Capt Tamar
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 13,248
- 18,435
Kuna waliopigana na hawakuwa askari kamili, nakumbuka kuna hadi madereva wa malori walishushwa kutoka kwenye malori yao na kupelekwa vitani, hao pia watahesabika kuwa ni askari kwenye mpango huo wa malipo? Wale ambao wengi baada ya vita kuisha nyerere aliwatunuku vi vyeo kama katibu kata na waliokuwa na elimu nzuri kidogo walipewa vyeo kwenye mashirika na makampuni ya serikali, nawajua baadhi ambao wapo hai hadi leo.