Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

1) Kwa Ushupavu wa Rais wetu, Watanzania tumeendelea na shughuli zetu zote, Hatuwazi Jambo moja tu la UCHAGUZI tuseme mazingira ya Corona, TANZANIA uchaguzi na kazi zote zinaendelea vilevile.

2) Tanzania ni nchi HURU, Watanzania tunafanya kazi zote bila uangalizi wa mtu yeyote toka kwa mabeberu, Hatuhitaji KIRANJA kutoka popote awe mwangalizi au MCHOCHEZI aseme ndio kilichofanywa au kilichosemwa kiwe na UHALALI.
KIRANJA wetu ni Rais wetu.

3) Inaudhi Sana, wasio Watanzania waisimange nchi yetu, walioko mbali waisimange nchi yetu, na walioko ndani WATUMIKE kuisimanga nchi yetu, yaani hatuoni kazi zilizofanyika tunaona tu hatuna tume huru?????.

4) NCHI YETU HATUJAWAHI KUFANYA UCHAGUZI BILA TUME HURU YA UCHAGUZI, MIJITU MINGINE ILIKUWEPO NDANI TANGU UJANA WAO HADI SASA, LEO NDIO WAONE HATUNA TUME HURU?? MLISHAISHI MAISHA YENU TANGU ASUBUHI, JIONI YENU MNATAKA KUTUHARIBIA AMANI YA NCHI YETU, VIJANA TUKO MACHO, "HATUTATUMIKA" HATUTARUHUSU TAMAA ZENU ZA MADARAKA KUVUNJA AMANI YA NCHI YETU.

WALIOWATUMA WAPENI TAARIFA kwamba TANZANIA IPO IMARA, na ina KIONGOZI wa Nchi IMARA zaidi ya JANA.
Dah mkuu umeniwahi, wewe ukiuweka kule kwenye mitandao ya mabeberu (Twitter,FB,Instagram) jua tu utafika hapa JF 😀
 
Nauliza tu,, kwani hatuwezi kuchukua waangalizi wa kimataifa nchini Burundi na Uganda hata Rwanda?? Ninlazima watoke ulaya ???
 
[SUB]Nyerere aliona mbali[/SUB]
 

Attachments

  • IMG-20200410-WA0000.jpg
    IMG-20200410-WA0000.jpg
    29.1 KB · Views: 4
Endelea kusifia Mwigulu ili utetee tumbo lako maana elimu mlizosoma nyie mnaojiita wasomi wa nchi hazijawakomboa kifikra kwani mnaamini bila siasa na kujikomba kwa binadamu mwenzio huwezi kuishi kwa kupata tonge...Jitu zima unakaa kutumia mda wako kutype unamsifia mwanamme mwenzako hata aibu huna..Njaa mbaya sana
 
Back
Top Bottom