Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wafungwa wengine wewe kijambio kikuwasheHapo hamna anayefunga bali wanashinda njaa tu
Ukiwa umefunga kula mchana mzima hata kiwango cha inslin mwilini pia inakuwa chini sana. Sukari ni rahisi sana kumeng'enywa, kuchakatwa na kufyonzwa mwilini kwa wingi kwa wakati mmoja (bolus), hali hii inapeleka sukari nyingi kwenye damu kwa muda mfupi harakaharaka wakati kiwango cha insulini mwilini kiko chini sana. Sukari nyingi kwenye damu itakaa kwenye damu bila kuchakatwa kwa muda, lakini baadae inakwenda kusababisha kongosho kuzalisha inslin nyingi sana (shooting) bila idadi ili kuhangaika na wingi wa sukari mwilini. Hali hii inaweza kusaababisha kisukari cha muda (Post prandial) effects. Insulin ikiwa nyingi sana kwenye mzunguuko kutasababisha glukose nyingi kwa wakati mmoja ihamishwe kwenye damu kwenda kwenye tissues.Asante,ila swali kwa nin juice au uji usio na sukari,tupe somo sukari inaleta uharibifu gani ukianza nayo? Najua sukari siyo nzr ikizidi ila fafanua Hapo kidogo
Àsante kwa hii elimu.Endelea kunywa uji wa aina moja ya nafaka, kama unakunywa mtama kunywa mtama leo, kama kesho unapenda ulezi kunywa ulezi kesho na kama kesho kutwa utapenda kunywa uji wa mchele kunywa mchele tu. Hii ni kwasabu, kila nafaka na kila aina ya chakula kinahitaji mazingira yake binafsi huko tumboni ili imeng'enywe na kufyonzwa mwilini. Mtama na mahindi kila kimoja kina maumbile tofuti mbele mimeng'enyo na mazingira ya tumboni. hivyo unapovichanganya pamoja kwenye mlo mmoja unakwenda kuutatizo mfumo wa usagaji wa chakula. Hivyohivyo, kama ukichanganya nyama na nafaka kwenye mlo mmoja utasababisha shida kubwa sana kwenye umeng'enyaji wa nyama na nafaka kwa wakati mmoja, maana nyama na nafaka vinahitaji mazingira na mimeng'enyo tofauti.
UKivichanganya yafuatayo yanaweza yakatokea:
1. chakula kushindwa kusangwa kwa ufasaha tumboni, hii itasababisha
2. chakula kuchelewa sana tumboni bila kusangwa, hii itasababisha
3. Chakula kuoza (ferment) na kuzalisha gesi nyingi tumboni (mashuzi), hii itasababisha
4. chakula kuchelewa kufika kwenye utumbo mdogo kwaajili ya kuendelea kusagwa na kufyonzwa mwilini, hii itasababisha
5. Chakula kuchelewa kufika kwenye utumbo mpana kama makapi na uvyonzwaji wa maji na chumvichuvi kurudi mwilini, hii itasababisha
6. Chakula kukaa sana kwenye mfumo wa chakula, hii inasababisha
7. maji mengi kwenye makapi ya chakula kilichooza sana na harufu kali na sumu kunyonywa kwenda mwilini, hii inasababisha
8. Mtu kuchelewa kupata haja kubwa na haja kubwa kuwa kavu sana (constipation), hii husababisha
9. Mtu kupata magonjwa kama constipation, cancer ya utumbo, bawasili na mzio (allergies )
Tumbo ni hilohilo moja na vyakula vyote vinakwenda hukohuko kwenye tumbo hili. Hicho ndio chanzo cha matatizo yetu. Kila aina ya chakula inahitaji aina tofauti ya mimeng'enyo (enzymes) na mazingira tofauti ili kimeng'enywe kwa ufasaha. Mfano, vyakula vya protein vinahitaji mazingira ya uchachu mwingi (acidic) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri, lakini mahindi (carbohydrates) usagaji wake tumboni hauhitaji acid kali (alkalinity) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri. Sasa kama utachanganya nyama, ugali, matunda, maziwa pamoja kwenye chakula chako na maji ya kunywa wakati huohuo lazima utapata shida tuuu iwe unajuwa au hujui.Mie nauliza hii mambo ya kusema usichanganye chakkula hiki au kile kwani utumbo nao una compartments za aina tofauti za vyakula? Meanning vyakula tumbni havichanganyiki?
