Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Kwa kweli kama huyu Mwigulu Nchemba angekuwa nje ya maccm basi angekuwa Rais pekee nchi hii,anaongea bila kumung'unya maneno. Wezi na mafisadi wa mali ya umma ni wa kufilisiwa,kushtakiwa na kufungwa bila mjadala.
 
Imetulia hii Mpwa. Umekaa na kufanya yako kwa hekima na busara kubwa, hongera sana. Baadhi ya Watanzania ni wakurukupukaji kupita kiasi sijui kwanini huwa hawapendi kutafakari kwa kina kabla ya kukurupuka na kuandika yale ambayo hayastahili kuandikwa.

Tutaendelea kufanya makosa ya kuwapa mdaraka wasiostahili mpaka lini!? Kwanini hatutaki kujifunza kupitia makosa yetu ya miaka ya nyuma ili kuinusuru nchi yetu ambayo ilitakiwa iwe na maendeleo makubwa sana lakini inayumba miaka nenda miaka rudi kutokana na viongozi wasio na sifa hata moja ya kuliongoza Taifa letu, wezi, wanafiki, majangili, wauza unga, wapokea rushwa, waongo, wahuni n.k. Dah! inauma sana kuwasoma baadhi ya watu humu kwa jinsi wanavyokurupuka kila siku iendayo kwa Mungu.


 
mwigulu akikaza anaweza kuja kupendwa na watanzania kama anavyopenda zitto, na pengine kupata umaarufu kama alioupata zitto
 
CCM Haina agenda ya Rais kuna agwnda ya CCM ambayo ndio ilani ya chama. Atakwepaje?
Mtu anayemmsikia huyu jamaa kwa mara ya kwanza leo lazima ameguswa. Lakini haya maono yote haya huwa anayo tangu anaanza kupata airtime kwny TV.
Ila alichowahi kufanya ndio hakionekani. Nilitegemea aseme jambo moja dogo alilolianzisha na kulisimamia hadi likaonekana
 
Amenivutia kwa kuwa na vipaumbele vitatu tuu ambavyo akivisimamia kwa dhati bila uoga Tanzania itakuwa imefanya mabadiliko makubwa sana
 
Mwigulukwa maraya kwanza ameni touch . Hotuba yake ndio mambo ambayo watanzania tunayahitaji na nimeshawishika kumuunga mkono. Lowassa na Wassira hotuba zao hazifikii ya Mwigulu hata robo

Umeuzi watu
 
Hizi Hotuba tamu masikioni mwetu tumezizoea, hata Kiwete kwenye hotuba yake ya kwanza Bungeni alitoa hotuba kali yenye ubora, hakuna mtu anaweza kubadili hii nchi kupitia CCM, we need changes, UKAWA ndio mpango

Umeongea vyema tatizo ukawa umungu MTU Na umm
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida leo katika tamko lako la kutangaza nia ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeonyesha kuwa uko serious, mwadililifu, mtu usiyependa makuu .....na ki historia wewe umetoka ndani ya familia masikini kwa hali hiyo unawajua walala hoi naamini kwamba ukipata hutasahau ulikotoka tofauti na hao wengine wenye kumwaga mapesa ili kuutafuta urais... hivi mapesa haya wanayomwaga watayarudishaje? kwa kuisema ukweli kati ya Lowassa na Mzee Wassira mimi binafsi nakupa .......... Bravooooo ...... Mwigulu .... Aluta continua
 
Insanity is doing the same thing in the same way over and over again and expecting a different result.

Hivi kuna jipya tunasubiria kutoka ccm? Ukoo wa panya huu hata bakuli ya plastiki wanatafuna! Dah
 

Duh, hv kumbe ni kweli baadh ya Watz wanafikiri kwa kutumia MATAKO...
 
Yani we jamaa ni kama mwanamke malaya kila mwanaume unamtaka. umeshamkana Lowasa tayari.
 
Mwigulu yuko upande wa Lowassa; Pasco knows that. Alichokifanya leo Mwigulu ni utekelezaji tu wa "game plan" ya Lowassa.
 
