Mwigulu anasema hakuna Mtanzania atagongewa mlango alipe Deni la Taifa, kwani tozo maana yake nini?

Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akitoa ufafanuzi kuusu deni la taifa amesema kuwa
“Hakuna Mtanzania atakwenda kugongewa mlango atoe mbuzi alipe Deni la Taifa, hakuna atakayeambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa, ni kama Mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakayekwenda kuchukua madaftari ya Mwanafunzi"

kwaiyo watanzania tusiwe na wasiwasi na tuondokane na zile story za vijiweni kwamba nchi itauzwa kutokana na deni kubwa.

Lakini pia amesema "Kuna utofauti kati ya deni la Taifa na deni la serikali, deni la Taifa linahusisha deni la serikali na sekta binafsi, mfano Bakhresa au TBL tunafahamu mitaji na uwekezaji wao ni mikopo, hivyo wakikopa, deni lao linajumuishwa katika deni la Taifa"
 
Mpaka sasa sijajua kwa uhakika pale Udsm huwa wanazalisha wataalamu wa Kitu gani wanaweza kujisifia

Maana kila sekta huibuka na kauli tata na kutuacha na mshangao

Christmas njema!
Labda huzalishwa wanasiasa wengi !! Mradi tu sio kosa !! Ndio maana huwa tunaona maprofesori wengi hukimbilia kwenye siasa na kuacha taaluma walizozisomea !! Hasara kubwa !!
 
Mwigulu toka uteuzi wake kila kukicha anatoa sababu mpya ya kudhihirishia ulimwengu kuwa hakupaswa kuwa waziri. Hili liko wazi kabisa.

Kisichoeleweka mpaka muda huu ni kwanini mamlaka iliyomteua inaogopa/inasita kutengua uteuzi wake.

Ni aidha ana kitu dhidi ya waliomteua kiasi kwamba wanahofu ya kumtengua ama wana maslahi ya moja kwa moja kupitia uwepo wake kama waziri.
Hili la pili linaogopesha zaidi kuona utawala wa juu umedhamiria kufanya maisha ya raia wa chini kuwa magumu kila kukicha.
 
Mwigulu toka uteuzi wake kila kukicha anatoa sababu mpya ya kudhihirishia ulimwengu kuwa hakupaswa kuwa waziri. Hili liko wazi kabisa.

Kisichoeleweka mpaka muda huu ni kwanini mamlaka iliyomteua inaogopa kutengua uteuzi wake. Ni kama vile iwe isiwe ni lazima awe yeye waziri tu.

Imekuwa kama kipindi cha Makonda na Magufuli.
Mwananguu !!
 
Mimi ni layman wa uchumi lakini alichoongea leo Mwigulu Nchemba katika kipindi cha 360 Clouds TV ni Doctorial Rubbish, amesema,

"Hakuna siku Mtanzania atakwenda kugongewa mlango kwamba sasa atoe mbuzi alipe Deni la Taifa. Na hakuna siku Mtanzania ataambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa. Hiyo inakuwa ni kama mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakwenda kuchukua madaftari ya mwanafunzi". Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.

Ninachojua mimi ukilipa KODI unagongewa mlango ukikatwa TOZO unagongewa mlango, ukilipa USHURU unagongewa mlango.
Tozo maana yake Ni tozo
 
Mwigulu haoni hizi tozo au anajizima data.

Imethibitishwa Tsh29,000.00 imetumwa kwa 2557xxxxxxxxx - XXXXXX XXXX Tarehe 13/12/22 saa 11:09 AM Jumla ya Ada Tsh686.00 (M-Pesa Ada Tsh380.00 + TOZO ya Serikali Tsh306.00). Salio lako ni Tshxxxxxxx.
 
Waziri wa fedha Mwiguru nchemba alipokua akitoa ufafanuzi kuusu deni la taifa amesema kuwa
“Hakuna Mtanzania atakwenda kugongewa mlango atoe mbuzi alipe Deni la Taifa, hakuna atakayeambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa, ni kama Mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakayekwenda kuchukua madaftari ya Mwanafunzi"

kwaiyo watanzania tusiwe na wasiwasi na tuondokane na zile story za vijiweni kwamba nchi itauzwa kutokana na deni kubwa.

