Mwezi wa Ramadhan: Zifahamu faida za kisayansi za kufunga kula chakula wasizozifahamu wafungaji

Asante,ila swali kwa nin juice au uji usio na sukari,tupe somo sukari inaleta uharibifu gani ukianza nayo? Najua sukari siyo nzr ikizidi ila fafanua Hapo kidogo
Ukiwa umefunga kula mchana mzima hata kiwango cha inslin mwilini pia inakuwa chini sana. Sukari ni rahisi sana kumeng'enywa, kuchakatwa na kufyonzwa mwilini kwa wingi kwa wakati mmoja (bolus), hali hii inapeleka sukari nyingi kwenye damu kwa muda mfupi harakaharaka wakati kiwango cha insulini mwilini kiko chini sana. Sukari nyingi kwenye damu itakaa kwenye damu bila kuchakatwa kwa muda, lakini baadae inakwenda kusababisha kongosho kuzalisha inslin nyingi sana (shooting) bila idadi ili kuhangaika na wingi wa sukari mwilini. Hali hii inaweza kusaababisha kisukari cha muda (Post prandial) effects. Insulin ikiwa nyingi sana kwenye mzunguuko kutasababisha glukose nyingi kwa wakati mmoja ihamishwe kwenye damu kwenda kwenye tissues.
 
Àsante kwa hii elimu.
Sasa shida ni je tufanyeje kwa vyakula kama nyama maana tuliisha zaea kula nyama kwa kuichanganya na vyakula vingne. Je tuwe tuna kula pekee pasipo kuchanganya chakula chochote (yan tusiifanye kama mboga bali iwe chakula kikuu kinacho jitosheleza)?
 
Mie nauliza hii mambo ya kusema usichanganye chakkula hiki au kile kwani utumbo nao una compartments za aina tofauti za vyakula? Meanning vyakula tumbni havichanganyiki?
Tumbo ni hilohilo moja na vyakula vyote vinakwenda hukohuko kwenye tumbo hili. Hicho ndio chanzo cha matatizo yetu. Kila aina ya chakula inahitaji aina tofauti ya mimeng'enyo (enzymes) na mazingira tofauti ili kimeng'enywe kwa ufasaha. Mfano, vyakula vya protein vinahitaji mazingira ya uchachu mwingi (acidic) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri, lakini mahindi (carbohydrates) usagaji wake tumboni hauhitaji acid kali (alkalinity) ili enzymes zake zifanye kazi vizuri. Sasa kama utachanganya nyama, ugali, matunda, maziwa pamoja kwenye chakula chako na maji ya kunywa wakati huohuo lazima utapata shida tuuu iwe unajuwa au hujui.
 
Sasa nakulaje ugali bila nyama mzeya mbona kama watupiga kamba
 
Kule nyama peke yakee kama wanavyofanya wamasai, simba, na mbwa kama unaweza. changanya/Kula ugali na maharagwe, kunde, njegele, na jamii zote za mikunde. Kula matunda peke yake, kunywa maziwa peke yake.
 
Sasa nakulaje ugali bila nyama mzeya mbona kama watupiga kamba
nafahamu kuwa watu tumekuta halimiko hivyo ya ugali na ng'ombe lakini pia tumekuta watu wakilalamika kutopata choo kwa siku nzima, kupata choo kigumu, kuapata bawasili, kanza za utumbo mpana, kujambia sana watu na wengine kulalamika kupata fungus na kuwashwa mwili mara kwa mara. uwamuzi ni wao.
 
Aya bana ila hapo mzee msosi uwe wa aina moja hapana ..tumbo wacha lipokee mixer ya ugali nyama na mtindi
 
Aya bana ila hapo mzee msosi uwe wa aina moja hapana ..tumbo wacha lipokee mixer ya ugali nyama na mtindi
Vipatie nafasi mkuu kama unaweza angalau mpishano wa dakika 45.