Nakupata Pasco! Jamaa anajua anachokiongea na anajua kuongea kwenye public! Leo kaongea very authoritative na kutoa picha kwamba if he is selected, he can make a best president of United republic of Tanzania! Ki ukweli sina imani na mgombea yoyote toka CCM to date kwa sababu najua Mwigulu kaanza kuongea kwa style ya kuwa upande wa wananchi pale alipoteuliwa kuwa naibu waziri, kabla ya hapo sura yake halisi tulikuwa tunaijua! Sema watanzania ni wepesi sana wa kusahau!
Kifupi speech yake plus appearance, anaonekana kuwa the best president to be, sema moyo wake hatujui umeficha nn!
Ila namsubiri Magufuli ( endapo atatangaza nia kama fununu zilivyo) tuone naye ataongea nn kwani huyo kupitia what He has already done to this nation. Pia uwezo wake wa kuchukua maamuzibila kujali wanaccm wenzake tunaujua! May be that one can make the best president!
Ngoja tuona game hii inaendaje!
 
Last edited by a moderator:
Hauwezi kumpima mwasiasa kwa kuongea tu! Ninafahamu amekuwa naibu waziri wa fedha kwa muda mfupi lakini amefanya nini mpaka sasa kwenye hiyo wizara?

He talks the talk but he doesn't walk the walk, pesa zimechotwa Stanbic Bank under his watch na shilingi inaporomoka kula kukicha lakini hakuna chochote anachofanya.
 
Mimi pia nimeisikiliza hotuba ya Mwigulu Nchemba leo wakati anatangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Wakati naendelea kuisikiza hotuba yake nilikuwa naona kama namsikiliza mgombea wa Ukawa, kwa kuwa almost yote aliyoyaongea ndiyo hayo ambayo viongozi wa upinzani wamekuwa wakiyapigia kelele sana kwenye majukwaa ya kisiasa na hata bungeni.

Mkuu Pasco umeeleza kuwa Mwigulu wakati anatoa hotuba hiyo ameonyesha genuinity.

Hilo naweza kupingana nawe kidogo, kwa kuwa ni Mwigulu huyo huyo ambaye wakati wa sakata la Escrow alidai bungeni kwa nguvu sana kuwa atahakikisha wale wote waliopewa mgao na Rugemalira, atahakikisha kuwa wanalipa kodi kwa pesa hiyo chafu waliyopata.

Hata hivyo ile ilikuwa danganya toto tu kwa kuwa mafisadi wale hadi leo hawajalipa kodi ile hata shilingi 10 pamoja na tambo zote zile za Mwigulu!

Sasa hapo genuinity ya Mwigulu iko wapi?

Mfano wa pili ni pale Mwigulu alipokuwa kwenye BMK ya maccm watupu, ambapo alitahadharisha kuwa wabunge waliopo mle bungeni baada ya kutoka Ukawa, hawataweza kupata 2/3 inayotakiwa ili katiba hiyo ipite.

Hata hivyo mwisho wa siku tulishuhudia maccm hao wakiipitisha katiba yao pendekezwa, kwa kupigiwa kura hata kwa njia ya 'sms'kwa wabunge ambao hawakuwemo bungeni, jambo lilioonyesha kuwa katiba hiyo pendekezwa ilipitishwa kwa uchakachuaji mkubwa uliofanywa na wabunge hao wa Sisiem watupu kwenye hiyo BMK.

Ni kwa nini Mwigulu hakuonyesha genuinety yake kwa kukemea uharamia huo wa hali ya juu?

Ni dhahiri basi kwa mfumo wa CCM ulivyo hata atokee mtu clean kiasi gani, hatakuwa na uwezo hata chembe wa kutekeleza yale anayokusudia, iwapo watu wanaomzunguka na kumpa ushauri ni hawa wafuatao:

1. King maker RA
2. Yule mzee mvaa Chou en lai, ambaye jana aliushangaza ulimwengu kutokana na yeye kujulikana kuwa ni die hard Socialist, lakini jana alionekana kama ndiye mpiga debe mkuu wa 'Capitalist' mzee wa mamvi!
3. Nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Conclusion yangu ni kuwa hata kama leo atashushwa 'Malaika' toka mbinguni aje ajoin chama hicho cha magamba, hataweza kufanya muujiza wa kubadilisha mfumo wa chama hicho wa kukumbatia rushwa, ufisadi na mafisadi wake.
 

Umekula maharage ya wapi??

Huwa napenda kusoma post zako, lakini naanza ku-doubt uwezo wako kwa kumsifia Mwigulu. Ananini Mwigulu??
Msanii tu huyo.
 
The guy is simply the best, ana majibu na maswali yote..ni kipindi cha vijana sasa..apewe nafasi. Look T at Kenya Vijana wanavyofanya wonders....ushabiki pembeni the guy is Good.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…