Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
NUKUU ZA MHE DKT MWIGULU LAMECK NCHEMBA AKITOA MREJESHO KUHUSU TOZO ZA MIAMALA YA SIMU.
"Tunapaswa kutambua kuwa nchi ni yako mwananchi, fedha ni zako lakini pia tuliyoyapanga kuyafanya ni yetu pia. Hivi ndivyo inavyokuwa katika nchi inayojitawala. Niwashukuru wote waliolielewa kwa kiasi hicho"
"Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu"
"Sisi Wizara ya Fedha na Mipango tunaamini kwamba, tunapopeleka bilioni 48 kwenye uchumi maana yake tunaongeza kasi ya kutumiana fedha na kuifanya fedha iende kwenye mzunguko na kasi ya kubadilisha fedha kwenye mikono itaongezeka pia"
"Tulikiri katika nchi yetu kuwa kuna miradi mikubwa ya kimkakati na tulikubaliana wote kuwa ni lazima iendelee, miradi hii ni ndoto yetu ambayo tunataka itimie"
"Tukaangalia hili suala la tozo za miamala ya simu, tukasema hakuna namna ya kwamba serikali na watoa huduma tukae kwa pamoja tuone namna gani tutampunguzia gharama ya jumla kwa mwananchi. Tupo katika hatua ya mwisho katika hili"
"Ombi langu moja kwa Watanzania wanaonitazama kwamba jambo hili ni letu sote sio la serikali, nchi hii ni yako wewe hapo ulipo na pesa ni yako na haya mambo tuliyokuwa tunapangilia tuyafanye ni yako, hivyo haya yote ni yetu"
"Tangu tozo za miamala ya simu kuanza tayari bilioni 48 zimepatikana huku bilioni 37 zikielekezwa kwenye ujenzi wa vituo vya afya kwa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na vituo hivyo na bilioni 7 zikienda kwenye ujenzi wa madarasa"
"Tunapaswa kutambua kuwa nchi ni yako mwananchi, fedha ni zako lakini pia tuliyoyapanga kuyafanya ni yetu pia. Hivi ndivyo inavyokuwa katika nchi inayojitawala. Niwashukuru wote waliolielewa kwa kiasi hicho"
"Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu"
"Bado yapo maeneo nchini ili uweze kufika kwenye kituo cha afya inakulazimu uende ama kwenye kata nyingine au tarafa nyingine, kwa umuhimu wa jambo hili tukasema sio la kuacha bila kufanyia kazi"
"Hapa katikati kuliibuka maneno mengi sana na Ilielezwa kwamba shughuli za miala ilipungua, niseme kwamba Watanzania waliendelea kutumiana na shughuli za kufanya miamala hazikuathirika na takwimu ziko pale pale, ni kati ya milioni 9 hadi milioni 11"
"Kuanzia mwaka kesho tutaanza kupokea kidato cha tano ambao wametokana na sera ya elimu bila malipo, tunafahamu mahitaji yatakuwa ni makubwa. Tunaona kabisa mambo haya tunapaswa kuyafanyia kazi na si kuyaahirisha"