Mwigulu Akiendelea kuwa waziri Basi ndie Rais ajae tutake tusitake. Atakuwa na timu Bora na zaidi ya Tillion 2 kibindoni

Mwigulu Akiendelea kuwa waziri Basi ndie Rais ajae tutake tusitake. Atakuwa na timu Bora na zaidi ya Tillion 2 kibindoni

Nitahama nchi kabisa. Simkubali hata kidogo huyu mwizi. Sijui alipewaje hata hiyo wizara nyeti hiyo. Ameingia tu na kuanza kuiba moja kwa moja. Bahati ni mshamba,anazuzuka na pesa moja kwa moja anaanza kujionyesha wazi.

Kwa nchi zilizopiga hatua anaweza kuchezea jera vizuri
Hilo Ni kwa jicho lako. Kwa jicho la Taifa Ni mzalendo, mpigania haki na mchapakazi na anayechukiwa na wasiompenda Raisi. Anajua kuzichanga karata ndio maana Ni waziri maarufu mpaka leo
 
Rais ajaye ni Either Mwinyi au Inocent Bashugwa baada ya Mtaka kuchafuka

Kila kitu kinaenda sawa kwenye vetting

Marais wenye asili ya dictator hawatakuja kuongoza tena hii nchi.

Save hii!!!
Ndio wanaotakiwa na nchi za kikomunist Kama China na Russia na ndio wanaipaga mbinu ccm
 
Wanaomchukulia Mwigulu kirahisi rahisi wanakosea Sana.
Siwezi zungumzia uadilifu wake lkn najua anavyojua kusaka pesa akiwa kwenye mamlaka.

Alipokuwa naibu tu Wizara ya fedha kwa miaka 2 tu aliunda pesa za kutosha. Mwaka 2015 Akaanza kampeni za uraisi kirahisi Sana. Akalipia matangazo ya redio na tv karibu zote kutangaza Nia.

Mabango, mawe, Barabara vijiwe vikajaa majina ya Mwigulu Raisi.

Alipeleza pesa kidogo tu.

Alichokosea kidogo alichelewa kuunda timu. Na wenzake hawakujua mfuko wake. Wangejipendekeza Sana tu.

Wakati akina kigwangala wakipambana na Mo awakopeshe pesa za kampeni za ubunge Jamaa alibaki na mzigo wa kutosha. Akatumia helkopta kuzunguka nchi mzima na msafara binafsi. Kupiga kampeni za Uraisi ili ajisibitishie Uwaziri.

Sasa akiweza kufanya urafiki wa kinafiki na wapinzani wake Kama akina mpina, timu Jpm ili kupunguza madongo Basi ndani ya miaka 2 atakuwa na mzigo wa kutosha.

Sijui Kama Ni mfanya biashara Ila chukueni hii. Hii singida big star imeibuka na usajili wa kutosha. Mapesa ya kutosha. Mfupa wa kuendesha timu uliomuumisha kichwa Mo na Manji jamaa kautafuna Kama stake.

Anajua kujenga mifumo inayofanya na kupendezwa nae.

Nazani hatujui nguvu ya Mwigulu lkn naamini 2025 anaweza akawa na zaidi ya Tillion 2 ambazo zitamfanya kuwa na timu yenye nguvu Sana.

Jamaa Anajua watu wa kuweka kwenye timu. Sio ajabu kelele kwa mama haziwezi sikika Sababu washauri wote wa mama Ni timu yake.

Mwigulu ndio Raisi ajae.
Hakuna Taarifa aweza kuja kuwa Rais wa Taifa la Tz. May be ktk kusadikika. Japo pia kuna Mungu so let keep...
 
Hilo Ni kwa jicho lako. Kwa jicho la Taifa Ni mzalendo, mpigania haki na mchapakazi na anayechukiwa na wasiompenda Raisi. Anajua kuzichanga karata ndio maana Ni waziri maarufu mpaka leo
Haya unaandika ukiwa sawa kichwani..yaani urais ni mambo ya kuchanga karata, mtu hajui hata kupanga maneno ya kusema anaropoka tu..unajua wakati mwingine vzr mtu ujipime kiwango cha akili ulizo nazo kabla ya kuandika lolote watu wasome..
 
Duuh.

Kwahiyo umeleta hii mada ututishie au unahalalisha fedha za umma??

Maana kutuambia kwamba atakua na Trilioni 2 bila kutupa vyanzo vyake vya mapato ni kutuambia kuwa atatumia nafasi aliyonayo kuipata hiyo fedha.

Sidhani kama ni sahihi kuendelea kumuacha katika hiyo nafasi ili achukue hizo pesa.
 
Back
Top Bottom