Sasa nakulaje ugali bila nyama mzeya mbona kama watupiga kambaTumbo ni hilohilo moja na vyakula vyote vinakwenda hukohuko kwenye tumbo hili. Hicho ndio chanzo cha matatizo yetu. Kila aina ya chakula inahitaji aina tofauti ya mimeng'enyo (enzymes) na mazingira tofauti ili kimeng'enywe kwa ufasaha. Mfano, vyakula vya protein vinahitaji mazingira ya uchachu mwingi (acidic) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri, lakini mahindi (carbohydrates) usagaji wake tumboni hauhitaji acid kali (alkalinity) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri. Sasa kama utachanganya nyama, ugali, matunda, maziwa pamoja kwenye chakula chako na maji ya kunywa wakati huohuo lazima utapata shida tuuu iwe unajuwa au hujui.
Kule nyama peke yakee kama wanavyofanya wamasai, simba, na mbwa kama unaweza. changanya/Kula ugali na maharagwe, kunde, njegele, na jamii zote za mikunde. Kula matunda peke yake, kunywa maziwa peke yake.Àsante kwa hii elimu.
Sasa shida ni je tufanyeje kwa vyakula kama nyama maana tuliisha zaea kula nyama kwa kuichanganya na vyakula vingne. Je tuwe tuna kula pekee pasipo kuchanganya chakula chochote (yan tusiifanye kama mboga bali iwe chakula kikuu kinacho jitosheleza)?
nafahamu kuwa watu tumekuta halimiko hivyo ya ugali na ng'ombe lakini pia tumekuta watu wakilalamika kutopata choo kwa siku nzima, kupata choo kigumu, kuapata bawasili, kanza za utumbo mpana, kujambia sana watu na wengine kulalamika kupata fungus na kuwashwa mwili mara kwa mara. uwamuzi ni wao.Sasa nakulaje ugali bila nyama mzeya mbona kama watupiga kamba
Aya bana ila hapo mzee msosi uwe wa aina moja hapana ..tumbo wacha lipokee mixer ya ugali nyama na mtindinafahamu kuwa watu tumekuta halimiko hivyo ya ugali na ng'ombe lakini pia tumekuta watu wakilalamika kutopata choo kwa siku nzima, kupata choo kigumu, kuapata bawasili na wengine kulalamika kupata fungus na kuwashwa mwili mara kwa mara. uwamuzi ni wao.
Vipatie nafasi mkuu kama unaweza angalau mpishano wa dakika 45.Aya bana ila hapo mzee msosi uwe wa aina moja hapana ..tumbo wacha lipokee mixer ya ugali nyama na mtindi
Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?Vipatie nafasi mkuu kama unaweza angalau mpishano wa dakika 45.
Mfano, wako watu wanasema kuwa nguruwe ni haram, hii sio kweli, ukweli ni kwamba ngurumwe ana sumu nyingi mwilini mwake, hafai kuliwa na kila mtu na watu wote. Sababu kubwa ya nguruwe kuwa na sumu ni kwasababu nguruwe anachanganya vyakula, nyama, majani, mahindi, matunda, maganda na kila kitu kwa wakati mmoja. mwili unashindwa kuvisaga vyakula vyote kwa wakati mmoja kwa haraka na kusababisha chakula kuoza tumboni na kufyonza sumu. Huwezi kula maini na utumbo wa nguruwe hivihivi. Watu wote wanaokula nyama nyingi ya nguruwe hawataishi miaka mingi kwa raha.
Hata binadamu kama atachanganya pamoja ugali, nyama, mboga za majani, ndimu, kachumbali, matikiti maji, na maziwa kwenye mlo mmoja mwili wake utafanana na nguruwe. mwili wake unajaa sumu nyingi.
Hawa hawana elimu hiyo ya food combinations, lakini pia shida iko kwa walaji. Ukikuta buffet maana yake "chagua kati ya hivi" haimaanishi "pakua vyote hivi"Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?
Mbona sasa mie nikigonga menu za hapo ndio napata choo vizuri tena kama nikila like siku tatu mfululizo choo nakipata kama clock work vile saa mbili na dakila 20 eveyday nakata gogo. Ila sasa nikila wali maharage ndio inapita siku tatu hamna choo. Wee jamaaa unatuzinguaHawa hawana elimu hiyo ya food combinations, lakini pia shida iko kwa walaji. Ukikuta buffet maana yake "chagua kati ya hivi" haimaanishi "pakua vyote hivi"
Kwaiyo hapa ata smooth sio nzuri kiafya pia?Kule nyama peke yakee kama wanavyofanya wamasai, simba, na mbwa kama unaweza. changanya/Kula ugali na maharagwe, kunde, njegele, na jamii zote za mikunde. Kula matunda peke yake, kunywa maziwa peke yake.
Hawa kazi Yao kubwa kwa mteja ni delicious foods, ni juu yako mteja kumwambia mpishi akuletee na kukutayarishia chakula gani na akitayarishe vipi.Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?
Ah wee acha zako bwana kwenye hizi five star hotels wana wataalam hadi wakuwapikia high perfomance athletes na tunaona kabisa wanachanganya carb na protein na vegetables kwenye mlo mmojaHawa kazi Yao kubwa kwa mteja ni delicious foods, ni juu yako mteja kumwambia mpishi akuletee na kukutayarishia chakula gani na akitayarishe vipi.
Nilidhani faida namba moja ni msamaha toka kwa MunguKuna Kwaresima na Ramadhan miezi ambayo waumini wa Kikristo na Kiislam wanafunga kama sehemu ya imani zao kwa lengo la kumpendeza Mungu wao ili awasamehe dhambi au awape kibali cha kuingia peponi. Kwenye upande huu wa dini sintakuongelea zaidi kwakuwa imani ya mtu ni package ambayo haiko wazi kujadiliwa wa kukosolewa na mtu mwingine. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Ukristo na Uisilam ni dini ambazo chimbuko lao ni Asia ya Kati, watu ambao wana mazingira, tabia, vyakula, utamaduni na bila shaka na magonjwa yanayofanana. Kufunga ilikuwa ni njia yao ya kuzuia (primary prevention) na kutibu (secondary prevention) magonjwa fulani fulani kwenye jamii zao. Njia hii ya kufunga kuacha kula chakula haifanyi kazi ya kukinga na kutibu magonjwa kwa wayahudi na waarabu tu bali hata kwa viumbe vyote vya mwenyezimungu ili vipate maisha marefu na afya tele.
Kufunga kula chakula kunasaidiaje kukinga na kutibu magonjwa kwa binadamu?
