Mwezi wa Ramadhan: Zifahamu faida za kisayansi za kufunga kula chakula wasizozifahamu wafungaji

Mwezi wa Ramadhan: Zifahamu faida za kisayansi za kufunga kula chakula wasizozifahamu wafungaji

Unajidanganya mwenyewe kaka, hata mbuzi, Kuku, ng'ombe, sungura, nk unapotaka kuwanenepeaha unawatoa kwenye mlo wao wa asili na kulivuruga tumbo lao kwa kuwapa vyakula mchanganyiko. Ukila hivyo utapona TU kama utafanya mazoezi mazito ya gym, boxing, riadha,nk. Vinginevyo after 40 you will notice the difference.
Ah sasa kam mpaka forty ndio madhara yanakuwa basi hapo umenidhibitishia kuwa hizi somjo. Mtu nina 42 nagonga mbususu vilivyo tena double double na nakimbia 5km mara tatu kwa wiki.
Mzeya each one is unique
 
Endelea kujidanganya, huwezi kwenda haja kubwa mara moja kwa siku halafu ujiite una afya njema ya kufa mtu, nonsense.
 
Endelea kujidanganya, huwezi kwenda haja kubwa mara moja kwa siku halafu ujiite una afya njema ya kufa mtu, nonsense.
Wee bwana ingekuwa hivyo watu wangekufa na miaka 20...tena africa ndio ata miaka mitatu tusingefika
 
Kuna Kwaresima na Ramadhan miezi ambayo waumini wa Kikristo na Kiislam wanafunga kama sehemu ya imani zao kwa lengo la kumpendeza Mungu wao ili awasamehe dhambi au awape kibali cha kuingia peponi. Kwenye upande huu wa dini sintakuongelea zaidi kwakuwa imani ya mtu ni package ambayo haiko wazi kujadiliwa wa kukosolewa na mtu mwingine. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Ukristo na Uisilam ni dini ambazo chimbuko lao ni Asia ya Kati, watu ambao wana mazingira, tabia, vyakula, utamaduni na bila shaka na magonjwa yanayofanana. Kufunga ilikuwa ni njia yao ya kuzuia (primary prevention) na kutibu (secondary prevention) magonjwa fulani fulani kwenye jamii zao. Njia hii ya kufunga kuacha kula chakula haifanyi kazi ya kukinga na kutibu magonjwa kwa wayahudi na waarabu tu bali hata kwa viumbe vyote vya mwenyezimungu ili vipate maisha marefu na afya tele.

Kufunga kula chakula kunasaidiaje kukinga na kutibu magonjwa kwa binadamu?

1. Kwa kukausha/kuchoma/kutumia mafuta mabaya yaliyozidi mwilini: Miili yetu ina tabia ya kuhifadhi vyakula vya ziada tunavyokula ili mwili wako ivitumie vyakula hivyo siku utakapokosa chakula.

Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, chai na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu vinapoliwa kwa wingi kuliko mahitaji ya siku ya mwili huwa ziada inahifadhiwa ndani ya mwili kama sukari (glucose, fructose na galactose) kwa matumizi ya mwili ya sasa hivi na baadae kidogo kama masaa 4 kama utakuwa hujakula chakula kingine, lakini kama baada ya masaa 4 utaendelea kula chakula kingine na kupata glucose mpya mwili utageuza ile glucose/fructose/galactose ya kwanza kuwa glycogen, aina ya sukari ambayo ni ngumu kidogo mwili kuitumia kuliko glucose; glycogen inatakiwa itumike kutia nguvu mwili kama glucose iliyopo imekwisha mwilini. Lakini, Kama mtu ataendelea na kula kula kula chakula kuliko mahitaji ya mwili, mwili wake utaigeuza ile glycogen inayohifadhiwa kuwa mafuta (lipids).

