHURU,IKO WAPI DEMOCRASIA,UKO WAPI UPENDO NDUGU ZANGU????....KIUKWELI INAUMA SANA BWANA,HII NCHI NI YETU SOTE NA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI JUU YA TANZANIA,KWANINI WANATUFANYIA HIVI LAKINIIIIIII???????
 

Attachments

  • 1447572821313.jpg
    1447572821313.jpg
    92.5 KB · Views: 135
Divide n' Rule hata wao hawatakuwa salama
Na naona wafuasi na viongozi wao wanafurahia haya matendo haramu kwa kudhani kwamba wao wako salama.Wamewageuza Watanzania kama Nyumbu ambao mwenzao anakamatwa na kuliwa na Simba halafu wengine wanaendelea na taratibu za maisha kana kwamba kilichotokea ni jambo la kawaida lisilo na athari za kimaisha.Wanashindwa katambua ya kwamba unapotajwa kuwa kiongozi wa Tanzania moja ya dhamana kubwa uliyo nayo ni kulinda uhai wa kila Mtu awe Mtanzania au yeyote aliyomo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Wewe mtoa post ni pimbi wa kienyeji,unaongea kama unakabwa,usihamishe maada kirahis namna hiyo bila ya kutafuta asili ya Tukio,sisi tulioko huku mbona hatufikirii hivyo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom