Mwigulu hatodumu Wizara ya fedha, hana traits za kuimudu kazi yake

Mwigulu hatodumu Wizara ya fedha, hana traits za kuimudu kazi yake

Nimemsikiliza huyu jamaa Bwana Madelu Mwigulu Nchemba akiongea na Timu ya Wizara ya Fedha jamaa anaonekana ni mtupu kabisa kichwani kuhusu mambo ya Uchumi!! Sijamsikia akiweka mkakati wowote namna atakavobuni mbinu mpya za kukusanya Kodi au kuongeza Wigo wa kukusanya kodi...!!!

Sana alikuwa anarejea tu hotuba ya Mhe. Mama Samia kasema, kasema, mama kasema na kujirudiarudia kwingi. Nimecheka sana alipotoa mfano wa kijijini kwao Iramba kuhusu Wafugaji wa ng 'ombe kuwa huwa hawakamui maziwa yote mpaka damu itoke....lazima wamwachie ndama naye kidogo!!!!

Huyo ndio Mchumi namba 1 aliyeaminiwa na Mama Samia Suluhu. What a shame to this man?? Bila shaka mama atakuwa ameingizwa choo cha kiume.
Kuna tofauti kubwa sana ya mtu kufaulu darasani with Honours na kile mtu anakwenda kuki-present site katika utekelezaji.

Tusubiri, muda utasema tu!!!
Mkuu nini ubaya wa mfano wa ng'ombe alioutowa Mh. Waziri? Auulitaka atoe mfano Uingereza ndiyo uelewe?
 
Mwigulu akiachana na mihemuko na vijembe vya kisiasa akatulia, Ni kiongozi mzuri Sana.....
 
Tunaomba mtuwekee hapa publications za madelu kwenye international journals ili angalau tuamini kwamba ni mchumi first class...
 
Ninyi watu humu mna habari madame President yumo humu anatusoma? Hili la madelu na ndugulile atalifanyia kazi mapema baada ya kikao Cha bajeti kuisha! Kipimo pekee Cha madelu ni jinsi atakavyojibu maswali kwenye kikao Cha bajeti! Tumuombe madame President afya njema ili aweze kumtafakari vizuri huyu njemba mgonga punda! Hamalizi mwaka huu pale hazina!
Huyo jamaa mugonga Punda a.k.a Fusso hapashwi kudumu ofisi ile hata kwa sekunde 1...!!!Yaelekea madame hamjui vzr jamaa ! Bila shaka atakapo ona graph ya Uchumi inadorora ndipo atajua ingawa atakuwa amechelewa sana🤩🤩
 
Mwanzo tu amekurupuka sio kila kauli ya raisi ni amri moja kwa moja zingine zinakingana na sheria za administration au utaratibu wa kufanya mambo.

Mwigulu badala ya kukaa kwanza na TRA kuelewa auditing reasons za wafanyabiashara kutakiwa kutunza nyaraka zao kwa miaka kadhaa, anaibuka na kuropoka ovyo.

Nina uhakika somewhere kuna sheria inaelezea ni information gani wafanyabiashara wanatakiwa kutunza na kwa miaka mingapi nchi nyingi ni miaka 5 au sita.

Mara nyingi watu wanaporudi nyuma ni kwa sababu wamebaini uongo leo na sheria inawaruhusu kukagua tena miaka ya nyuma kama ulitumia mbinu hizo hizo kukwepa kodi.

Tatizo hapo kuna maafisa wa TRA wasio na maadili wanaweza tumia nafasi hiyo kunyanyasa wafanyabiashara.

Lakini kutunza risiti sio utaratibu wa Tanzania tu ni kote duniani ipo ivyo, ata baada ya kupewa tax clearance. Isitoshe mfanyabiashara anaeweka hela nyumbani elewa ni dalili za kwanza huyo mtu ni mkwepa kodi and there is something dodgy.
 
Mchawi mpe mtoto akulelee.. Naamini
Ilimpasa Raisi kumtoa Mpango pale na kumpa uVP a ceremonial position, ili aweze kumweka mtu atakayemmudu yeye Raisi.
Mwigulu kama ilivyokuwa kwa Mpango hatofanya kitu nje ya nini boss wake anataka afanye. Ni wizara naamini itaiangaliwa na madam President kwa ukaribu mno.