Hivyo mafuta yanayopatikana kwa kula ziada ya Ugali, ubwabwa, viazi, majimbi, ngano, mihogo, soda, artificial juices na vyakula vyote vya kutia mwili nguvu yanaungana mwilini na mafuta mengine unayoongeza kwenye chakula kama vile mafuta ya mbegu za mimea (nazi, kweme, ufuta, alizeti, mahindi, mawese, pamba, korie, nk) pamoja na mafuta uliyokula yenye asili ya wanyama (jibini, siagi, nyama zilizonona, senene, kumbikumbi, nk) kutengeneza tabaka kubwa la mafuta (adipose tissue) mwilini, hivyo kusababisha mwili kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta kuliko mahitaji ya mafuta yanayohitajika kwa kazi za mwili.

Changamoto za kuwa tabaka kubwa la mafuta mwilini:

Mafuta haya mwili unayahifadhi kwenye vioungo na sehemu mbalimbali za mwili kama vile tumbuni (vitambi), matakoni (wowowo), mapajani, shingoni, mikononi, misuli na kwenye ngozi. Kama sehemu zote hizi zikijaa mwili utayatafutia mafuta yako sehemu nyingine za kuyahifadhi kama vile kwenye utumbo, moyo, ndani ya mishipa ya damu, via vya uzazi, mafigo, ini na kila sehemu yenye nafasi, haiyatupi maana mwili hautupi chakula.

Kusudi kubwa la mwili wako kugeuza chakula chako cha ziada ulichokula kuwa mafuta na kuyahifadhi ni ili mwili wako uweze kuyatumia mafuta hayo kutoa nishati ya kusukuma mwili KAMA mwili wako utakosa chakula kwa muda mrefu (starvation), hivyo mtu mwenye mafuta mengi mwilini anaweza kuishi hata siku 30 bila kula chakula bila kufa. Katika kipindi hicho mwili utayaunguza/unayafagia/unayapakua/unayatumia mafuta yote ili kupata chakula.

Hivyo, changamoto za kutunza mafuta hayo mwilini ni mapoja na:

1. Kuongezeka uzito kuliko uwezo wa misuli yako (mifupa, tendons, muscles) inavyoweza kubeba.
2. Kuminya mishipa ya damu na fahamu, hii inasababisha presha na ganzi kwenye mikuu, mikono au kwenye makalio.
3. Kupunguza kiwango cha maji mwilini, Mtu mwenye mafuta mengi (mnene) ana kiwango kidogo cha maji.
4. Kupunguza tundu (lumen) la mishipa ya damu na kusababisha kupata ugonjwa wa pressha (high blood pressure, kiharusi)
5. Kupunguza kiwango cha dawa kutibu magonjwa (lazima dose yako iwe kubwa kuliko kawaida)
6. Kupunguza uwezo wa kongosho (pancrease) kutoa insulin na insulin kushindwa kuchakata chakula unachokula na kusababisha kupata ugonjwa wa Kisukari (diabetes)
7. Kupunguza nguvu za kiume
8. Kupumua kwa shida na kukoroma sana usingizini
9. Kupata ugumba na utasa
10. Kutembea kwa shida na miguu kupata maumivu
11. Kinga ya mwili kushuka
12. Kuongeza uwezekano wa kupata kansa (cancer) ya matiti, utumbo, ngozi, mfumo wa uzazi na viungo vingine.
13. Siku mafuta yaliyoko ndani ya mishipa ya damu yakimeguka na kuzunguuka pamoja na damu ndani ya mishipa yanaweza kwenda kuziba mishipa midogo midogo mwilini na kusababisha kiharusi au moyo kusimama kutegemea bonge la mafuta limeenda kukwamia wapi na kwenye kiungo gani.