Lakini pia amesema "Kuna utofauti kati ya deni la Taifa na deni la serikali, deni la Taifa linahusisha deni la serikali na sekta binafsi, mfano Bakhresa au TBL tunafahamu mitaji na uwekezaji wao ni mikopo, hivyo wakikopa, deni lao linajumuishwa katika deni la Taifa"
 
Mimi ni layman wa uchumi lakini alichoongea leo Mwigulu Nchemba katika kipindi cha 360 Clouds TV ni Doctorial Rubbish, amesema,

"Hakuna siku Mtanzania atakwenda kugongewa mlango kwamba sasa atoe mbuzi alipe Deni la Taifa. Na hakuna siku Mtanzania ataambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa. Hiyo inakuwa ni kama mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakwenda kuchukua madaftari ya mwanafunzi". Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango.

Ninachojua mimi ukilipa KODI unagongewa mlango ukikatwa TOZO unagongewa mlango, ukilipa USHURU unagongewa mlango.

Mwigulu haoni hizi tozo au anajizima data.

Imethibitishwa Tsh29,000.00 imetumwa kwa 2557xxxxxxxxx - XXXXXX XXXX Tarehe 13/12/22 saa 11:09 AM Jumla ya Ada Tsh686.00 (M-Pesa Ada Tsh380.00 + TOZO ya Serikali Tsh306.00). Salio lako ni Tshxxxxxxx.

Mwigulu anaongea kana kwamba serikali Ina pesa zake yenyewe, wakati pesa inatoa kwa wananchi na wananchi ndio wanaolipa Deni la nje kilupitia Kodi na tozo.

Serikali haijawahi kulipa deni la nje bali Serikali inatumia pesa zilizochangwa na wananchi kulipa madeni ya nje.
 
Waziri wa fedha Mwiguru nchemba alipokua akitoa ufafanuzi kuusu deni la taifa amesema kuwa
“Hakuna Mtanzania atakwenda kugongewa mlango atoe mbuzi alipe Deni la Taifa, hakuna atakayeambiwa alipe Deni la Taifa atoe mchango mkubwa, ni kama Mzazi ukikopa mshahara wako hakuna atakayekwenda kuchukua madaftari ya Mwanafunzi"

kwaiyo watanzania tusiwe na wasiwasi na tuondokane na zile story za vijiweni kwamba nchi itauzwa kutokana na deni kubwa.

Lakini pia amesema "Kuna utofauti kati ya deni la Taifa na deni la serikali, deni la Taifa linahusisha deni la serikali na sekta binafsi, mfano Bakhresa au TBL tunafahamu mitaji na uwekezaji wao ni mikopo, hivyo wakikopa, deni lao linajumuishwa katika deni la Taifa"

Mbona anamdhalilisha Bakhresa?. Kwamba naye ni mmoja waliokopa Trilioni 20?. Sasa Kama Bakhresa kakopa Trilioni moja, Hilo Deni ni la Bakhresa au Tanzania Kama taifa. Na atakaye lipa ni Bakhresa au sisi wa wananchi.
 
Kama ni Hivyo, atueleze kwa lugha Rahisi hiyo hiyo ni kwa namna gani hizo hela zilizokopwa zitakavyolipwa? Asitumie maneno ya "trat na trab" kwenye maelezo yake maana yatatuchanganya.
Kwanza niliposikia tu kasema hivyo na hakuna aliyemwambia kwamba kodi ndio kugongewa mlango kwenyewe nikajua tu hapa hakuna mahojiano,ni kikao cha wanaCCM tu
 
Mpaka sasa sijajua kwa uhakika pale Udsm huwa wanazalisha wataalamu wa Kitu gani wanaweza kujisifia

Maana kila sekta huibuka na kauli tata na kutuacha na mshangao

Christmas njema!
Kitu pekee ambacho UDSM na vyuo vingine vya Tanzania wanaweza kujivunia ni kuzalisha mafisadi/wala rushwa/wahujumu uchumi/wabadhirifu wa mali za umma.

Kuna I.P.I na Shule ya Uhandisi kwenye mekanika,lakini wana mamia ya magari yamelala pale Auxillary yakiwa mabovu mpaka unashangaa hiki ni chuo au sehemu ya kulaza magari mabovu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom