Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Kinachofanya mwanasiasa awe mzuri au mbaya si aina yake ya kuongea. Kuna mwanasiasa aliyekuwa rough talker zaidi ya JPM? "Kama hamuwezi kulipa 200 kapige mbizi", na kauli kama hizo lakini I can tell you yule jamaa alikuwa mwanasiasa kindakindaki...
Tatizo ni MATAGA na SUKUMA GANG...
alafu eti wanaungana na Chadema kumpinga Mama..

Moto utawawakia.
 
Fresh tu,waongeze zaidi TOZO
Ifike mahali kwa mwezi wawe
Wanakusanya BLN 200

ova
 
Hongera sana waziri Mwigulu kwa kutoka na kuzitetea tozo zenu kwa hoja mujarabu.

Kama umenotice kuna change of attitude ya wananchi (hata kwa kutumia sample ya wanaJF) baada ya wewe kuzitolea maelezo hizo tozo (nini kimekusanywa, kilipokusanywa kimefanya nini, na falsafa iliyosukuma ujio wa hizo tozo ni nini).

Kilichomiss katika maelezo yako ni evidence. Mfano vijiji gani vilikuwa havina vituo vya afya na sasa kuna vituo vya afya vinajengwa baada ya hizo pesa kupelekwa.

Hii nchi ishaumizwa sana na wanasiasa na itahitaji watu creative katika hoja na katika vitendo ili kuweza kutuweka wote on the same page kimtazamo kuhusu maendeleo ya nchi yetu na kutondolea mashaka mashaka kama mnayoyasema kweli ndiyo yanayofanyika.
Hoja Hii Ni Ya Msingi.

Mwigulu Nchemba njoo utujibu.
 
Kinachofanya mwanasiasa awe mzuri au mbaya si aina yake ya kuongea. Kuna mwanasiasa aliyekuwa rough talker zaidi ya JPM? "Kama hamuwezi kulipa 200 kapige mbizi", na kauli kama hizo lakini I can tell you yule jamaa alikuwa mwanasiasa kindakindaki.

What makes a good politician ni ushawishi tu. Leo Mwigulu umeona walau amebadilika si kwa sababu ya style yake ya kuongea. Sema kaongea kwa ushawishi wa hoja. Kazitetea tozo zake kwa hoja zinazogusa nini watanzania wanataka kukiona katika nchi yao. Ukweli ni kwamba watu hawapingi tozo kwa sababu eti wanakamuliwa (mwananchi wa kawaida katika maisha ya kawaida anaspend pesa nyingi kwenye mambo ya kipuuzi hujapata kuona), seuze kumshawishi atoe 1000 yake kwenye kitu kitakacholeta impact katika barabara na huduma za afya? Kitu kinachofanya watu wawe na wasiwasi kuhusu hizi tozo ni kwamba huko nyuma hakukuwahi kuonekana any value for money kwenye kodi za serikali. Barabara zinazojengwa kwenye halmashauri zetu ni of very poor quality. Ukienda hospitalini hakuna madawa wala vifaa vya kisasa. Nitoe kodi kwa ajili ya kuneemesha wanasiasa takataka dizaini hizi?

You could see mabadiliko ya mitazamo ya wananchi kuhusu kodi pale Magufuli pamoja na ukaksi wake alivyoingia na kusema anataka huduma ya afya wanayoifuata watanzania kule India ipatikane hata Tanzania. Operations za figo na moyo zinafanyika sasa Tanzania. Hayo ndiyo watanzania wanataka kuona kodi zao zinafanya. Wanataka waone shule za serikali kuna vifaa vya kisasa vya maabara na zana za kufundishia viendanavyo na elimu bora. Na kadhalika.

Sasa kuhusu wafanyabiashara visa-vis wananchi, wafanyabiashara pia ni wananchi. Unaposema mzigo wa kodi unamwelemea mwananchi kwani mfanyabiashara hawi sehemu ya mzigo huo? Kama wewe ni mfanyabiashara wa hardware haimaanishi kwamba hununui groceries zinginezo ikiwemo chakula, nguo, umeme, na mambo kama hayo.

Ni sawa na mfanyakazi. Wafanyakazi wanalipa kodi kupitia PAYE na wakati huo huo wanalipa kodi zinginezo kuhusu bidhaa wanazonunua. Sekta binafsi wanajukumu lingine pia la kwamba wakistawi na kuweza kutengeneza ajira nyingi nje ya ajira za serikali hiyo ni service nyingine ya muhimu kwa nchi zaidi ya kodi.

Nchi hii tujienge wote

You are all over the place listen kuna namna nyingi sana za mwanasiasa kukubalika na kuna interpersonal skills nyingi mwanasiasa anazihitaji kuonyesha leadership qualities. Either choices of words ni muhimu in persuasion or building trust.

Magufuli was not persuasive but he managed to build trust among its people; that requires actions and consistency. Yeye aliweka wazi kila mtu atakula kwa jasho na maarifa yake; jukumu lake ni kuweka mazingira wezeshi yatakayotoa fursa.

Alikadhalika uonevu wa wananchi kwake ilikuwa mwiko yaani kila mtu ajione Tanzania ni mali yake, kila mtu apate haki zake, kujaribu kuwapunguzia gharama za maisha watu wa chini, mawaziri wake wote walikuwa wanamuogopa akiongea leo kesho wapo site; leo wanaopiga kazi kwa hari ile ile wamebaki ‘Juma Aweso’ na ‘Ummy Mwalimu’ kidogo hakina Bashe wote sijui wamepotelea wapi. Hakuna mtu tena mwenye shida ya kumfurahisha boss.

Magufuli alipokuwa anaongea alikuwa amung’unyi maneno (japo maneno mengine not desirable it must be said) but he was decisive, na kile alichoongea impact zake wananchi ziliwagusa.

Na ndio sifa ya kwanza ya kuwa Kiongozi nchi za wenzetu, yaani wewe if you can’t win the trust of the majority ya wapiga kura kwenye liberal democracy za West Europe, North America, some Asian countries kama India in some states, Japan, South Korea, Singapore, Australia, and so forth; ushindi uchaguzi miaka minane.

Magufuli ndio kiongizi wa kwanza Tanzania kuwajengea wananchi trust, kuwajengea wao wenyewe confidence na pili kutaka wamuamini katika kazi yake pamoja na mipasho aliyokuwa akiwapa wazi wazi wakimtibua; lakini aina maana he was perfect in every way.

Kabla ya kurudi kwenye tozo na post inayofuata; ila tafadhali usimfananishe Mwigulu, wala mama kwa Magufuli awatoshi kwake ata robo in terms of leadership qualities.

Wewe unaweza shawishika na Mwigulu kweli akikwambia twende vitani kukomboa kijiji tu yeye kama kamanda, binafsi siendi.

Ummy Mwalimu tangia aende TAMISEMI ameanza kuonyesha leadership qualities ambazo sikutegemea anazo akifika sehemu watendaji wajinga wajinga wanaanza kuogopa (but I still believe Jaffo was better than him, TAMISEMI).
 
Kinachofanya mwanasiasa awe mzuri au mbaya si aina yake ya kuongea. Kuna mwanasiasa aliyekuwa rough talker zaidi ya JPM? "Kama hamuwezi kulipa 200 kapige mbizi", na kauli kama hizo lakini I can tell you yule jamaa alikuwa mwanasiasa kindakindaki.

What makes a good politician ni ushawishi tu. Leo Mwigulu umeona walau amebadilika si kwa sababu ya style yake ya kuongea. Sema kaongea kwa ushawishi wa hoja. Kazitetea tozo zake kwa hoja zinazogusa nini watanzania wanataka kukiona katika nchi yao. Ukweli ni kwamba watu hawapingi tozo kwa sababu eti wanakamuliwa (mwananchi wa kawaida katika maisha ya kawaida anaspend pesa nyingi kwenye mambo ya kipuuzi hujapata kuona), seuze kumshawishi atoe 1000 yake kwenye kitu kitakacholeta impact katika barabara na huduma za afya? Kitu kinachofanya watu wawe na wasiwasi kuhusu hizi tozo ni kwamba huko nyuma hakukuwahi kuonekana any value for money kwenye kodi za serikali. Barabara zinazojengwa kwenye halmashauri zetu ni of very poor quality. Ukienda hospitalini hakuna madawa wala vifaa vya kisasa. Nitoe kodi kwa ajili ya kuneemesha wanasiasa takataka dizaini hizi?

