Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Hivi ushaidi wa ugaidi unapelekwa kwa mwanasiasa? Kwa nini aliyerekodi video hiyo asiipeleke polisi kwanza?

Tusipokuwa makini watatusahaulisha ya Ulimboka, maana Wabunge wa CCM akina Stella Manyanya wanasema ni Chadema walihusuka, sasa mbona kimya? Na hili la KIBANDA nalo vipi? HII inaweza kuwa Anti Ballistic Misile na watanzania kwa kusahau haraka!

Kesi ya "Mume" wa Josephine Slaa hivi bado ipo ?
Ivi ile kesi ambayo mchungaji Mtikila alimuita Kikwete gaidi illishia wapi? Inawezekana magaidi ni hao hao wanowasingizia wenzao ni magaidi, just imagine mwenyekiti wao ni gaidi wao watakuwaje?
 
Mimi kwa upande wangu hili la lwakatale bado sijalielewa nani mkweli na nani muongo. "truth is one and it is only one, truth is indivissible"
 
eti ata mbinguni atatoa ushahidi wewe mwendawazimu mwigulu mbinguni utapasikia kwenye bomba we ni wa shetani,kwa iyo tabia yako mbaya unafikiri mungu atataka kukuona
 
To me, hili halina mashaka tena video ni halali. It was bad kwa chama kupitia kiongozi wa juu kupanga kitu kama hicho
 
Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo.

Watanzania wanaangalia Bunge, wanajua Bunge linavyoendeshwa. Wanajua Spika unavyofanya, wanaona Unavyopendelea. CCM mmeshangilia sana, hongereni. Mlianza na Udini wa CUF na sasa wa CHADEMA, Mkaja Ukatoliki wa Slaa, na Uchaga wa CHADEMA.

Mlijaribu Udini suala la Kuchinja limepata busara ya Mwinyi tumepata nafuu ya siku moja. Sasa la Kuchakachua Katiba kunakoendelea mtaani sasa, na kuruhusu ujinga Bungeni kuipendelea CCM kutukana........... mnaharakisha kupeleka nchi kusikovutia wengi.

Mkuu KARAMAG umemaliza kila kitu. Naongeza kidogo kwenye ulichosema ambacho nakubaliana nacho 100 kwa 100. WATANZANIA wengi ni wasahaulifu kama nguruwepori, kwani kila kibaya kinachoendelea hapa nchini ni matunda ya CCM: (1) udini ulipandwa na CCM, wakaibebesha CUF mzigo huo ili isifanikiwe kisiasa; (2) ukabila ni zao la CCM, zigo hilo wakaitwisha NCCR-MAGEUZI; (3) ufisadi ndiyo mbinu iliyotumiwa na MANGULA, MKAPA na JUMA JOHN MALECELA kupambana na upinzani, jimbo likichukuliwa na upinzani wao walichofanya ni kutafuta mwenye mahela ya kumwaga ili jimbo likombolewe; na (4) sasa ugaidi, wanajua unauzika kwa wakubwa akina OBAMA na CAMERON, wanataka kuitwisha CDM ili ife ____________ WA-TZ tusiwe kama nguruwepori, mbinu za CCM ni chafu siku zote, tusisahau.

Ni aibu leo chama cha MWL JKN kuwa na MWIGULU kama NK MKUU na NAPE kama K wa 'ideology'! KWELI, hawa wanaelewa ni nini? Wanajua kweli kujenga taifa na utaifa?

SASA matokeo yake ni kwamba wao wanatuletea yale tusiyoyataka: UBAGUZI NA UKABURU, UDINI, UKABILA ...

MASIKINI hofu ya kupoteza madaraka inaifanya CCM kuwa 'desperate' na kufanya mambo ya aibu ...
 
Mwigulu yupo sahihi Mbowe,Slaa na Lissu wanatetea na kulea Ugaidi! Zitto alisema Lwakatare atoswe wakajidai kulemba maneno!
 
Miezi 4 nyuma huyu mwendawazimu Mwigulu akiwa star tv pamoja na Zito,mtatiro alisema maneno hayo hayo. Kabla tukio halijatokea. Sina imani kabisa na polisi kutomkamata. Waanzie kwenye clip za kile kipindi.
 