Mpango atabakia kuzindua mbio za Mwenge na kutumwa tumwa huko na huko ili asimsumbue Mwigulu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mataifa makubwa ikiwemo S.Africa kauli ya Waziri wa Fedha inaweza kuchangia positively or negatively kwenye uchumi. Waziri wa Fedha akizungumza Jambo watu hupima mapokeo kwa kuhojiana na Wafanyabiashara, wachumi na pia kuangalia trend ya soko la hisa la nchi husika.

Nikimwangalia nakumsikiliza Mwigulu, nikiangalia historia yake kwenye hii nchi ninakiri hana uwezo wa kuongoza wizara ya fedha. Ana uwezo mkubwa darasani lakini siyo mbunifu, Ni mtu anayefaa kuajiriwa na kusimamiwa siyo kusimamia.

Kinachokwenda kutokea ni Makamu wa Rais anakwenda kufanya kazi za Waziri wa Fedha. Swali, kwa malengo ya kisiasa ya Mwigulu atakubali kuongoza na Dr. Mpango? Ukweli ni kwamba hatokubali. So lazima ugomvi utatokea vinginevyo Dr. Mpango achague kukaa kimya Jambo ambalo ni gumu kwa sababu Mhe Rais ameshamkabidhi jukumu la kumsimamia na kumwongoza Mwigulu.

Mhe. Rais alipompa jukumu la wizara ya fedha Makamu wa Rais alijua kabisa Waziri na Naibu ni wachanga kwenye Wizara hii.
Mzee Ndugai alisema Waziri wa Fedha anshitajika sana kipindi hiki lakini hapohapo akasema sasa hivi tunaye Mwigulu alafu akacheka sikumwelewa Cheka take lakini muhusika alimwelewa
 
Mataifa makubwa ikiwemo S.Africa kauli ya Waziri wa Fedha inaweza kuchangia positively or negatively kwenye uchumi. Waziri wa Fedha akizungumza Jambo watu hupima mapokeo kwa kuhojiana na Wafanyabiashara, wachumi na pia kuangalia trend ya soko la hisa la nchi husika.

Nikimwangalia nakumsikiliza Mwigulu, nikiangalia historia yake kwenye hii nchi ninakiri hana uwezo wa kuongoza wizara ya fedha. Ana uwezo mkubwa darasani lakini siyo mbunifu, Ni mtu anayefaa kuajiriwa na kusimamiwa siyo kusimamia.

Kinachokwenda kutokea ni Makamu wa Rais anakwenda kufanya kazi za Waziri wa Fedha. Swali, kwa malengo ya kisiasa ya Mwigulu atakubali kuongoza na Dr. Mpango? Ukweli ni kwamba hatokubali. So lazima ugomvi utatokea vinginevyo Dr. Mpango achague kukaa kimya Jambo ambalo ni gumu kwa sababu Mhe Rais ameshamkabidhi jukumu la kumsimamia na kumwongoza Mwigulu.

Mhe. Rais alipompa jukumu la wizara ya fedha Makamu wa Rais alijua kabisa Waziri na Naibu ni wachanga kwenye Wizara hii.
Kazi sana, yaani wewe unamfahamu saaana? Nyinyi watu inaonekana mmeaminishwa tofauti hasa kiutendaji na alivyo.

Labda uongozi wake wakati mwajiriwa Benki kuu alifanya vizuri kimaigizo. Mbona kichwa chake na ufahamu wa mambo ya Fedha na Uchumi yupo vizuri tuu.

Akishindwa atakuwa ameamua kushindwa na atajilaumu mwenyewe.
 
Kwa msiojua Mwigulu ni mzuri wa kupokea maelekezo na kutekeleza......
sio mbunifu.....
mm binafsi namuona akitekeleza maelekezo ya VP.....
si ajabu VP ndio alimpendekeza hiyo post...
mtakumbuka hata wakati VP anaumwa Mwigulu alishika mikoba ya VP bungeni ilhali akiwa waziri wa sheria.....
 
Mh Mwigulu anahitaji kupewa mawazo si kuwa critized mwanzoni anapoanza majukumu.

Mimi nitaonesha mfano wa mawazo hapa. Kuna shutuma ambazo zinapelekewa mwenda zake pengine ni kutaka kupata umaarufu angalau kuzima umaarafu wa Mwili wake huko mitaani na mitandaoni.