1. Kwa kukausha/kuchoma/kutumia mafuta mabaya yaliyozidi mwilini: Miili yetu ina tabia ya kuhifadhi vyakula vya ziada tunavyokula ili mwili wako ivitumie vyakula hivyo siku utakapokosa chakula. Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, chai na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu vinapoliwa kwa wingi kuliko mahitaji ya siku ya mwili huwa ziada inahifadhiwa ndani ya mwili kama sukari (glucose, fructose na galactose) kwa matumizi ya mwili ya sasa hivi na baadae kidogo kama masaa 4 kama utakuwa hujakula chakula kingine, lakini kama baada ya masaa 4 utaendelea kula chakula kingine na kupata glucose mpya mwili utageuza ile glucose/fructose/galactose ya kwanza kuwa glycogen, aina ya sukari ambayo ni ngumu kidogo mwili kuitumia kuliko glucose; glycogen inatakiwa itumike kutia nguvu mwili kama glucose iliyopo imekwisha mwilini. Lakini, Kama mtu ataendelea na kula kula kula chakula kuliko mahitaji ya mwili, mwili wake utaigeuza ile glycogen inayohifadhiwa kuwa mafuta (lipids). Hivyo mafuta yanayopatikana kwa kula ziada ya Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, artificial juices na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu yanaungana mwilini na mafuta mengine unayoongeza kwenye chakula kama vile mafuta ya mbegu za mimea (nazi, kweme, ufuta, alizeti, mahindi, mawese, pamba, korie, nk) pamoja na mafuta uliyokula yenye asili ya wanyama (jibini, siagi, nyama zilizonona, senene, kumbikumbi, nk) kutengeneza tabaka kubwa la mafuta (adipose tissue) mwilini, hivyo kusababisha mwili kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kuliko mahitaji ya mafuta yanayohitajika kwa kazi za mwili.
Changamoto za kuwa tabaka kubwa la mafuta mwilini:
Mafuta haya mwili unayahifadhi kwenye vioungo na sehemu mbalimbali za mwili kama vile tumbuni (vitambi), matakoni (wowowo), mapajani, shingoni, mikononi, misuli na kwenye ngozi. Kama sehemu zote hizi zikijaa mwili utayatafutia mafuta yako sehemu nyingine za kuyahifadhi kama vile kwenye utumbo, moyo, ndani ya mishipa ya damu, via vya uzazi, mafigo, ini na kila sehemu yenye nafasi, haiyatupi maana mwili hautupi chakula.
Kusudi kubwa la mwili wako kugeuza chakula chako cha ziada ulichokula kuwa mafuta na kuyahifadhi ni ili mwili wako uweze kuyatumia mafuta hayo kutoa nishati ya kusukuma mwili KAMA mwili wako utakosa chakula kwa muda mrefu (starvation), hivyo mtu mwenye mafuta mengi mwilini anaweza kuishi hata siku 30 bila kula chakula bila kufa. Katika kipindi hicho mwili utayaunguza/unayafagia/unayapakua/unayatumia mafuta yote ili kupata chakula.
Hivyo, changamoto za kutunza mafuta hayo mwilini ni mapoja na:
1. Kuongezeka uzito kuliko uwezo wa misuli yako (mifupa, tendons, muscles) inavyoweza kubeba.
2. Kuminya mishipa ya damu na fahamu, hii inasababisha presha na ganzi kwenye mikuu, mikono au kwenye makalio.
3. Kupunguza kiwango cha maji mwilini, Mtu mwenye mafuta mengi (mnene) ana kiwango kidogo cha maji.
4. Kupunguza tundu (lumen) la mishipa ya damu na kusababisha kupata ugonjwa wa pressha (high blood pressure, kiharusi)
5. Kupunguza kiwango cha dawa kutibu magonjwa (lazima dose yako iwe kubwa kuliko kawaida)
6. Kupunguza uwezo wa kongosho (pancrease) kutoa insulin na insulin kushindwa kuchakata chakula unachokula na kusababisha kupata ugonjwa wa Kisukari (diabetes)
7. Kupunguza nguvu za kiume
8. Kupumua kwa shida na kukoroma sana usingizini
9. Kupata ugumba na utasa
10. Kutembea kwa shida na miguu kupata maumivu
11. Kinga ya mwili kushuka
12. Kuongeza uwezekano wa kupata kansa (cancer) ya matiti, utumbo, ngozi, mfumo wa uzazi na viungo vingine.
13. Siku mafuta yaliyoko ndani ya mishipa ya damu yakimeguka na kuzunguuka pamoja na damu ndani ya mishipa yanaweza kwenda kuziba mishipa midogo midogo mwilini na kusababisha kiharusi au moyo kusimama kutegemea bonge la mafuta limeenda kukwamia wapi na kwenye kiungo gani.
