Mwigulu: Kodi ya majengo kwa kutumia LUKU sio ya Mpangaji ni ya Mmiliki

Mwigulu: Kodi ya majengo kwa kutumia LUKU sio ya Mpangaji ni ya Mmiliki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Fedha na Mipango amesema mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mita za LUKU haitawahusu wapangaji bali ni wamiliki wa nyumba husika.

Ametoa mfano wa ilivyokuwa kwamba mpangaji anapokuwa amelipa malipo ya mmiliki huwa anawasiliana na mwenye nyumba wake ili arudishiwe hela yake.

Amesema mambo mengine yote yatakuwa ‘programmed’ vizuri ili kuepusha watu kupanga foleni ya kwenda kulipa kodi ya pango.
 
Waziri wa hovyo kabisa kuwahi kutokea
Kwa hili serikali imefanya vyema sana. Inataka kuwe na compliance kubwa sana, pia administration cost itakuwa negligible kwa sababu the tax will be tapped at source.

Itakuwa na ufanisi kama road licence ambayo inatozwa kwenye mafuta. Hakuna senti inayopotea. Compliance is at excess.
 
Je nyumba ikiwa na mita zaidi ya 1?
 
Je nyumba ikiwa na mita zaidi ya 1?

Sijajua utaratibu, hiyo ni changamoto ambayo wanapaswa kuifanyia kazi baada ya kupokea kutoka kwako ewe mwananchi unayeipenda nchi yako. Na hata ukiwa na tentative solution go to share with them. They will appreciate, coz they are also Tanzanians we build the same house.

CC: DONARD MUSIMU
 
Je nyumba ikiwa na mita zaidi ya 1?

Zote zitalipiwa Kodi ya nyumba ili kufidia wale ambao hawana umeme😆😆
Nyumba zote Tanzania zinaenda kuwa na umeme,niamini Mimi,hongera serikali kwa ubunifu huu🙏🙏

Tulipe Kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Sijajua utaratibu, hiyo ni changamoto ambayo wanapaswa kuifanyia kazi baada ya kupokea kutoka kwako ewe mwananchi unayeipenda nchi yako. Na hata ukiwa na tentative solution go to share with them. They will appreciate, coz they are also Tanzanians we build the same house.
Acha wapangaji tuongezewe mzigo wa kodi
 
Ana hakika nyumba zote zina luku 2 yaani ya wapangaji na wenye nyumba?
Waziri wa Fedha na Mipango amesema mfumo wa ulipaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mita za LUKU haitawahusu wapangaji bali ni wamiliki wa nyumba husika

Ametoa mfano wa ilivyokuwa kwamba mpangaji anapokuwa amelipa malipo ya mmiliki huwa anawasiliana na mwenye nyumba wake ili arudishiwe hela yake

Amesema mambo mengine yote yatakuwa ‘programmed’ vizuri ili kuepusha watu kupanga foleni ya kwenda kulipa kodi ya pango
 
Ovyo Sana kuwahi kutokea...suala hili kuliongea rahisi Sana ila utekelezaji wake ndio changamoto...wananchi wengi watalipishwa hii Kodi bila kuwa wahusika.Muda utaongea..
 
Huyu ndiye huwa anaota Urais.
Anachambua as if yeye ndiye huwa anaishi na wapangaji na mwenye nyumba.
 
Mwigulu nilikuwa sikubaliani nawe ktk mengi, ila kwa hili nakuunga mkono, haya malalamiko ni kaupepo tu katapita, Mimi ni muumini wa indirect tax coz maumivu yake huwa hayaumizi kama direct tax,
 
Back
Top Bottom