You could see mabadiliko ya mitazamo ya wananchi kuhusu kodi pale Magufuli pamoja na ukaksi wake alivyoingia na kusema anataka huduma ya afya wanayoifuata watanzania kule India ipatikane hata Tanzania. Operations za figo na moyo zinafanyika sasa Tanzania. Hayo ndiyo watanzania wanataka kuona kodi zao zinafanya. Wanataka waone shule za serikali kuna vifaa vya kisasa vya maabara na zana za kufundishia viendanavyo na elimu bora. Na kadhalika.

Sasa kuhusu wafanyabiashara visa-vis wananchi, wafanyabiashara pia ni wananchi. Unaposema mzigo wa kodi unamwelemea mwananchi kwani mfanyabiashara hawi sehemu ya mzigo huo? Kama wewe ni mfanyabiashara wa hardware haimaanishi kwamba hununui groceries zinginezo ikiwemo chakula, nguo, umeme, na mambo kama hayo.

Ni sawa na mfanyakazi. Wafanyakazi wanalipa kodi kupitia PAYE na wakati huo huo wanalipa kodi zinginezo kuhusu bidhaa wanazonunua. Sekta binafsi wanajukumu lingine pia la kwamba wakistawi na kuweza kutengeneza ajira nyingi nje ya ajira za serikali hiyo ni service nyingine ya muhimu kwa nchi zaidi ya kodi.

Nchi hii tujienge wote
You know what I am not even going to bother na defence yako ya tozo.

Huyo mwigulu wako anatambua GNI per capita ya mtanzania ndio kwanza ipo above $1500 ndio iliyotuingiza uchumi wa kati.

Hapo kuna vitozo tozo disposable income ni less halafu huyu mtu umuwekee matozo kwenye huduma na bidhaa unadhani hela yake itaenda mbali kweli kwenye matumizi zaidi ya kununua unga wa sembe, kulipa kodi na kubaingiza kutafuta hela ya mboga mwezi mzima.

Hizi tozo kwa wananchi ifike hatua serikali iseme inatosha it’s too much.
 
Tatizo ni MATAGA na SUKUMA GANG...
alafu eti wanaungana na Chadema
You are all over the place listen kuna namna nyingi sana za mwanasiasa kukubalika na kuna interpersonal skills nyingi mwanasiasa anazihitaji kuonyesha leadership qualities. Either choices of words ni muhimu either in persuasion or building trust.

Magufuli was not persuasive but he managed to build trust among its people; that requires actions and consistency. Yeye aliweka wazi kila mtu atakula kwa jasho na maarifa yake; jukumu lake ni kuweka mazingira wezeshi yatakayotoa fursa.

Alikadhalika uonevu wa wananchi kwake ilikuwa mwiko yaani kila mtu ajione Tanzania ni mali yake, kila mtu apate haki zake, kujaribu kuwapunguzia gharama za maisha watu wa chini, mawaziri wake wote walikuwa wanamuogopa akiongea leo kesho wapo site; leo wanaopiga kazi kwa hari ile ile wamebaki ‘Juma Aweso’ na ‘Ummy Mwalimu’ kidogo hakina Bashe wote sijui wamepotelea wapi. Hakuna mtu tena mwenye shida ya kumfurahisha boss.

Magufuli alipokuwa anaongea alikuwa amung’unyi maneno (japo maneno mengine not desirable it must be said) but he was decisive, na kile alichoongea impact zake wananchi ziliwagusa.

Na ndio sifa ya kwanza ya kuwa Kiongozi nchi za wenzetu, yaani we wewe if you can’t win the trust of the majority ya wapiga kura nchi zilifokia liberal democracy za West Europe, North America, some Asian countries kama India, Japan, South Korea, Singapore; ushindi uchaguzi miaka minane.

Magufuli ndio kiongizi wa kwanza Tanzania kuwajengea wananchi trust, kuwajengea wao wenyewe confidence na pili kutaka wamuamini katika kazi yake pamoja na mipasho aliyokuwa akiwapa wazi wazi wakimtibua; lakini aina maana he was perfect in every way.

Kabla ya kurudi kwenye tozo na post inayofuata; ila tafadhali usimfananishe Mwigulu na wala mama kwa Magufuli awatoshi kwake ata robo in terms of leadership qualities.

Wewe unaweza shawishika na Mwigulu kweli akikwambia twende vitani kukomboa kijiji tu yeye kama kamanda, binafsi siendi.

Ummy Mwalimu tangia aende TAMISEMI ameanza kuonyesha leadership qualities ambazo sikutegemea anazo akifika sehemu watendaji wajinga wajinga wanaanza kuogopa (but I still believe Jaffo was better than him, TAMISEMI).
 
You are all over the place listen kuna namna nyingi sana za mwanasiasa kukubalika na kuna interpersonal skills nyingi mwanasiasa anazihitaji kuonyesha leadership qualities. Either choices of words ni muhimu either in persuasion or building trust.

Magufuli was not persuasive but he managed to build trust among its people; that requires actions and consistency. Yeye aliweka wazi kila mtu atakula kwa jasho na maarifa yake; jukumu lake ni kuweka mazingira wezeshi yatakayotoa fursa.

Alikadhalika uonevu wa wananchi kwake ilikuwa mwiko yaani kila mtu ajione Tanzania ni mali yake, kila mtu apate haki zake, kujaribu kuwapunguzia gharama za maisha watu wa chini, mawaziri wake wote walikuwa wanamuogopa akiongea leo kesho wapo site; leo wanaopiga kazi kwa hari ile ile wamebaki ‘Juma Aweso’ na ‘Ummy Mwalimu’ kidogo hakina Bashe wote sijui wamepotelea wapi. Hakuna mtu tena mwenye shida ya kumfurahisha boss.

Magufuli alipokuwa anaongea alikuwa amung’unyi maneno (japo maneno mengine not desirable it must be said) but he was decisive, na kile alichoongea impact zake wananchi ziliwagusa.

Na ndio sifa ya kwanza ya kuwa Kiongozi nchi za wenzetu, yaani we wewe if you can’t win the trust of the majority ya wapiga kura nchi zilifokia liberal democracy za West Europe, North America, some Asian countries kama India, Japan, South Korea, Singapore; ushindi uchaguzi miaka minane.

Magufuli ndio kiongizi wa kwanza Tanzania kuwajengea wananchi trust, kuwajengea wao wenyewe confidence na pili kutaka wamuamini katika kazi yake pamoja na mipasho aliyokuwa akiwapa wazi wazi wakimtibua; lakini aina maana he was perfect in every way.

Kabla ya kurudi kwenye tozo na post inayofuata; ila tafadhali usimfananishe Mwigulu na wala mama kwa Magufuli awatoshi kwake ata robo in terms of leadership qualities.

Wewe unaweza shawishika na Mwigulu kweli akikwambia twende vitani kukomboa kijiji tu yeye kama kamanda, binafsi siendi.

Ummy Mwalimu tangia aende TAMISEMI ameanza kuonyesha leadership qualities ambazo sikutegemea anazo akifika sehemu watendaji wajinga wajinga wanaanza kuogopa (but I still believe Jaffo was better than him, TAMISEMI).
Mi wala sina hata lengo la kumuweka Mwigulu kwa levels za Magufuli. For me Magufuli was another class.

Ninachosema ni kwamba mwanasiasa yoyote atakayetaka kufanya mambo yake ya kisiasa yafanikiwe ni lazima aige baadhi ya tips kutoka kwa wanasiasa waliofanikiwa, hata kama hawawezi kufanana.

Magufuli aliwin trust kwa njia yake na kwa style yake. Utawala wa Samia si lazima ufuate model ya Magufuli ( na ishaonekana wazi kwamba Samia is no Magufuli when it comes to political energy and charisma).

Lakini litakapokuja suala la kufanya maamuzi, kufanya mambo yatokee, hapo hakuna cha Samia wala Magufuli. Hapo suala ni kuamini unachokifanya na kusimamia maamuzi. Kuyumba yumba katika maamuzi si sifa ya uongozi na huwezi kufika popote usipokuwa na dira na kukaa katika mwelekeo.

Ndipo linapokuja suala la akina Mwigulu na Tozo zao. Walipokuja na tozo lazima kulikuwepo na deliberations kwa nini zije tozo. Wewe unalichukulia tozo kama kumuumiza wananchi wa kawaida (unaweza kuwa sawa kwa mtazamo wako). Lakini kwa mtazamo wa uongozi kama wanaamini katika hizo tozo, na nini zinaenda kufanya, na kweli zikafanya na wakatuonesha kuwa ni kweli tozo do make things happen, utashangaa kuona watu watakavyochange attitude ikiwemo wewe mwenyewe.