Faida za kufanga ni zipi?
Kufunga kula chakula ni muhimu sana kwa kila mtu, sio kwaajili ya kwenda mbinguni tu, lakini kwa
1. kuzuia na kuponya magonjwa yote hayo niliyoyasema hapo juu kwa mwili kuyafagia mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa.
2. Ini, tumbo, utumbo, kongosho na nyongo (bile) ndivyo vinavyofanya kazi kubwa ya kuchakata chakula na mafuta, hivyo kufunga kula chakula kutasaidia viungo hivyo kurudisha afya yake (kupunzika na kupona majeraha na uchovu)
3. Mafuta yakipungua magonjwa yote hayo yatapotea ghafla bin vuu.
4. Kufunga kunaongeza uwezo wako wa kufikiri, kutafakari na kuzingatia (focus). Hii inasaidia kwenye kutatua shida na migogoro na mahusiano yako na watu wengine kwa kumaanisha.
Hivyo kufunga sio tu ni ibada lakini ni tiba kamili kwa viumbe, usisubiri mpaka Ramadhan na Kwaresma ndipo ufunge, unakosa mengi sana,
Namna ya kufunga:
Hakikisha kuwa unafunga kula chakula na vinywaji vyenye sukari, sio kama wengine wanavyosema kuwa wamefunga kusema uongo, sijui kuseng'enya na nini, Kufunga ni kuacha kula chakula kwa masaa 12. Unaweza kunywa maji tu kwa wanaofunga kwajili ya afya ya magonjwa haya.
1,Wakati wa kufungua jioni hakikisha kuwa huli vyakula viiiingi na vyenye mafuta mengi kama wengine wanavyofanya wakati wa kufungua. Kunywa maji mengi na matunda zaidi ukishafungua jioni na baada ya nusu saa ndio ule vyakula vingine vya kawaida.
2. Usile daku alfajiri ili kupunguza ukali wa njaa, hapo utakuwa umejidanganya mwenyewe, kula kama kawaida yako.
3. Anza kufungua kwa kula vitu vyepesi kama maji, matunda, juice isiyokuwa na sukari, au uji usiokuwa na sukari. Epuka soda na vitu vitamu sana kama halua.
4. Usichanganye nyama na carbohydrates kwenye mlo mmoja, usichanganye matunda na chakula pamoja, usichanganye maziwa na chakula kwenye mlo.
5. Fanya mazoezi, fanya kazi, usilale wakati umefunga ili kupata ubora wa kufunga.
6. Wakati umefunga jaribu tena kuTatua migogoro iliyokushinda huko nyuma utaona maajabu makubwa.
Hawa Wayahudi na Waarabu nina uhakika elimu hii ya kufunga kwa afya walikuwa nayo tangu siku nyingi ndio maana ukawa utamadini wao ukaingizwa kwenye dini, tuwapigie makofi mengi.
.Kama una swali niulize, nimejikita kwenye sayansi za afya sio kwenye dini ya huyu wala yule, samahani, msinipige mawe.
Kaka binadamu anatakiwa kupata haja kubwa sio chini ya mara 3 kwa siku yenye massa 24 maana chakula kinatakiwa kuchukua sio zaidi ya massa 4 TU kutoka kuingia mdomoni hadi kufika kwenye kinyeo, ukiona sio hivyo umekosra kula.Mbona sasa mie nikigonga menu za hapo ndio napata choo vizuri tena kama nikila like siku tatu mfululizo choo nakipata kama clock work vile saa mbili na dakila 20 eveyday nakata gogo. Ila sasa nikila wali maharage ndio inapita siku tatu hamna choo. Wee jamaaa unatuzingua