Faida za kufanga ni zipi?
Kufunga kula chakula ni muhimu sana kwa kila mtu, sio kwaajili ya kwenda mbinguni tu, lakini kwa
1. kuzuia na kuponya magonjwa yote hayo niliyoyasema hapo juu kwa mwili kuyafagia mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa.
2. Ini, tumbo, utumbo, kongosho na nyongo (bile) ndivyo vinavyofanya kazi kubwa ya kuchakata chakula na mafuta, hivyo kufunga kula chakula kutasaidia viungo hivyo kurudisha afya yake (kupunzika na kupona majeraha na uchovu)
3. Mafuta yakipungua magonjwa yote hayo yatapotea ghafla bin vuu.
4. Kufunga kunaongeza uwezo wako wa kufikiri, kutafakari na kuzingatia (focus). Hii inasaidia kwenye kutatua shida na migogoro na mahusiano yako na watu wengine kwa kumaanisha.

Hivyo kufunga sio tu ni ibada lakini ni tiba kamili kwa viumbe, usisubiri mpaka Ramadhan na Kwaresma ndipo ufunge, unakosa mengi sana,

Namna ya kufunga:
Hakikisha kuwa unafunga kula chakula na vinywaji vyenye sukari, sio kama wengine wanavyosema kuwa wamefunga kusema uongo, sijui kuseng'enya na nini, Kufunga ni kuacha kula chakula kwa masaa 12. Unaweza kunywa maji tu kwa wanaofunga kwajili ya afya ya magonjwa haya.

1.Wakati wa kufungua jioni hakikisha kuwa huli vyakula viiiingi na vyenye mafuta mengi kama wengine wanavyofanya wakati wa kufungua. Kunywa maji mengi na matunda zaidi ukishafungua jioni na baada ya nusu saa ndio ule vyakula vingine vya kawaida.
2. Usile daku alfajiri ili kupunguza ukali wa njaa, hapo utakuwa umejidanganya mwenyewe, kula kama kawaida yako.
3. Anza kufungua kwa kula vitu vyepesi kama maji, matunda, juice isiyokuwa na sukari, au uji usiokuwa na sukari. Epuka soda na vitu vitamu sana kama halua.
4. Usichanganye nyama na carbohydrates kwenye mlo mmoja, usichanganye matunda na chakula pamoja, usichanganye maziwa na chakula kwenye mlo.
5. Fanya mazoezi, fanya kazi, usilale wakati umefunga ili kupata ubora wa kufunga.
6. Wakati umefunga jaribu tena kuTatua migogoro iliyokushinda huko nyuma utaona maajabu makubwa.

Hawa Wayahudi na Waarabu nina uhakika elimu hii ya kufunga kwa afya walikuwa nayo tangu siku nyingi ndio maana ukawa utamadini wao ukaingizwa kwenye dini, tuwapigie makofi mengi.

Kama una swali niulize, nimejikita kwenye sayansi za afya sio kwenye dini ya huyu wala yule, samahani, msinipige mawe.
♦️Hivyo kwa mujibu wa hili gazeti uliloandika ambalo limejaa maneno ya propaganda ya kidini wanazomezeshwa watoto wadogo unamaanisha

♦️Kwamba wanaofunga ndio wanaishi maisha marefu zaidi hapa Tanzania?

♦️Kwamba kwa faida hizo kedekede ambazo natambua kuwa 90% ya waislamu hufunga , hivyo waliojaa mahospitalini kwa magonjwa mbalimbali ni wasio waislamu pekee?
 
Wee bwana ingekuwa hivyo watu wangekufa na miaka 20...tena africa ndio ata miaka mitatu tusingefika
Sawa lakini ni kweli pia kuwa watu wanaopata magonjwa kansa, damu na moyo ni wengi sana pia, Ni kweli pia kuwa watu wanaokosa nguvu za kiume, kisukari na uzito mkubwa ni wengi, ni kweli pia kuwa watu wanaokufa ghafla ni wengi kwenye jamii. Inshallah na wewe iko siku utaungana nao. Kwani fomular ya kunenepesha kuku, ngurume, ng'ombe na wanyama wengine inafahamika kwa watu wengi, haitofautiani sana na namna unavyosema unakula wewe.
 