Kwani Magufuli alipobinya wafanyakazi miaka tano bila ongezeko la mshahara kuna mfanyakazi alipenda? Lakini the man believed in what he was doing kiasi alikaza shingo kutosikiliza kuhusu mambo ya ongezeko la mishahara. Guess what? Juzi nilikuwa shule fulani kadhaa kwenye ishu zangu wafanyakazi wa hizo shule mida ya chai wanamwongelea Magufuli jinsi alivyokuwa kiongozi kweli kweli na jinsi alivyopenda shule zake na kizifuatilia kila mara kutaka zifanye vizuri kwenye mitihani. They like the man pamoja na kwamba kawabinya kwenye maslahi yao.

Mimi bado naamini kwamba tozo za miamala za kuwafanya hao unaowaita wananchi wa chini kushiriki katika kuijenga nchi yao. Kama mtu ni maskini basi hawezi kuwa na hata kitu cha kutuma au kupokea kupitia mpesa. Lakini kama anacho au ameweza kukipata usijenge mazingira ya kumfanya huyo mtu hana cha kufanya kwa nchi yake.

Hata maandiko yanatwambia mwenye nacho atazidi kuongezewa, ila yule anayejifanya hana kitu hata kile kidogo alicho nacho kitampotea. Wape watu fursa ya kushiriki katika kuijenga nchi yao.
 
Adui kubwa kabisa linalo tusumbua waTANZANIA leo hii ni UNAFIKI.... UNAF7IKI... UNAFIKI .....

Lakini tukumbuke... Mama ni Mama...na ana kifua, atapoanza wajibu hawa wapumbavu ......moto utawaka.

Alituambia tumkosoe...ila kistaarabu... MATAGA yanavuka mipaka.
SUBIRI
Duu wameongezeka [emoji24][emoji24]
 
Kwani Mbona tuliambiwaga kwenye Madini kuna Neema?

Kwanini wasitumie fedha za kwenye madini?
 
Mi wala sina hata lengo la kumuweka Mwigulu kwa levels za Magufuli. For me Magufuli was another class.

Ninachosema ni kwamba mwanasiasa yoyote atakayetaka kufanya mambo yake ya kisiasa yafanikiwe ni lazima aige baadhi ya tips kutoka kwa wanasiasa waliofanikiwa, hata kama hawawezi kufanana.

Magufuli aliwin trust kwa njia yake na kwa style yake. Utawala wa Samia si lazima ufuate model ya Magufuli ( na ishaonekana wazi kwamba Samia is no Magufuli when it comes to political energy and charisma).

Lakini litakapokuja suala la kufanya maamuzi, kufanya mambo yatokee, hapo hakuna cha Samia wala Magufuli. Hapo suala ni kuamini unachokifanya na kusimamia maamuzi. Kuyumba yumba katika maamuzi si sifa ya uongozi na huwezi kufika popote usipokuwa na dira na kukaa katika mwelekeo.

Ndipo linapokuja suala la akina Mwigulu na Tozo zao. Walipokuja na tozo lazima kulikuwepo na deliberations kwa nini zije tozo. Wewe unalichukulia tozo kama kumuumiza wananchi wa kawaida (unaweza kuwa sawa kwa mtazamo wako). Lakini kwa mtazamo wa uongozi kama wanaamini katika hizo tozo, na nini zinaenda kufanya, na kweli zikafanya na wakatuonesha kuwa ni kweli tozo do make things happen, utashangaa kuona watu watakavyochange attitude ikiwemo wewe mwenyewe.

Kwani Magufuli alipobinya wafanyakazi miaka tano bila ongezeko la mshahara kuna mfanyakazi alipenda? Lakini the man believed in what he was doing kiasi alikaza shingo kutosikiliza kuhusu mambo ya ongezeko la mishahara. Guess what? Juzi nilikuwa shule fulani kadhaa kwenye ishu zangu wafanyakazi wa hizo shule mida ya chai wanamwongelea Magufuli jinsi alivyokuwa kiongozi kweli kweli na jinsi alivyopenda shule zake na kizifuatilia kila mara kutaka zifanye vizuri kwenye mitihani. They like the man pamoja na kwamba kawabinya kwenye maslahi yao.

Mimi bado naamini kwamba tozo za miamala za kuwafanya hao unaowaita wananchi wa chini kushiriki katika kuijenga nchi yao. Kama mtu ni maskini basi hawezi kuwa na hata kitu cha kutuma au kupokea kupitia mpesa. Lakini kama anacho au ameweza kukipata usijenge mazingira ya kumfanya huyo mtu hana cha kufanya kwa nchi yake.

