Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa ahamasisha Mbowe, Zitto na wengine wanaoikwamisha Serikali 'washughulikiwe'

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa ahamasisha Mbowe, Zitto na wengine wanaoikwamisha Serikali 'washughulikiwe'

Akiwa Arusha katika mkutano ukumbi wa AICC Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James alitoa maelekezo ya kuwashambulia wapinzani wanaoibeza serikali.

Kwa akili yake wapinzani wajibu wao ni kuisifia serikali.

Hata kama Lissu anasema tusameheane, lakini tukio LA Jana kumshambulia Mbowe ni kutokana na hoja hizi hadharani na hatua hazichukuliwi. Lazima hawa tuje tuwawajibishe ili liwe fundisho

 
Mimi nina mashaka Inawezekana hizi ni njama ndani ya chama kumpoteza Mbowe ili kuwapokonya watu wa Kilimanjaro Chama
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Mbowe amekua mtu wa busara busara nyiiiiingi hata mahali zisipohitajika/anapoonewa tofauti kabisa na Kina Lema na yule mbunge wa kule Nyamongo ambao wao ni watu wa misimamo kama ni mbaya iwe mbaya tu.

Mbowe akitoka hosp. Nadhani atapunguza zile busara busara zake ambazo hua zinapelekea kuonewa bila mpango.
 
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Heri James amewalaumu vijana wa CCM Tanzania kuwaacha wanasiasa wa upinzani Zitto Kabwe na Freeman Mbowe wakitembea mitaani bila kubughudhiwa/kushambuliwa kwa madai kuwa wanataka kulipasua taifa kwa vitendo vyao vya kuhujumu Serikali na Taifa

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Kenani Kihongosi amesema wapinzani wanaoichafua Serikali wanapaswa kukosolewa au Kuuawa kabisa.

UPDATE: Katibu Mkuu wa CCM amekemea kauli hizi > Dr Bashiru aonya kauli tata za makada wa CCM, ni zile za kuwatisha wapinzani!
Tayari mambo yameanza
 
Wanatekeleza ilani ya chama na maagizo ya rais kuhusu upinzani
 
Wako punguani wanasema tukio la Mbowe kuvamiwa na kupigwa ni "cheche" za ndani, wanaleta hisia wakati kuna uthibitisho wa aina hii wanajidai hawauoni.

Mna laana.
 




Freeman Mbowe kapoteza vingi sana katika kipindi cha miaka 5; biashara, marafiki na sasa wamemvunja mguu… binafsi sijawahi kusikia hata kauli moja ya Mbowe akimtusi mtu… kinachosikitisha zaidi ni kwamba viongozi wa upinzani bungeni wanaishi kwenye makazi rasmi sio uchochoroni.

Tunaposema ubaguz upo kila sehemu duniani hii ndiyo maana yake. Bora ubaguzi wa mzungu kuliko wa mtu mweusi. Mtu mweus anakubagua, anakunyanyasa, anakufilisi, anakufunga kwa kesi za uwongo. Ukipona uko anaamua kukuvamia akuue ili upotee kabisa. Ssa wale watu maarufu wapase sauti.

Freeman Mbowe Hakuwa Na Walinzi Wake Kwasababu Waliondolewa Kipindi Cha Sakata La Corona, Sasa Wakati Anapanda Ngazi Wakashuka Watu Watatu Wakamuambia Wewe Unaisumbua Sana Serikali, Sasa Sisi Hatuna Mpango Wa Kukuua Ila Tunataka Tukuvunje Ili Ushindwe Kufanya Kampeni.
 
Mtu akimbeza Rais ...kwani MBOWE AMEMBEZA RAIS?
 
Back
Top Bottom