Hivi hatuwezi kujiuliza kwa nini ilifikiwa uamuzi wa watu kufungiwa akaunti zao? Kulikuwa hamna sababu za msingi kwa ushuru kukusanywa kwa aina hiyo iliyofanyika? Hakuna kitu chenye mashiko kilichopelekea maamuzi hayo?

Je wafanyabiashara waTanzania wamekua malaika kuliko wengine huko ulimwenguni? Kuwa ni waaminifu kiasi hicho? Trump anatuhuma nyingi mno za ukwepaji wa kodi ingawa anakingiwa kifua kiaina. Leo unataka kuniambia Tanzania wanao wafanyabiashara na Watumishi wa TRA mahiri na waaminifu kuliko USA? Ni kujidanganya tu kuamini hivyo.

Kama tutafika mahali tupuuze mambo kama meli 60 zimetia nanga na hamna rekodi mahali popote au flow mita haifanyikazi kwa miaka 5 basi hili litakuwa Taifa la watu wa ajabu sana.

Unapojua aliye korofisha flow mita bandarini au ambaye kapitisha mizigo bila kulipa kodi stahiki biashara yake ni ile na account yake ni ile hata ikiwa kumepita miaka 5 utaacha usimfuatilie? Pengine biashara yake bado ni hiyo kwa kipindi cha miaka yote anayotuhumiwa? Sheria si inasema kipindi kadhaa cha kuweka records za biashara yako huko nyuma.

Kwa nini mzigo inayoingizwa kutoka nje serikali isichukue chake kwa bei ya soko iwaache Wafanyabiashara kukusanya VAT yao ambayo wameshailipa serikali in advance kutoka kwa wateja wao wakati na wale mwisho? Tuone kama kuna mfanyabiasha atakubali kodi ambayo keshailipia in advance serikalini aikwepe asiikusanye!

Tatizo la watumishi wa TRA la kutengeneza mazingira ya kuhongwa kwa kutumia sheria za kumbana mlipa kodi ilikumtishia linatatuliwa vipi.?

Je serikali inajua kuwa yako baadhi ya makampuni mawakala wa wakadiria kodi ambao wanaungana na TRA upande mmoja na mfanyabiasha upande wa pili kutengeneza mazingira ya kukwepa ulipaji kodi?

Utapanua wigo wa kulipa kodi wakati hujatafuta ufumbuzi wa Watumishi wako wa TRA ulio wa ajiri unao wa mudu na kuwadhibiti ukitaka? Uko utashi wa kweli kutoka serikalini kudhibiti vitendo vya baadhi ya watumishi hawa? Sioni kama hilo linatiliwa maanani.

Serikali lazima ikae na wafanyabiashara iwasikilize lakini iwahimize kukataa vitendo vya rushwa. Hii itafanikiwa kama TRA kutadhibitiwa.

Hivi serikali inashindwa nini kuweka watu ama idara ambazo zitaweza kuhakiki mahesabu ambayo mfanyabiashara anakadiriwa na TRA na mawakala wa kufanya mahesabu ya wafanyabiashara? Iwe ni lazima kabla mfanyabiashara hajalipa kilichokadiriwa nao wajiridhishe kwa kufuata taratibu flani ikiwemo kumjua mfanyabiashara huyo na kuona kama anaridhika na makadirio yao.

Lakini kwa nini viwango vya kodi viwe vikubwa kiasi cha kumshawishi mfanyabiashara kuona ni bora kuziendea hatari za ukwepaji kuliko kwenda kulipa kwa haki,halali na hiari?

Tanesco na umeme huko nyuma ilikuwa ni kimbembe kuhusu kupata malipo ya huduma zao. Luku ilipokuja imepunguza sana hili tatizo ikabakia bypassing na vitu vidogo vidogo. Huu mtindo hauwezi kuhuhishwa kwa baadhi ya kodi na wafanyabiashara hata kama sio zote/ wote?

Kwenye ulimwengu huu wa sayansi na technologia inashindikana kweli kwa serikali kupata kodi yake inayostahili kutoka kwenye bei ya soko? Kitu kama sementi kiwanda kiko. Bei ya soko inajulikana serikali iliyo sereous ina shindwa kupata kodi yake? Mimi na fikiri watu hawajibunishi wafanye nini maana wanajua wakiweka mbinu imara hakuna kupiga na mradi huu utakufa. Hivyo suluhisho ni kuweka njia legelege ili waendelee kunufaika nazo na mradi wa kupiga kodi kwa kwenda mbele uendelee.
 
Back
Top Bottom