Hata maandiko yanatwambia mwenye nacho atazidi kuongezewa, ila yule anayejifanya hana kitu hata kile kidogo alicho nacho kitampotea. Wape watu fursa ya kushiriki katika kuijenga nchi yao.
Nakubaliana hapo kwenye leadership style sio lazima zifanane na there is no single approach of winning trust.

Isitoshe Magufuli zilipendwa ata iweje na Samia is entitled to steer the ship on her terms.

However pamoja na kuwa na mbinu mbali mbali za kujijengea imani kwa wananchi; kwenye kufanya harakati hizo lazima utambue people needs come first and depending on various factors ‘Maslow hierarchy of needs’ summed it better.

But because people’s choices vary based on their circumstances ndio maana nchi za wenzetu kodi wamejikita sana kwa watu wenye kipato cha juu na kwenye biashara. Maana sio kila mtu yupo tayari kuchangia shule hao maskini si ndio hao wengine walikuwa wanaona watoto zao bora wabaki nyumbani kuliko kulipia karo, sasa iweje leo uwalazimishe.

Na mama Samia as yet ajaonyesha yupo kwa ajili ya kuwasaidia watanzania maskini kuboresha maisha yao binafsi, wala kuwaaminisha ni raia wenye kumiliki nchi yao.

Ndio maana ni jukumu la serikali kuwekeza kwenye merit goods za jamii kupitia kodi sasa unapoanzisha tozo kila siku unamuumiza mwananchi hasa mwenye kipato kidogo.

Kwenye hiyo receipt ya TANESCO tu mwananchi anachangia mapato ya EWURA, anachangia REA, kwenye mafuta nako kuna michango mingine, bandarini michango, simu michango, daladala michango; yaani kila sehemu ni michango michango michango on top of VAT ambayo ni kodi inayotakiwa kwenda kuwekeza hizo sehemu. Huko kwa wakulima ndio balaa.

Michango inapozidi huo sasa sio uzalendo ni unyonyaji inafikia hatua watu wanaishi kwa hasira yaani hela yao inaishia kwenye michango tu na kuongeza umaskini kwao; wakati ukusanyaji wa kodi ni hafifu kwanini serikali isijikite kuboresha makusanyo.

Wewe unaona sawa kwa mishahara ya vigogo na watunga sera; lakini kwa mwananchi wakawaida hii michango ni mzigo ambao una compromise quality ya maisha yake, isitoshe elementary economics tu inakwambia rise in price reduces demand hiyo impact tayari ishaonekana kwenye hizo tozo the volumes of trade has dropped na hiyo itapelekea loss of VAT and income/corporate taxes za serikali too.

Haya makelele hiyo ni message tosha ya kwamba hii nchi yetu tulio wengi ni maskini and we are sensitive to price increase in our expenditure na sehemu kubwa ya hii hela inaenda kwenye michango on top taxes people pay.

Michango inatosha sasa ata ipewe jina zuri vipi.
 
Wakuu,

Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi ya Serikali pamoja na Tozo za miamala ya simu pamoja na mafuta. Kuwa nami kukujuza yanayojiri

==========

Mwigulu Nchemba-Waziri wa Fedha na Mipango
=▷
Itakuwa aibu mtanzania yoyote alie hai, kuna mradi umekwama kwasababu tu viongozi waanzilishi labda hawapo duniani au hawapo kwenye madaraka, itakuwa aibu ya kila mtanzania alie hai leo.

=▷ Watanzania wameendelea kufanya shughuli za miamala, namba zinaendelea kucheza mulemule kama zilivyokuwa kabla. Kwa mfano kabla hatujaanza kulikuwa na miamala milioni kumi/ kumi na moja na sasa inacheza humo humo kwenye milioni 10/ tisa kama ilivyokuwa mwanzo.

