Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Lameck Nchemba akiongoza kikao kazi cha kuchakata maagizo ya Rais Samia kwa Wizara hiyo.

Waziri amewaambia Wafanyabiashara nchini kote na Watanzania kwa ujumla wasiogope kuweka fedha zao Benki kwani zitakuwa salama na hazitachukuliwa.

Dkt. Mwigulu ameteuliwa hivi karibuni na Mhesh Rais Samia kuongoza Wizara ya Fedha akitokea Wizara ya Sheria na Katiba.

Hapa kazi tu & Zege halilali

MCL

=============

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha tabia hiyo kwa maelezo kuwa fedha zao haziwezi kuchukuliwa.

Dk Mwigulu ameeleza hayo leo Jumamosi Aprili 3, 2021 katika kikao na watendaji wa wizara hiyo na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hazina (TR).

“Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”

“Kodi itatozwa tu kwa sehemu ya fedha inayotakiwa kukusanywa na sisi tujenge utaratibu wa kutii sheria kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa nchi yetu.” Amesema Mwigulu.
Hapa kazi tu imeondoka na awamu yake.Sasa ni Zege halilali.
 
Yuko kwenye probation period ya kuongoza malaika, akichemka anatumbuliwa.
Hivi ni kweli alitamka akifa ataenda kuwa kiongozi wa malaika? Je, huko kuna kutumbuana? Na akitumbuliwa atarudi hapa kuwa tena shujaa wetu kipenzi?.
 
“Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”
Uongozi wa TRA umeondolewa au bado ni ule ule? i.e. Ule uliokuwa unatekeleza UNYANG'ANYI wa fedha za watu huko kwa mabenki, nk
 
Lugha yake ni kama ya ndumila kuwili vile!
Ogopa sana watu wa aina hii, wanaovaa bendera kama huyu na Lugola.
 
Back
Top Bottom