Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Amesema anaangalia Kutoza tozo Kwa wenye mifugo wengi.
 
Ni jambo jema la kumshukuru Muumba wetu kwa kutujaaria uhai pasina kulipa kodi ama tozo......Yaani hapa Mungu amewaweza sana watoza ushuru,tozo na kodi isingekuwa rimoti ipo kwake tozo ya kupumua wangetuwekea
 
Mwigulu Nchemba, wafafanulie watanzania tofauti ya tozo na kodi. ( Makamu wa Rais aliyekuwa Waziri wa fedha asaidie kufa fauna).

Kuna uweze kano mkubwa wizara ya fedha ikachangia mpasuko mkubwa Kati ya serikali na wananchi hasa kuelekea 2025.
Jaribu uone!! Vyombo vya dola vipo macho kuliko wakati wowote ule!!
 
Sipangishi basi. Nyumba yangu sio nyumba ya biashara, nilitaka kusaidiana na wasio na makazi hapa mjini. Kodi wange deal na wenye apartment na wenye nyumba kwa kazi za kibiashara
Wakianzisha tu hiyo kodi, wenue nyumba wapandishe bei ya pango mara moja. Asiyetaka, aondoke.

Akubali akatae! Huo mzigo wa kodi wataubeba wapangaji.
 
Hizi nyumba za mtaani kama kusaidiana. Ukifanya kama biashara unawaumiza wakatwa tozo mwenzako.
Wasomi wetu wengi wana elimu ya kukariri tu darasani! Wengi wao hawana elimu ya maisha.

Wenye nyumba kamwe hawatakubali huo ujinga wa kugawana pasu kwa pasu jasho lao na hawa mafisadi wanaowaza muda wote kununua Ma V8 ya milioni 500, kwa ajili ya kutembelea!

Kitakacho tokea ni kuongeza tu kodi ili mwisho wa siku, huo mzigo wa tozo urudi kwa wapangaji.
 
Wengi wametoka kwenye umaskini wanajua hustle ya kitaa. Sema wana roho mbaya
 
Kwenye kodi za nyumba za biashara(zenye frem za maduka),ingebakia vile vile,mpangaji akilipa TRA,analipa kabisa na asilimia ya pango.Mpangaji apewe risiti mbali ya KODI YA ZUIO,ampe mwenye nyumba,isichanganywe na risiti ya kodi ya biashara,aliyolipa mpangaji.
 
Mwigulu hiyo ofisi ni kubwa kwake unaweza ukawa na Uprofesa wa mchongo ila kama viatu vikubwa hata ukivaa na soksi nyingi itajulikana tuu...ona alichoongea leo ni kama vile hana washauri kabisa..
 
Huyu Jamaa Hana ubinadamu kabisa. Kila wizara anayopewa ni shida tupu. Rais mfanyie kazi hafai, hafai hafai. Aambiwe ukweli kabisa.

Sasa watanzania watajua faida za majimbo. Hii ya kukusanya makodi kwa mtu mmoja bila kuhojiwe ni shida.

Tunaomba elimu ya majimbo na magavana itolewe Sasa tupo tayari kuipigania ifanye kazi. Na mchakato uanze.
 
Serikali ya majimbo. Point taken.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA imeliona Hilo, Tuipambanie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…