Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Uchaguzi 2020 Mwigulu Nchemba: Rais wetu ni Magufuli, waambieni waliowatuma enyi wenye tamaa ya Madaraka

Wewe Mwigulu ndio wale wanasiasa ;malaya malaya" aliowasema Nyerere. "Malaya malaya kwa kuwa mna bei, yaani mnanunulika". Bei yako ni cheo.

Yale mawe uliyoyaandika "mwigulu rais 2015" nenda kayafute.
Yaani yuko kama anatokea Kongwa vile.
 
Yani nyie ni vitasa kweli,! Mnadai tume huru leo? Miezi 3 kabla?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
Tume huru kimekuwa ni kilio Cha muda mrefu Cha vyama vyote vya upinzani nchini na hata wapenda Haki wa chache ndani ya ccm, Nini maana ya wananchi kukaa juani siku nzima kupiga kura, alafu mwisho wa siku mwenye maamuzi ya kuamua Nani ashinde ni time ya uchaguzi yenye vibaraka wa chama tawala
 
Yaani Membe hajawahi kusema tume huru wakati anashinda ubunge Mara zote Leo yuko nje ndo atake tume huru anayotaka yeye, ajiandae kunyolewa tu
Waafrica hatuna hulka ya kuongea wakati tunakula,hata mwigulu anajua tume siyo huru Ila kwa kuwa yupo mezani Sasa hawezi ongea
 
Kitila Mkumbo anakusubiri.Wewe shupalia Magufuli tu badala ya kuongelea uliyoyafanya Singida mashariki sijui magharibi.
Hoja hapa ni dola huru kufanya mambo yake kwa uhuru bila kuingiliwa na mabeberu. Kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi.Ndio maana miaka yote chaguzi zimekuwa huru na zinafanyika kwa amani.
 
Mkuu Mwigulu anasema Magufuli ndo rais wetu Sasa huo uchaguzi wa October ni kwa ajiri ya kuchagua rais wa wapi?
Mwigulu ni mwanasiasa wa ccm! Hana tofauti na Masigwa au Mbowe, au Lisu kutokea na kusema Rais wetu ni Lisu kuanzia oktoba,!

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wangu kwako:

Ndugu Mwigulu, wewe kama mwanasiasa na binadamu ambe huijui kesho yako,ni vyema ukaweka akiba ya maneno na zaidi utambue Mzee huyu,kwa umri wake, anaweza asiwe na muda mrefu wa kubaki kwenye siasa kama ulivyo wewe; hivyo, hii tume anayoililia leo hii, inaweza kuja kuwa msaada kwako na wala si kwake yeye ambae leo kaamua kuililia.

Jambo lingine unalopaswa kutambua ni kuwa,kesho na keshokutwa, mwanao au hata mjukuu wako anaweza kuja kuwa mwanasiasa kama ulivyo wewe(akakurithi kwa njia hiyo); hivyo, tume hii anayoililia mzee huyu leo hii inaweza kuja kumnfaisha mwanao huyo kama sio mjukuu wako na pengine ukajikuta unamshukuru kimoyoyo na hata kuanza kujilaumu wewe mwenyewe.

Tuwe tunatazama mbele.
 
Ni haki yako kutoa maoni sawa na uonavyo. Hongera kwa hilo.

Lakini pia ni haki ya wengine kuwa na mtazamo tofauti na kile unachoamini wewe.

Ukisema tuna tume huru wengine watakuuliza uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa huru?

Ukidai vyombo au washirika wa nje wasiiingilie mambo ya nchi yetu wengine wenye mtazamo tofauti na wewe watakuuliza kuwa kuna matukio ya watu kupotea ama kuuawa kutokana na itikadi za kisiasa, je usalama wa mazingira ya leo ama kesho wayajua?

Niseme wazi nakushangaa sana tena sana jinsi ulivyojivika upofu kama vile hujawahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ama kuwa mshirika wa haya mambo.

Pole sana. Huenda walioumizwa wasiweze kuchukua hatua yeyote ile, ila KUMBUKA karma is real, nayo yaja upesi sana.

Kesho ni fumbo, vilevile October ni fumbo pia.


Naipenda Tanzania, naiombea amani Tanzania.

Mola tunusuru na wasaka tonge walio wazuri kutetea maslahi binafsi kuliko maslahi mapana ya nchi.