Mfano, wako watu wanasema kuwa nguruwe ni haram, hii sio kweli, ukweli ni kwamba ngurumwe ana sumu nyingi mwilini mwake, hafai kuliwa na kila mtu na watu wote. Sababu kubwa ya nguruwe kuwa na sumu ni kwasababu nguruwe anachanganya vyakula, nyama, majani, mahindi, matunda, maganda na kila kitu kwa wakati mmoja. mwili unashindwa kuvisaga vyakula vyote kwa wakati mmoja kwa haraka na kusababisha chakula kuoza tumboni na kufyonza sumu. Huwezi kula maini na utumbo wa nguruwe hivihivi. Watu wote wanaokula nyama nyingi ya nguruwe hawataishi miaka mingi kwa raha.

Hata binadamu kama atachanganya pamoja ugali, nyama, mboga za majani, ndimu, kachumbali, matikiti maji, na maziwa kwenye mlo mmoja mwili wake utafanana na nguruwe. mwili wake unajaa sumu nyingi.
 
Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?
 
Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?
Hawa hawana elimu hiyo ya food combinations, lakini pia shida iko kwa walaji. Ukikuta buffet maana yake "chagua kati ya hivi" haimaanishi "pakua vyote hivi"
 
Hawa hawana elimu hiyo ya food combinations, lakini pia shida iko kwa walaji. Ukikuta buffet maana yake "chagua kati ya hivi" haimaanishi "pakua vyote hivi"
Mbona sasa mie nikigonga menu za hapo ndio napata choo vizuri tena kama nikila like siku tatu mfululizo choo nakipata kama clock work vile saa mbili na dakila 20 eveyday nakata gogo. Ila sasa nikila wali maharage ndio inapita siku tatu hamna choo. Wee jamaaa unatuzingua
 
Kule nyama peke yakee kama wanavyofanya wamasai, simba, na mbwa kama unaweza. changanya/Kula ugali na maharagwe, kunde, njegele, na jamii zote za mikunde. Kula matunda peke yake, kunywa maziwa peke yake.
Kwaiyo hapa ata smooth sio nzuri kiafya pia?
 
Sasa mbona wanaopika kwenye hizi five star hotels wamesea mambo ya nutrition lakini pale serena nikienda kwenye buffet nakuta mazagazaga kama yote...au hawa wao sayansi yao walisomea mars?
Hawa kazi Yao kubwa kwa mteja ni delicious foods, ni juu yako mteja kumwambia mpishi akuletee na kukutayarishia chakula gani na akitayarishe vipi.
 
Hawa kazi Yao kubwa kwa mteja ni delicious foods, ni juu yako mteja kumwambia mpishi akuletee na kukutayarishia chakula gani na akitayarishe vipi.
Ah wee acha zako bwana kwenye hizi five star hotels wana wataalam hadi wakuwapikia high perfomance athletes na tunaona kabisa wanachanganya carb na protein na vegetables kwenye mlo mmoja
 
Nilidhani faida namba moja ni msamaha toka kwa Mungu
 
1)Wanaofunga ,wanapofuturu na daku jumla wanaongoza calories ngapi on average ukilinganisha na milo yao wakiwa hawajafunga?

2) watu Wanaofunga,wakija kumaliza mfungo uzito huongezeka au kupungua?
 
Kaka binadamu anatakiwa kupata haja kubwa sio chini ya mara 3 kwa siku yenye massa 24 maana chakula kinatakiwa kuchukua sio zaidi ya massa 4 TU kutoka kuingia mdomoni hadi kufika kwenye kinyeo, ukiona sio hivyo umekosra kula.

Mchele wetu umekobolewa sana hivyo unapokula ubwabwa magarage lazima ule na mboga nyingi sana. Inavyotakiwa iwe ni sahani iwe na ubwabwa kidogo kuliko maharagwe na mboga, lakini mwengi wanakosea sana, utakuta ubwabwa ni mwingi Kwenye sinia kuliko mboga na mbogamboga. Ukila ubwabwa mwingi kuliko mboga utachelewa kupata haja kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…