Mkuu KARAMAG umemaliza kila kitu. Naongeza kidogo kwenye ulichosema ambacho nakubaliana nacho 100 kwa 100. WATANZANIA wengi ni wasahaulifu kama nguruwepori, kwani kila kibaya kinachoendelea hapa nchini ni matunda ya CCM: (1) udini ulipandwa na CCM, wakaibebesha CUF mzigo huo ili isifanikiwe kisiasa; (2) ukabila ni zao la CCM, zigo hilo wakaitwisha NCCR-MAGEUZI; (3) ufisadi ndiyo mbinu iliyotumiwa na MANGULA, MKAPA na JUMA JOHN MALECELA kupambana na upinzani, jimbo likichukuliwa na upinzani wao walichofanya ni kutafuta mwenye mahela ya kumwaga ili jimbo likombolewe; na (4) sasa ugaidi, wanajua unauzika kwa wakubwa akina OBAMA na CAMERON, wanataka kuitwisha CDM ili ife ____________ WA-TZ tusiwe kama nguruwepori, mbinu za CCM ni chafu siku zote, tusisahau.

Ni aibu leo chama cha MWL JKN kuwa na MWIGULU kama NK MKUU na NAPE kama K wa 'ideology'! KWELI, hawa wanaelewa ni nini? Wanajua kweli kujenga taifa na utaifa?

SASA matokeo yake ni kwamba wao wanatuletea yale tusiyoyataka: UBAGUZI NA UKABURU, UDINI, UKABILA ...

MASIKINI hofu ya kupoteza madaraka inaifanya CCM kuwa 'desperate' na kufanya mambo ya aibu ...

Acha porojo za ngonjera hapa JF
 
Kama jeshi la polisi lingekuwa huru na haki. Mwigulu sasa hivi angekuwa ndani au angalau angekuwa amehojiwa. Kwa jinsi inavyoonekana, polisi nao ni sehemu ya mchezo huu mchafu!
Ulichosema kina ukweli kwa asilimia 100!!
 
‘Vita'ya ugaidi yapasua Bunge

Jumamosi, Aprili 13, 2013 07:06 Na Maregesi Paul, Dodoma

*Mwigulu Nchemba, Tundu Lissu watoana jasho
*Wote wanadai wana ushahidi, Spika awaonya


lwakatare.jpg
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare

MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayekabiliwa na kesi ya ugaidi mahakamani, Wilfred Lwakatare, jana alilitikisa Bunge baada ya kuhusishwa katika mjadala.

Lwakatare alijadiliwa wakati wabunge walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014. Aliyeanzisha mjadala huo, ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), ambaye alianza kwa kuwatuhumu viongozi wa Chadema, wamekuwa wakipanga kuua watu na wakati huo huo wakitaka wananchi wawape ridhaa ya kuongoza nchi.

Alisema pamoja na viongozi hao kuwa na tabia hiyo, wamekuwa wa kwanza kulalamika juu ya vitendo vyao na kwamba tabia hiyo ni sawa na mchawi ambaye akiroga mtu na kumuua, anakuwa wa kwanza kulia akionyesha uchungu alionao juu ya marehemu.

"Mheshimiwa Spika, kuna jambo ambalo limekuwa likiandikwa na kulalamikiwa na watu, kwamba ugaidi ugaidi. Katika jambo hili nawaomba Watanzania wasikilize kwa makini, kuna jambo lilitokea na jambo hili ni jambo la kigaidi, limeandikwa sana na kwa masikitiko linapotoshwa, yaani watu wanapotosha mpaka mambo yanayohusu maisha ya watu.

"Eti wanasema usalama wa taifa, mara wanasema polisi wanatesa watu, katika hili wala msihangaike na kwenye jambo hili hakuna polisi wala usalama wa taifa. Jambo la mkanda, aliyerekoki huo mkanda yuko tayari kusema kokote, aliyeniletea huo mkanda yuko tayari kusema kokote na mimi niko tayari kwenda kokote hata kama ni mbinguni.

"Chadema walipanga kuteka na kuua na huyu mwandishi walipanga kumuua eti wanadai picha ilitengenezwa, sasa kwa taarifa yenu hata pale alipokuwa anaongea, (akimaanisha Lwakatare), aliandika hata ile karatasi ninayo, ni hii hapa, fingerprint ni ya kwake, mwandiko ni wa kwake na vyote alivyokuwa anafanyia kazi vimepatikana na alisema atatoa ushahidi na mimi niko tayari kutoa ushahidi kokote iwe ni hapa na hata mbinguni nitakwenda," alisema Mwigulu akionyesha karatasi hiyo na kuongeza.

"Eti Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), anasema anayewasiliana na gaidi eti naye aunganishwe na ugaidi, hebu fikirieni, yule aliyekuwa akipanga njama ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, kama ni viongozi, amewasiliana na viongozi gani kama siyo wakubwa zake ambao wamemwagiza kufanya hayo tena?

"Jitihada zinazoonyeshwa ambazo ni za kumtetea mtu hata kabla hajafika mahakamani, inadhihirisha ule ulikuwa ni mpango wa chama.

