Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne


NUKUU ZA MHE DKT MWIGULU LAMECK NCHEMBA AKITOA MREJESHO KUHUSU TOZO ZA MIAMALA YA SIMU.

“Tangu makato ya tozo yaanze kwa hizi Wiki 4 hadi leo tumekusanya zaidi ya Bilioni 48, zaidi ya Bilioni 22 tulishapeleka kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), leo tumepeleka zaidi ya Bilioni 15 kwenye eneo hilohilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150“

"Tunapaswa kutambua kuwa nchi ni yako mwananchi, fedha ni zako lakini pia tuliyoyapanga kuyafanya ni yetu pia. Hivi ndivyo inavyokuwa katika nchi inayojitawala. Niwashukuru wote waliolielewa kwa kiasi hicho"

"Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu"

"Sisi Wizara ya Fedha na Mipango tunaamini kwamba, tunapopeleka bilioni 48 kwenye uchumi maana yake tunaongeza kasi ya kutumiana fedha na kuifanya fedha iende kwenye mzunguko na kasi ya kubadilisha fedha kwenye mikono itaongezeka pia"

"Tulikiri katika nchi yetu kuwa kuna miradi mikubwa ya kimkakati na tulikubaliana wote kuwa ni lazima iendelee, miradi hii ni ndoto yetu ambayo tunataka itimie"

"Tukaangalia hili suala la tozo za miamala ya simu, tukasema hakuna namna ya kwamba serikali na watoa huduma tukae kwa pamoja tuone namna gani tutampunguzia gharama ya jumla kwa mwananchi. Tupo katika hatua ya mwisho katika hili"


"Ombi langu moja kwa Watanzania wanaonitazama kwamba jambo hili ni letu sote sio la serikali, nchi hii ni yako wewe hapo ulipo na pesa ni yako na haya mambo tuliyokuwa tunapangilia tuyafanye ni yako, hivyo haya yote ni yetu"

"Tangu tozo za miamala ya simu kuanza tayari bilioni 48 zimepatikana huku bilioni 37 zikielekezwa kwenye ujenzi wa vituo vya afya kwa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na vituo hivyo na bilioni 7 zikienda kwenye ujenzi wa madarasa"

"Tunapaswa kutambua kuwa nchi ni yako mwananchi, fedha ni zako lakini pia tuliyoyapanga kuyafanya ni yetu pia. Hivi ndivyo inavyokuwa katika nchi inayojitawala. Niwashukuru wote waliolielewa kwa kiasi hicho"

"Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu"

"Bado yapo maeneo nchini ili uweze kufika kwenye kituo cha afya inakulazimu uende ama kwenye kata nyingine au tarafa nyingine, kwa umuhimu wa jambo hili tukasema sio la kuacha bila kufanyia kazi"

"Hapa katikati kuliibuka maneno mengi sana na Ilielezwa kwamba shughuli za miala ilipungua, niseme kwamba Watanzania waliendelea kutumiana na shughuli za kufanya miamala hazikuathirika na takwimu ziko pale pale, ni kati ya milioni 9 hadi milioni 11"

"Kuanzia mwaka kesho tutaanza kupokea kidato cha tano ambao wametokana na sera ya elimu bila malipo, tunafahamu mahitaji yatakuwa ni makubwa. Tunaona kabisa mambo haya tunapaswa kuyafanyia kazi na si kuyaahirisha"







 
Huu uporaji utawatokea puani. "It is a matter of time".
 

Wewe mwananchi kuwa mzalendo kwa miradi yetu ya kimkakati !​

MRADI WA RELI MWANZA - ISAKA 3.0617 trillion shillings​

Two Chinese firms to build $1.32 billion Tanzanian rail line​



Palamagamba Kabudi, Tanzania's Foreign Minister, addresses a news conference at the launch of Twiga Minerals Heralds Partnership between Tanzania Government and Barrick Gold Corp in Dar es Salaam, Tanzania October 20, 2019.
REUTERS/EMMANUEL HERMAN/FILE PHOTO
(Reuters) - Two Chinese companies have won the contract to build a 3.0617 trillion shillings ($1.32 billion) modern rail line in Tanzania, the East African nation's foreign minister said, extending more than a decade of Chinese involvement in the country.
China Civil Engineering Construction Corporation and China Railway Construction Limited will build the 341 km link to connect the Lake Victoria port city of Mwanza in the north to the town of Isaka, on the way to the Indian Ocean port of Dar es Salaam.
The Tanzanian government will pay for the line, Foreign Minister Palamagamba Kabudi said late on Wednesday, ahead of the signing of the agreement in the presence of his Chinese counterpart, Wang Yi, who is on a visit.
 
Hapo sijui atashusha basi mpya ngapi.......maana kapu halina mwenyewe, wazeee wa sandarusi mpooooooo! kuna kapesa ka mboga kamekwiva huku........
 
Ewe Mwananchi unga mkono miradi mikubwa ya kimkakati, US$1Bilioni kwa bandari yetu

US$1B Mradi wa maboresho ya Bandari

Tanzania Ports Authority (TPA) has secured in excess of US$1B in funding to support its Dar es Salaam Maritime Gateway project. The plan aims to expand and improve the port’s position as one of the leading cargo handling gateways in East Africa. In addition to deepening, strengthening, modernising and revamping operations at berths 1-7, it will involve the development of three new wharves Dar es Salaam Maritime Gateway Project: Fact Sheet
 
sh48,000,000,000÷ watu 60,000,000= sh800 tu

waongeze kasi ya makusanyo
 
Wananchi muendelee kupata taarifa za mikakati ya serikali yenu ili mpate kujifunga mkanda kwa kuunga juhudi zake za kuwaletea maendeleo

6 Jun 2021

Benki ya Dunia yaidhinisha mkopo wa trilioni 2.01 kwa Serikali ya Tanzania


Benki ya dunia imeidhinisha mikopo mitatu ya mashart nafuu yenye jumla ya dola za kimarekani milioni 875 sawa na shilingi trilion 2.0125 za kitanzania kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania kwa aijili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini

Source : Daily News Digital

 
Hivi wakuu ni taratibu gani nipitie na Mimi nije kuwa waziri. Maana hizi sekta zinaela sana aise..
 
Mkuu mimi sasa hivi silalamiki tena, bali situmii miamala ya simu, labda iwe lazima sana. Natumia njia ya bank zaidi, ama kutuma mtu kwa bodaboda, au kondakta wa bus.
 
"Tulikiri katika nchi yetu kuwa kuna miradi mikubwa ya kimkakati na tulikubaliana wote kuwa ni lazima iendelee, miradi hii ni ndoto yetu ambayo tunataka itimie"
Tuna samaki, tuna madini, tuna misitu, tuna gas yaani sisi ni Wapuuzi wa mwisho. Full stop
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…