Mwigulu, Makamba, Mbarawa kusomewa Albadir Tanga kwa ufisadi ripoti ya CAG

Mwigulu, Makamba, Mbarawa kusomewa Albadir Tanga kwa ufisadi ripoti ya CAG

Mikwara tu....

Albadiri ni kisomo kinachotokana na kitabu mathalani JALIYATUL QADAR....ni mashuhuda wa Vita vya badri....ni dua/maombi kama mengine yoyote tu.....sema hao "wadigo" wanakwenda KUWAROGA kwa kujifanya wanasoma Albadiri.....

Ikiwa ni maombi basi tujue si uchawi....na maombi hujibu Mungu vile atakavyo ila ALBADIRI UCHAWI (si maombi) kwa Mungu.......

Mwigulu yupo
Mbarawa yupo.....

Mungu ni mlinzi wa kila mmoja wetu.....
Maombi hayo hayo huwapata watu waovu wanaofanya dhulma kwa jamii !!
 
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Tanga,Ismail Masoud amesema kama wananchi wanaumizwa na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanyika Serikalini na kuwa watafanya dua ya Albadiri kwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.​

Huyu anakuwa mtanzania wa pili kutangaza kufanya maamuzi magumu dhidi ya waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ikiwa ni siku chache tangu Mtanzania mwingine Mkulima kuwafikisha Mahakamani Dk. Mwigulu Nchemba, Januari Makamba, Prof. Makame Mbarawa kutokana na kashfa za ubadhirifu wa mali za umma.​

Nimetafakari sana juu ya uamuzi wa wananchi wa Tanga kuandaa kisomo maalum kwa ajili ya viongozi na watendaji serikalini walioguswa kwenye ripoti ya CAG. Mbali na watu wa Tanga kuamua kufanya dua maalum kwa kina Mwigulu, Makame Mbarawa, Januari na wakubwa wengine waliotajwa na CAG. Pia yuko mtanzania mwingine ameamua kwenda mahakamani kuwashtaki watu hao hao waliotajwa na CAG.

Maamuzi haya ya wananchi kwa kumbukumbu zangu ndogo sina hakika kama matukio haya yamewahi kutokea hapa nchini tangu nchi yetu ipate Uhuru.

Swali je ni watanzania wangapi wanapaza sauti juu ya watu hao ila hazisikiki kwa sababu ya umasikini wao, kutokuwa na simu janja ya kufika mitandaoni na kukosa bando la kuweza kuwasilisha hisia zake kwenye umma.
 
Maombi hayo hayo huwapata watu waovu wanaofanya dhulma kwa jamii !!
Alaa kumbe wanakwenda kuroga eeee?!!!

Waroge tu....

Mwigulu yupo na ni mwafrika haswa....[emoji1787]

Kuna mwafrika asiyejua "anti-dote" ya uchawi?!!!

Mwigulu yupo.....waambie wafanye haraka huo uchawi wao.....
 
Maombi ni maombi tu sio uchawi ni sawa na maombi ya kuomba mvua inyeshe. ! Na maombi hayawezi kumpata mtu kama anasingiziwa kitu ambacho hajakitenda ! Iko hivyo Mkuu. !
Sawa.....

Kwa kuwa wametangaza vita hadharani basi wajue wameshachelewa.....[emoji1787][emoji1787]
 
Nashauri hiyo albadiri ichinjwe na ng'ombe au mbuzi ka sadaka uone ka mtu atamaliza wiki
Moja ya Imani potufu zinazo chelewesha maendeleo africa 😊 😁😁😁😁
Solution ni KATIBA MPYA itakayo zipa mamlaka taasisi zetu kuwashuhurikia wabadhilifu wote wa Mali za UMMA...........

KATIBA MPYA NDIO ALBADIRI KUU NA MZIZI WA KUTIBU😊😊😊😊😊
 
Alaa kumbe wanakwenda kuroga eeee?!!!

Waroge tu....

Mwigulu yupo na ni mwafrika haswa....[emoji1787]

Kuna mwafrika asiyejua "anti-dote" ya uchawi?!!!

Mwigulu yupo.....waambie wafanye haraka huo uchawi wao.....
Sio uchawi ni maombi tu ! Na kama mtu anasingiziwa basi hatakiwi hata kushtuka maana hawezi kupata shida yeyote !
 
Sio uchawi ni maombi tu ! Na kama mtu anasingiziwa basi hatakiwi hata kushtuka maana hawezi kupata shida yeyote !
Waombe tu....

Si peke yao wanaojua "maombi"...

To every action there's an equal and opposite reaction [emoji1787]
 
Moja ya Imani potufu zinazo chelewesha maendeleo africa 😊 😁😁😁😁
Solution ni KATIBA MPYA itakayo zipa mamlaka taasisi zetu kuwashuhurikia wabadhilifu wote wa Mali za UMMA...........

KATIBA MPYA NDIO ALBADIRI KUU NA MZIZI WA KUTIBU😊😊😊😊😊
Na huo ndio ukweli mchungu 🙏🙏
 
Kwa namna fulani hili pia ni dongo kwa Sa100 kwamba yeye kama mkuu wa nchi kwakuwa ameshindwa kuwachukulia hatua acha wao(wananchi) wamuombe Mungu atende miujiza maana hawana namna ingine wa kuwasaidia hakuna!.
Hii staili ya kuongoza nchi kiubongozozo sasa ni rasmi tunaelekea msoga election 2015. Chadema changamkeni
 
Moja ya Imani potufu zinazo chelewesha maendeleo africa 😊 😁😁😁😁
Solution ni KATIBA MPYA itakayo zipa mamlaka taasisi zetu kuwashuhurikia wabadhilifu wote wa Mali za UMMA...........

KATIBA MPYA NDIO ALBADIRI KUU NA MZIZI WA KUTIBU😊😊😊😊😊
Labda ka na wewe albadiri itakuhusu ndo mana una comment uto... skia hìi katiba wala si mbaya saaana kusema haikatazi wala kuwajibisha majizi ila watelezaji ni majizi yanaishi kijamaa
 
Nadhani hii ndo njia sahihi!hizi njia nyingine hawa mafisadi wanalindana sana!
 
Back
Top Bottom