#Fitina kwangu ni mwiko, nitasema kweli daima. (Ahadi #8 TANU)
 
Mwigulu huitetei nchi, bali unajipendekeza kwa rais kwakuwa anaweza kukupa madaraka, ambayo yatakufanya ww, familia yako na ukoo wenu kuepukana na umasikini. Huna historia ya kuitetea nchi, bali siku zote umekuwa na utamaduni wa kukitetea ccm, maana huko ndio una nafasi ya kuepukana na umasikini. Isitoshe we sio mtu muadilifu, bali ni mtu wa siasa za chuki, ukatili na uhasama. Unajipa jukumu la kumtetea rais kwani kwa yale uliyoyafanya, cheo cha urais tu ndio kinaweza kukupa cover. Lakini kwa maneno marahisi ww sio mzalendo, bali ni muhuni mwenye madaraka ya kujipendekeza.
Haya ni maoni ya Mwigulu kama yeye ameweka kando madaraka yake. Na hapa anaeleza ukweli. Tanzania ni dola huru na inafanya mambo yake bila kuingiliwa na taifa lolote lile.

Ndio maana hata kukabiliana na Corona virus hakuiga nchi yoyote. Na hata inapofanya uchaguzi inafanya kwa misingi ya katiba ya JMT na sheria za za JMT. Ndio maana toka tumepata uhuru chaguzi zote zimekuwa huru. Habari ya kipato chake kama waziri wewe unaleta wivu wa kiswahili.
 
Kama ilivyo haki yako kutaka Magufuli atawale milele, Ndivyo ilivyo haki yetu wengine kutaka dikteta Magufuli aondoke katika Uchaguzi ulio huru na haki; kinachokufanya uogope Tume Huru ni nini wewe Pumbavu
 
Mkuu unadhani hapa wanaokomolewa ni CHADEMA?
Tukiharibu kwenye uchaguzi na kupata Viongozi wabovu maumivu hayatakuwa ya CHADEMA,yatakuwa kwa wananchi wote...

Tujikumbushe kwa uchache tu...
Maamuzi mabovu yaliyofanywa kwenye zao la korosho,wanamtwara na Lindi watwambie,waliokuwa CCM waliuza kwa bei kubwa zaidi ya wale wa CUF,ACT NA CHADEMA?

Watumishi wa umma waliochagua CCM wameongezewa mishahara yao kwa miaka 5 ukilinganisha na wale waliochagua UKAWA?

Mawazo Kama ya kwako,(kudhani kwamba kudai haki ni kazi ya kundi fulani),ni hafifu sana, kwani madhara ya kutokuwepo kwa haki hiyo hata wewe yatakupata
Nani kasema waanakomolewa
 
Kaka umeibuka! Huna hoja zaidi ya kujaa hasira tu. Vijana unaowasema ni vijana gani hao? Wewe mwenyewe mwaka huu hutoboi. Na ukicheza game lako vibaya ni lazima upotezwe tu. Ni suala la muda tu! Jangili Mkubwa wewe!
 
Yatamkuta tu ni habari ya muda! kwani Membe anaepiga Miayo sasa hivi wakati akiwa kwenye panel na mkwere ungemwambia leo atakuwa mlizi angekuelewa?

Jitu Kama Mwigulu Nchemba ATI Daktari(sijajua ni daktari wa nn)linafikri MAGUFULI atakuwa Rais wa MAISHA na si ajabu ndo kundi la kina Kessy, Ngamia na Ayubu wanaopiga debe baadhi ya Vifungu vibatilishwe ili Magufuli AONGEZEWE MUDA wa Urahisi mpaka 2039 watakaporudi Bungeni Nov, 2020!! Yajayo ni kichefuchefu!
 
Jitu Kama Mwigulu Nchemba ATI Daktari(sijajua ni daktari wa nn)linafikri MAGUFULI atakuwa Rais wa MAISHA na si ajabu ndo kundi la kina Kessy, Ngamia na Ayubu wanaopiga debe Magufuli AONGEZEWE MUDA wa Urahisi mpaka 2040 watakaporudi Bungeni Nov, 2020!! Yajayo ni kichefuchefu!
Mnafiki tu huyo anajitengenezea sifa za kurithi uongozi wa kidikteta!
 
Back
Top Bottom