Mie mbona sijajinenepea hovyo mzeya...wee tukubaliane kutokukubaliana basi
 
♦️Hivyo kwa mujibu wa hili gazeti uliloandika ambalo limejaa maneno ya propaganda ya kidini wanazomezeshwa watoto wadogo unamaanisha

♦️Kwamba wanaofunga ndio wanaishi maisha marefu zaidi hapa Tanzania?

♦️Kwamba kwa faida hizo kedekede ambazo natambua kuwa 90% ya waislamu hufunga , hivyo waliojaa mahospitalini kwa magonjwa mbalimbali ni wasio waislamu pekee?

Hiyo ni ngumu kutoa hitimisho kuhusu hili lakini, Fanya utafiti wako mdogo utagundua kitu, Mfano, Mzee Mwinyi anafunga yupo, Mzee Kikwete anafunga nae yupo. Kifo kinaweza kusababishwa na mambo mengi lakini ulaji wa vyakula na mtindo wa maisha vinachangia sana sana sana.
 
Mie mbona sijajinenepea hovyo mzeya...wee tukubaliane kutokukubaliana basi
kama hujanenepeana sana basi mshukuru mungu kuwa unachokula kinatumika chote kwa kazi za mwili, kama siku utashindwa kutumia chakula chote ulichokula basi rudi kwenye uzi huu upate majibu yako
 
Hiyo ni ngumu kutoa hitimisho kuhusu hili lakini, Fanya utafiti wako mdogo utagundua kitu, Mfano, Mzee Mwinyi anafunga yupo, Mzee Kikwete anafunga nae yupo. Kifo kinaweza kusababishwa na mambo mengi lakini ulaji wa vyakula na mtindo wa maisha vinachangia sana sana sana.
Kwa hiyo hao viongozi ndio wenye umri mkubwa kuliko watanzania wote?
 
Kwa hiyo hao viongozi ndio wenye umri mkubwa kuliko watanzania wote?
hapo nimetoa mfano/sample ndogo tu unaofahamika kwa wengi ambao hatutabishana sana. Lakini hata waislamu kuna wanaokula kizembe sana hata kama wanafunga. Lakini amini usiamini kula nyama na wanga pamoja, vinywaji baridi, sukari nyingi, chumvi n Mafuta ni kosa kubwa la kiafya
 
Ah sasa kam mpaka forty ndio madhara yanakuwa basi hapo umenidhibitishia kuwa hizi somjo. Mtu nina 42 nagonga mbususu vilivyo tena double double na nakimbia 5km mara tatu kwa wiki.
Mzeya each one is unique

‘Test your servants please, for ten days, and let us have vegetables to eat and water to drink. And then see how we look and how the boys look who are eating the king’s food, and on the basis of what you see decide what you do with your servants.’

Book of Daniel 1:12-16
 
Kwa hiyo nisile nyama ama?
 
Kwa hiyo hao viongozi ndio wenye umri mkubwa kuliko watanzania wote?
Naomba unitafutie wazee 3 tu mtaani kwako ambao wana miaka 70 wenye vitambi.

Mzee binadamu anamalizwa na ulaji mbaya wa vyakula, nyama, sukari, mafuta, chumvi na vinywaji baridi ndio adui mkuu wa afya na umri wake. Kumbuka hata wanyama porini wanaishi bila kuhudhuria hospitali kwakuwa hawachanganyi vyakula, hawali sukari, chumvi wala kunywa maji baridi.

Hata ng'ombe ukitaka anenepe na kuwa kuwa mgonjwa mchanganyie nyama, sukari, mashudu na majani kwenye chakula chake.
 
Wewe unaumwa au hujawahi kusafiri, nikupe kazi rahisi tengeneza safari ya vijiji vya kilamanjaro na Arusha , kule ambako nguruwe ndio nyama yao ya asili na vinjwaji vyao ni mbege na bia , tembelea kila nyumba yenye babu , uwaone kwanza walivyo , hutohitaji kuuliza umei wao, wapo wazee kibao wana miaka 120 + na wanadunda
 
Jibu maswali haya tafadhali

1. Je, Wanakula hiyo nyama ya nguruwe pamoja na ugali/wali?
2, Je, wanakula kila siku?
3. Je, baada ya kula wanakwenda kufanya kazi gani?
4, Je, wana vitambi?
5. Je, nguvu zao za kiume wanazo za kutosha? (waulize wake zao tafadhali swali hili ili upate ukweli)
6, Je, wanakula kiasi gani (kilo) hiyo nyama?
7. Je, wanakula na kunywa bia baridi kutoka kwenye friji?
 