"Kwa kauli hii, ambayo ameandika kiongozi wa upinzani, viongozi wanaowasiliana nao waunganishwe katika kesi ya ugaidi kuanzia leo wakamatwe na polisi, hapa simuoni kiongozi wa Kambi ya Upinzani, labda wameshamkamata," alisema Mwigulu.

Katika mazungumzo yake, Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, alitaka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa, akamatwe kwa kuwa alihusika kumtetea Lwakatare.

Kwa mujibu wa Mwigulu, aliyekuwa akipanga njama za ugaidi huo ni mwanachama wa Chadema na kwamba fedha zilizotumika katika kufanikisha mpango huo, ni za chama hicho.

"Mnasubiri nini polisi, mtu ameshaomba kuunganishwa mwenyewe katika kesi?"

"Mkishapanga maovu mnawahi kwenda kutetea kama vile mchawi ambaye akishaua, anawahi kwenda kulia na kugalagala msibani. Mimi kwenye hili suala la mauaji, nawaomba Chadema mfanye vitu viwili, kwanza kimbieni haraka zaidi kwenye makanisa ama misikiti mliyokaribu nayo ili mkatubu kuwa mmepanga kuwauwa watu wasio na hatia.

"Baada ya kuomba toba, mrudi kutubu kwa wananchi, yaani mnataka uongozi halafu unawaza kuuwa watu, look at you,
" alisema.

Wakati akiendelea kusema, Mbunge wa Mbulu, Mustafa Akunay (CHADEMA), aliomba utaratibu na kumlalamikia Mwigulu, kwamba anazungumzia masuala ya Lwakatare wakati akijua yako mahakamani.

Alipomaliza kusema hayo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alikubaliana naye na kuwataka wabunge waheshimu kanuni za Bunge. Hata hivyo hoja hiyo Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Pauline Gekul alisimama na kuomba mwongozo kwa kutumia Kanuni ya 68 (7).

Alipokuwa akizungumza, alionyesha kutoridhishwa na maelezo ya Spika kwa kuhoji kama wabunge wanatakiwa kufuata kanuni kwa nini Mwigulu alipokuwa akizungumzia masuala yaliyo mahakamani hakuzuiwa na badala yake aliachwa na kuendelea kusema hadi mwisho.

Hoja hiyo, ilimfanya Spika asimame tena na kusema wabunge wanatakiwa kufuata kanuni kwa kuwa hata Mbowe alipokuwa akiwasilisha maoni ya kambi yake juzi kuhusu bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kuna maneno yasiyofaa aliyasema, lakini akaachwa hadi mwisho.
 
[h=2]UGAIDI WALIVURUGA BUNGE[/h]

  • [*=center]Friday, 12 April 2013
    [*=center]Written by Mjengwa Blog


bunge_77749.jpg

Dodoma. Spika wa Bunge, Anne Makinda jana ni kama aliruhusu mvutano wa wazi baina ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chadema ambao kila upande uliutuhumu upande mwingine kwa kuhusika kwa viendo vya ugaidi.
Licha ya kutozungumzia suala hilo moja kwa moja, lakini msingi wa tuhuma hizo ni kesi iliyofunguliwa mahakamani dhidi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Chadema, Willifred Lwakatare ambaye anakabiliwa na makosa yanayomtuhumu kwa ugaidi.


Katika mazingira hayo ni dhahiri wabunge waliingilia uhuru wa mahakama kwani kesi husika iko mahakamani na Spika Makinda katika moja ya miongozo yake jana alisema: "Itabidi Kamati ya Kanuni ikutane kwa kuwa mambo yanayozungumzwa yako mahakamani, hivyo ni muhimu mahakama ikaheshimiwa."
Kifungu cha 114 (1) cha Sheria ya Kanuni za adhabu (Penal Code), kinatoa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela kwa mtu yeyote ambaye kwa namna yoyote anatoa matamshi yenye mwelekeo wa kushawishi uamuzi wa mahakama kwa suala lolote ambalo liko mahakamani likisubiri uamuzi.
Matamshi hayo ni yale yenye mwelekeo wa kupindisha mwenendo wa kesi husika au yenye mwelekeo wa kutaka uamuzi upendelee upande fulani au matamshi yenye lengo la kudhalilisha au kushusha hadhi ya mamlaka ya mtu ambaye kesi yake iko mbele ya mahakama.
Mjadala kuhusu ugaidi ulianza kuchipua juzi wakati Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alipowasilisha maoni ya kambi yake kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu kwa kusema: "Umeibuka uchochezi mpya wa kisiasa wenye ubia kati ya chama tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa ugaidi."
Mbowe alisema kambi yake inashangazwa na uhodari wa Serikali katika kuchukua hatua kwa suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi kuwa yeye ndiye gaidi.
"Kambi yetu inasikitika sana kuona wale wote waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM na washirika wao hawajachukuliwa hatua yoyote," alisema Mbowe na kuongeza:
"Tunaulaani mkakati huu wenye nia ovu ya kufifisha demokrasia hapa nchini...mpango huu haramu hautafanikiwa ... na hili nalo likiachiwa likakomaa litaliingiza Taifa letu katika hatari nyingine ya machafuko."
Jana suala hilo lilichukua sura ya kisiasa zaidi pale wabunge wawili; Mwigulu Nchemba wa Iramba Magharibi (CCM) na Tundu Lissu wa Mbunge wa Singida Mashariki walipochangia hotuba hiyo na kuzama katika eneo la ugaidi, hali iliyosababisha mvutano mkali bungeni.
Kauli ya Nchemba

Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara) aliishambulia hotuba ya Mbowe akieleza kuwa hakuna haja ya kuhangaika na suala la ugaidi kwa kuwa Chadema ndiyo wanahusika nalo kwa kupanga kumdhuru mwandishi wa habari.


 
huyu mwiguru ni limbukeni wa siasa, kazidi hata wajinga kwa kiwango cha juu sana. mi sioni hata usomi wake kwa hizo pumba anazo zitoa.... very shame on him. halafu, vipi hao wanao shangilia kwa ujinga anao usema hasa CCM!!!!!!!!!!hili bunge letu vipi? mbona siwaelewi, so, anawafurahisha na wanaona ndo star wao wa kulemaza chama TEULE CHA WATANZANIA (CHADEMA)au nao ndo walewale......mwiguru hadi mtoto wangu mdoogo anamshangaa, hop anahitaji concelling amesha chizika huyo. Anakera taifa hadi nikisikia jina lake naona aibu kwa mtu anaejiita msomi tena mchumi kwa ujinga anao fanya. MWIGURU UMESHA KUWA DUDU LA TAIFA HILI
 
hili jamaa uwelewa wake ni mdogo sana, atachukiwa sana na jamii kwa siasa zake za kipuuzi na kwa kwendo huu hatafika mbali kisiasa.

Wazee mkeemeeni kijana huyu maana ameivamia siasa kwa pupa.
Hili ni tatizo la kusomea vyeti vya kugushi. Alipaswa awe anachunga ng'ombe huko saa hizi.
 
Kwa watu wakawaida ni rahisi sana kuamini. Lakini TECHNOLOGY iliyotumika kuandaa video hiyo ni ya kiwango cha chini sana. Au mnataka niwatengenezee video ya jinsi hiyo ya Mkulu akiagiza vijana wa usalama wa Taifa kuua watu? sijui mtasemaje siku nikiwawekea hapa. Mwgulu ni mchumi haijui hata robo ya robo ya technology ya mawasiliano. Aache kubwabwaja kama bata anayeharisha. Mahakama zina watu makini ingawa hata majuha yamo, itaeleweka tu muda si mrfu. Au nitengeneze video ya Mwigulu akifanya hayo hayo yaliyoko kwenye video inayodaiwa ya Lwakatale? sijui mtasemaje tena? Ndiyo maana watu wanaoijua Technolojia ya mawasiliano wala hawaongei, maana hiyo ni kama vilamu tu ya maigizo ya kina Rambo na kina James Bondi Nawaomba watanzania kote nchini wayapuuze na vyama vya siasa wafanye siasa safi na siyo kwa mwenendo huu waliofikia. Sisi tunaoishi nje ya nchi yetu yanatusikitisha sana mambo haya yanapotokea ndani ya nchi yetu, halafu inaonyesha bado kabisa hatuna elimu ya TECHNOLOJIA. Maana tunashabikia vitu ambavyo hata wenzetu wanatushangaa.
 
Kiukweli mwigulu kidume kwa chadema, panda shuka, tukana, kimbia, jinyonge, bisha, lkn UKWEL NDIO YUO. kamtu kamoja kananyima watu elfu kumi usingizi. embu fikiria wangekuwepo watu wawili km mwigulu CHADEMA ingekuwaje, najua utanitukana lkn UKWELI ndio huuooooooooooooooooooooo///////////
 
kumbe unaongea tu, ujui chochotee. fuatilia elimu ya mwigulu. utajiona kibudu?????/ yule ni kichwa
 
Haka kajamaa kakishavuta bangi iliyochanganywa na ute wa bamia basi kanaropooka! Ipo siku katakalishwa kwenye ncha kali
 
Back
Top Bottom