=▷ Katika wiki nne ambazo tumefanya hii shughuli wakati tukisubiri marekebisho haya tunayopanga kuyafanya, kwasababu hii ilikuwa sheria ya bunge iliendelea kutekelezwa

=▷ Lakini katika kipindi hicho ambapo shughuli hii ilianza hapo tarehe 15 mwezi wa saba mpaka hivi tunavyoongea leo ukioanisha na mapendekezo tuliyokuwa tumeyapangilia, tayari tumeshakusanya 48,489,225,670(Bilioni 48.4)

=▷
Katika hizo, tayari tumeshapeleka zaidi ya bilioni 22 kwenye vituo vya afya kwa maeneo ambayo hayana vituo vya afya kabisa ambapo ukipiga hesabu kwa haraka haraka ni zaidi ya vituo 90 vya afya

=▷ Tumeshapeleka nyingine zaidi ya bilioni 15 iende kwenye eneo hilohilo ambayo itafanya zaidi ya vituo 150 sasa kwenye maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na kituo

=▷ Zaidi ya bilioni saba zingine kwaajili ya madarasa kwa ajili ya kujiandaa kupokea watoto wa form one, waziri mwenye sekta atakuja kusema jinsi alivyopangilia.

=▷ Kipindi cha mwezi mmoja Serikali imekusanya Sh 24 bilioni, kutokana na tozo za mafuta ambazo ni mahususi kwa ajili ya kujenga barabara.

=▷ Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko Serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu

=▷ Tuliokuwepo hapa ni dhamana tu, la msingi hata yote tunayofanya ni yetu na ni njia ya kupangalia namna ya kuyafanya, ndio maana ndio maana kiongozi wetu mkuu alisikia sauti hizo na akaelekeza kwamba haya mambo yafanyike.

=▷ Imechukua muda, ni utaratibu tu za kiutekelezaji wa maelekezo na sababu nitazielezea mbele, huwa tunahusisha na makundi mengine ambayo yako nje yetu sisi.

=▷ Mheshimiwa Rais akishakuwa na malengo mazuri namna hii na kule vijijini kwenye maeneo yetu, yakishakuwa mazuri hivi tusigombane kuhusu malengo wala khusu utaratibu. Tushauriane tu namna ya kufanya vizuri kwa ufanisi mzuri zaidi.

=▷ Tunapata ufanisi zaidi tukifanya hivyo, watanzania wanaoishi vijijini na wanaoishi mjini wote wajione wako Tanzania.

=▷ Hii ndio itakayotuondlea pengo la walionacho na wasianacho, zamani ilikuwa inatokea wanafanya mtihani, kijiji kizima hatokei hata mtoto mmoja aliefaulu kwahiyo kuboresha hii miundombine, afya watanzania tukibebe kwa yowe kabisa kwa sababu ni chetu. Niwaombe watanzania kuendela kuwa watulivu na wavumilivu.

Pia, soma=▷ Dkt. Ndugulile: Rais Samia ameagiza tulitazame upya suala la tozo, wananchi kuweni na subira tutakuja na mapitio
Kwani huyu waziri anaona uchungu gani hata ikikatwa tozo ya 50%? Yeye kila kitu bure mawasiliano, usafiri, malazi, maji, umeme, na pesa za kujikimu nje ya mshahara, anapewa na kodi zetu kila mwezi kila siku. Sisi tumemuwa jiwe la kusagia kila kitu tozo tozo!!!!!!!!!!!!!!!! Naona wamesahau ya kupumua, kwenda chooni na kulala na wake/ waume zetu. Mungu anawaona hata Mulla Omar karudi Kabul
 
Athari yake itaonekana bear future na ndipo hao loan providers watakaanza kutupangia cha kufanya kama masharti!

Kila mmoja hajali akijua kesho ataondoka
Huu uzalendo huu
Nasikitika sana kwa vizazi na vizazi
Hapo masharti na mikataba itasainiwa kwa lazima na jinsi wanavyotaka
 
Mnavyomganda Mama ni kama vile amekaa miaka Nane... Kumbe maskini ya Mungu she is hardly 6 months in the office..

Hivi vichwani mwenu mna minyoo!??
Huenda inachangiwa na hasira na uchungu zidi ya kumfunga Mboe eeeh Samahani kumbe Mandela!

Huyu jamaa ni kati ya watu waungwana sana , ni mtu aliyejaa subira, amekuwa akizuia munkari ya watu kutaka ku-react kwenye mambo kadha wa kadha!

Lakini Mwenyezi Mungu ni Mkuu sana na matendo yake yanatisha kama nini!

Afunguliwe Mandela , Mandela ni mwana Africa [emoji440][emoji442][emoji443][emoji447][emoji448][emoji449] afunguliwe Mandela!

Mandela eeeeh eeeeh Mandela!
 
Back
Top Bottom