Kwa hiyo nisile nyama ama?
Miili yetu haihitaji nyama kabisaam hata aina ya neno yetu (dental formula) sio ya kula nyama kama yale meno ya mbwa, paka, chui, duma, simba, fisi, mbweha, nk. Meno yetu na utumbo wetu sisi ni maalum kwa kula mihogo, matunda, mayai na nafaka tu baasi. Ndio maana tunashauri namna ya kula nyama kama unataka kula nyama.
 
Tupe ujuzi wa kula nyama maana hot chair choma mtamu balaa ukiweka na kuku choma ndio kabisaaa.
 
Tupe ujuzi wa kula nyama maana hot chair choma mtamu balaa ukiweka na kuku choma ndio kabisaaa.
Kiti moto haifai sio kwamba ni dhambi kuila, no. Ndio maana hata watu wa dini wameipiga ban na kuozingizia kuwa ni haramu au mapemo yamekimbilia kwenye nguruwe, nk. Ukweli ni kwamba nyama ya nguruwe Ina sumu nyingi sana, kutona na nguruwe kutokuchagua vyakula. Yaani anakula kila kitu nakusababisha mwili wake kijaa sumu.

Hata binadamu anaekula kila kitu yaani nyama , ubwabwa, mayai, majani, sukari, mafuta, vitunguu, soda, bia na maji baridi hapohapo mwili wake unabeba sumu nyingi sana. Mtu anaekula hivyo kwanza mwili wake unafubaa, unawasha, allergies, una fungus na jasho lenye harufu mbaya sana. Yaani ni kama mzoga unaotembea.

Kama unataka kula kiti moto angalau basi choma kwenye jiko ili mafuta na serum na majimaji mengine yadondoke. Yaani usiroast au kupikia. Hata kama unataka kula nyama ya ng'ombe chagua nyama ambayo imening'inizwa kwa muda mrefu kudondosha damu na majimaji yake, yaani nenda kanunue nyama jioni Chama iliyochinjwa asubihi.

Kula nyama bila kuongeza chumvi Wala kula na ugali. Fakamia nyama yenyewe TU bila chakula, kula nyama ya kuchoma usinywe mchuzi/supu. Wazee wetu walikuwa wanachoma au kuaniaka nyama juani hadi itoke maji yote ndio wanakula.
 
Sawa nimekupata wacha sasa nikaweke oda yangu ya kitimoto choma na sprite baridi sana
 
CHAKula kinaliwa hivi, asubihi kingi sana, mchana kidogo na usiku kidogo sana. Vingi wa chakula Utategemea mahitaji Ya mwili: umri, kazi na Afya ya mlaji. Hata hivyo mwili unahitaji makundi 6 ya vyakula kila siku ambayo ni vyakula vya kutia mwili nguvu, kujenga mwili, kulinda mwili, kulainisha haja kubwa (roughage), mafuta, na Maji Safi ya kunywa. Hakikisha kuwa makundi yote haya unayapata Kila siku. Cha kuzingatia tu usichanganye PAMOJA NYAMA NA UGALi/CHAPATI/UBWABWa/Magimbi, nk, Matunda yaliwe kwenye tumbo tupu, maziwa yanywewe YENYEWE tu kwa wakati wake. Mpangilio utaujuwa wewe.
Nashukuru kwa Muongozo huu...Ngija nikaongeze madini kwa Dr Sebi (The Geniuous of Human Health aliyewatingisha Wamarekani na Big Pharmaceutical Industries)..
 
Back
Top Bottom