Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Kinachofanya mwanasiasa awe mzuri au mbaya si aina yake ya kuongea. Kuna mwanasiasa aliyekuwa rough talker zaidi ya JPM? "Kama hamuwezi kulipa 200 kapige mbizi", na kauli kama hizo lakini I can tell you yule jamaa alikuwa mwanasiasa kindakindaki...
Tatizo ni MATAGA na SUKUMA GANG...
alafu eti wanaungana na Chadema kumpinga Mama..

Moto utawawakia.
 
Fresh tu,waongeze zaidi TOZO
Ifike mahali kwa mwezi wawe
Wanakusanya BLN 200

ova
 
Hoja Hii Ni Ya Msingi.

Mwigulu Nchemba njoo utujibu.
 

You are all over the place listen kuna namna nyingi sana za mwanasiasa kukubalika na kuna interpersonal skills nyingi mwanasiasa anazihitaji kuonyesha leadership qualities. Either choices of words ni muhimu in persuasion or building trust.

Magufuli was not persuasive but he managed to build trust among its people; that requires actions and consistency. Yeye aliweka wazi kila mtu atakula kwa jasho na maarifa yake; jukumu lake ni kuweka mazingira wezeshi yatakayotoa fursa.

Alikadhalika uonevu wa wananchi kwake ilikuwa mwiko yaani kila mtu ajione Tanzania ni mali yake, kila mtu apate haki zake, kujaribu kuwapunguzia gharama za maisha watu wa chini, mawaziri wake wote walikuwa wanamuogopa akiongea leo kesho wapo site; leo wanaopiga kazi kwa hari ile ile wamebaki ‘Juma Aweso’ na ‘Ummy Mwalimu’ kidogo hakina Bashe wote sijui wamepotelea wapi. Hakuna mtu tena mwenye shida ya kumfurahisha boss.

Magufuli alipokuwa anaongea alikuwa amung’unyi maneno (japo maneno mengine not desirable it must be said) but he was decisive, na kile alichoongea impact zake wananchi ziliwagusa.

Na ndio sifa ya kwanza ya kuwa Kiongozi nchi za wenzetu, yaani wewe if you can’t win the trust of the majority ya wapiga kura kwenye liberal democracy za West Europe, North America, some Asian countries kama India in some states, Japan, South Korea, Singapore, Australia, and so forth; ushindi uchaguzi miaka minane.

Magufuli ndio kiongizi wa kwanza Tanzania kuwajengea wananchi trust, kuwajengea wao wenyewe confidence na pili kutaka wamuamini katika kazi yake pamoja na mipasho aliyokuwa akiwapa wazi wazi wakimtibua; lakini aina maana he was perfect in every way.

Kabla ya kurudi kwenye tozo na post inayofuata; ila tafadhali usimfananishe Mwigulu, wala mama kwa Magufuli awatoshi kwake ata robo in terms of leadership qualities.

Wewe unaweza shawishika na Mwigulu kweli akikwambia twende vitani kukomboa kijiji tu yeye kama kamanda, binafsi siendi.

Ummy Mwalimu tangia aende TAMISEMI ameanza kuonyesha leadership qualities ambazo sikutegemea anazo akifika sehemu watendaji wajinga wajinga wanaanza kuogopa (but I still believe Jaffo was better than him, TAMISEMI).
 
You know what I am not even going to bother na defence yako ya tozo.

Huyo mwigulu wako anatambua GNI per capita ya mtanzania ndio kwanza ipo above $1500 ndio iliyotuingiza uchumi wa kati.

Hapo kuna vitozo tozo disposable income ni less halafu huyu mtu umuwekee matozo kwenye huduma na bidhaa unadhani hela yake itaenda mbali kweli kwenye matumizi zaidi ya kununua unga wa sembe, kulipa kodi na kubaingiza kutafuta hela ya mboga mwezi mzima.

Hizi tozo kwa wananchi ifike hatua serikali iseme inatosha it’s too much.
 
 
Mi wala sina hata lengo la kumuweka Mwigulu kwa levels za Magufuli. For me Magufuli was another class.

Ninachosema ni kwamba mwanasiasa yoyote atakayetaka kufanya mambo yake ya kisiasa yafanikiwe ni lazima aige baadhi ya tips kutoka kwa wanasiasa waliofanikiwa, hata kama hawawezi kufanana.

Magufuli aliwin trust kwa njia yake na kwa style yake. Utawala wa Samia si lazima ufuate model ya Magufuli ( na ishaonekana wazi kwamba Samia is no Magufuli when it comes to political energy and charisma).

Lakini litakapokuja suala la kufanya maamuzi, kufanya mambo yatokee, hapo hakuna cha Samia wala Magufuli. Hapo suala ni kuamini unachokifanya na kusimamia maamuzi. Kuyumba yumba katika maamuzi si sifa ya uongozi na huwezi kufika popote usipokuwa na dira na kukaa katika mwelekeo.

Ndipo linapokuja suala la akina Mwigulu na Tozo zao. Walipokuja na tozo lazima kulikuwepo na deliberations kwa nini zije tozo. Wewe unalichukulia tozo kama kumuumiza wananchi wa kawaida (unaweza kuwa sawa kwa mtazamo wako). Lakini kwa mtazamo wa uongozi kama wanaamini katika hizo tozo, na nini zinaenda kufanya, na kweli zikafanya na wakatuonesha kuwa ni kweli tozo do make things happen, utashangaa kuona watu watakavyochange attitude ikiwemo wewe mwenyewe.

Kwani Magufuli alipobinya wafanyakazi miaka tano bila ongezeko la mshahara kuna mfanyakazi alipenda? Lakini the man believed in what he was doing kiasi alikaza shingo kutosikiliza kuhusu mambo ya ongezeko la mishahara. Guess what? Juzi nilikuwa shule fulani kadhaa kwenye ishu zangu wafanyakazi wa hizo shule mida ya chai wanamwongelea Magufuli jinsi alivyokuwa kiongozi kweli kweli na jinsi alivyopenda shule zake na kizifuatilia kila mara kutaka zifanye vizuri kwenye mitihani. They like the man pamoja na kwamba kawabinya kwenye maslahi yao.

Mimi bado naamini kwamba tozo za miamala za kuwafanya hao unaowaita wananchi wa chini kushiriki katika kuijenga nchi yao. Kama mtu ni maskini basi hawezi kuwa na hata kitu cha kutuma au kupokea kupitia mpesa. Lakini kama anacho au ameweza kukipata usijenge mazingira ya kumfanya huyo mtu hana cha kufanya kwa nchi yake.

Hata maandiko yanatwambia mwenye nacho atazidi kuongezewa, ila yule anayejifanya hana kitu hata kile kidogo alicho nacho kitampotea. Wape watu fursa ya kushiriki katika kuijenga nchi yao.
 
Duu wameongezeka [emoji24][emoji24]
Your browser is not able to display this video.
 
Kwani Mbona tuliambiwaga kwenye Madini kuna Neema?

Kwanini wasitumie fedha za kwenye madini?
 
Nakubaliana hapo kwenye leadership style sio lazima zifanane na there is no single approach of winning trust.

Isitoshe Magufuli zilipendwa ata iweje na Samia is entitled to steer the ship on her terms.

However pamoja na kuwa na mbinu mbali mbali za kujijengea imani kwa wananchi; kwenye kufanya harakati hizo lazima utambue people needs come first and depending on various factors ‘Maslow hierarchy of needs’ summed it better.

But because people’s choices vary based on their circumstances ndio maana nchi za wenzetu kodi wamejikita sana kwa watu wenye kipato cha juu na kwenye biashara. Maana sio kila mtu yupo tayari kuchangia shule hao maskini si ndio hao wengine walikuwa wanaona watoto zao bora wabaki nyumbani kuliko kulipia karo, sasa iweje leo uwalazimishe.

Na mama Samia as yet ajaonyesha yupo kwa ajili ya kuwasaidia watanzania maskini kuboresha maisha yao binafsi, wala kuwaaminisha ni raia wenye kumiliki nchi yao.

Ndio maana ni jukumu la serikali kuwekeza kwenye merit goods za jamii kupitia kodi sasa unapoanzisha tozo kila siku unamuumiza mwananchi hasa mwenye kipato kidogo.

Kwenye hiyo receipt ya TANESCO tu mwananchi anachangia mapato ya EWURA, anachangia REA, kwenye mafuta nako kuna michango mingine, bandarini michango, simu michango, daladala michango; yaani kila sehemu ni michango michango michango on top of VAT ambayo ni kodi inayotakiwa kwenda kuwekeza hizo sehemu. Huko kwa wakulima ndio balaa.

Michango inapozidi huo sasa sio uzalendo ni unyonyaji inafikia hatua watu wanaishi kwa hasira yaani hela yao inaishia kwenye michango tu na kuongeza umaskini kwao; wakati ukusanyaji wa kodi ni hafifu kwanini serikali isijikite kuboresha makusanyo.

Wewe unaona sawa kwa mishahara ya vigogo na watunga sera; lakini kwa mwananchi wakawaida hii michango ni mzigo ambao una compromise quality ya maisha yake, isitoshe elementary economics tu inakwambia rise in price reduces demand hiyo impact tayari ishaonekana kwenye hizo tozo the volumes of trade has dropped na hiyo itapelekea loss of VAT and income/corporate taxes za serikali too.

Haya makelele hiyo ni message tosha ya kwamba hii nchi yetu tulio wengi ni maskini and we are sensitive to price increase in our expenditure na sehemu kubwa ya hii hela inaenda kwenye michango on top taxes people pay.

Michango inatosha sasa ata ipewe jina zuri vipi.
 
Kwani huyu waziri anaona uchungu gani hata ikikatwa tozo ya 50%? Yeye kila kitu bure mawasiliano, usafiri, malazi, maji, umeme, na pesa za kujikimu nje ya mshahara, anapewa na kodi zetu kila mwezi kila siku. Sisi tumemuwa jiwe la kusagia kila kitu tozo tozo!!!!!!!!!!!!!!!! Naona wamesahau ya kupumua, kwenda chooni na kulala na wake/ waume zetu. Mungu anawaona hata Mulla Omar karudi Kabul
 
Deni la Taifa limefika ngapi na wanarejesha ngapi au hawana hata habari ya kulipa?
Au ndio kukopa harusi na kulipa Matanga


Athari yake itaonekana on the near future na ndipo hao loan providers watakaanza kutupangia cha kufanya kama masharti!
 
Athari yake itaonekana bear future na ndipo hao loan providers watakaanza kutupangia cha kufanya kama masharti!

Kila mmoja hajali akijua kesho ataondoka
Huu uzalendo huu
Nasikitika sana kwa vizazi na vizazi
Hapo masharti na mikataba itasainiwa kwa lazima na jinsi wanavyotaka
 
Mnavyomganda Mama ni kama vile amekaa miaka Nane... Kumbe maskini ya Mungu she is hardly 6 months in the office..

Hivi vichwani mwenu mna minyoo!??
Huenda inachangiwa na hasira na uchungu zidi ya kumfunga Mboe eeeh Samahani kumbe Mandela!

Huyu jamaa ni kati ya watu waungwana sana , ni mtu aliyejaa subira, amekuwa akizuia munkari ya watu kutaka ku-react kwenye mambo kadha wa kadha!

Lakini Mwenyezi Mungu ni Mkuu sana na matendo yake yanatisha kama nini!

Afunguliwe Mandela , Mandela ni mwana Africa [emoji440][emoji442][emoji443][emoji447][emoji448][emoji449] afunguliwe Mandela!


Mandela eeeeh eeeeh Mandela!
 
Wakiwa wanatoa takwimu basi wataje na mahali huko vituo vimejengwa ili watanzania tuhakikishe hicho kinachosemwa
Kweli kabisa ili tukahakiki value for money na existence ya mradi physically kuepuka ubabaishaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…