Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Hili tamko waandikiwe kabisa mabenki waandikiwe kabisa TRA wamedsababisha shida kwa wafanyabiashara mfano unadaiwa kodi umepewa order ya mzigo mteja anaweka pesa kwenye Akaunti ili umtumie mzigo au umnunulie TRA wabazibeba !!!

St Jude secondary Arusha walibeba ada za wanafunzi na ni shule ambayo wafadhili ndio hulipia wanafunzi wanaotoka familia maskini

Benki madalali wa mazao hadi wanaziogopa sababu unapewa mzigo uuze kisha umpe tajiripesa yake ukiuza umpe wakikuta pesa benki wanasomba unaonekana mtakatisha pesa au mkwepa kodi
Income badala ya kuangalia business wanaangalia hela zinazoingia kwenye account na ku zi treat kama income wakati pesa ni za customer unayemuwekea kama dalali au aliyekutumia umnunjlie mzigo
Hili la kuangalia deposts na kuziona kama business income na kudai maelezo na ku zi treat kama money laundering si sahihi zina scare depositors
Umesahau mwanzilishi wa haya ni nani?
 
Mambo ya Robin Hood,je hiyo pesa ambazo serikali iliwanyanganya au kupora pesa hizo kutoka kwenye account zao iziirejeshe
Samahani tu haitoshi.irejeshe pesa zao with interest ndio itapojenga imani kwa wananchi wake.
 
Mwigulu asiseme kwamba pesa kwenye ma bank hazitachukuliwa sababu hii itakua imekaa kisiasa zaidi ya kiutendaji..... Bali aseme ni pesa gani ambazo hazitachukuliwa ili kuwasaidia watanzania kuwa makini na pesa zinazopita kwenye mikono yao

Nchi hii inaendeshwa kwa sheria na taratibu, pesa kama zile bilion4 kasoro za TPA zitatafutwa popote zilipo na kurudishwa mikononi mwa serikali

Pesa kama zilizosemekana kukwapuliwa BOT kama ni kweli zitatafutwa kwenye accounts zozote na zitachukuliwa
Zitafutwe kwenye account gani? Yule mungu mtu wenu ndo alikuwa anatenda yote haya. Watanzania Tunapumua sasa baada ya jitu lenye roho mbaya kunyakuliwa.
 
Safi sana.
Huu ni mwanzo mzuri.
Nafikiri sasa makusanyo ya TRA ya kutegemea adhabu Penalty) yatapungua kama sio kuisha kabisa.
Wafanyabiashara walio wengi wanadaiwa mamilioni sio kwa kutolipa kodi halali,bali kwa kutofaili nyaraka mbalimbali kwa muda mrefu. Jambo hili ndio linalowaliza Wafanyabiashara walio wengi hasa wa kati na wadogo.
Hii mimi naona ndio shida kubwa inayowakabili wafanyabiashara.
Madai ya kodi kama hizi yakifutwa (waived) biashara zitasisimuka upya.
 
Moja ya Legacy ya Magu ilikua kupora fedha za wafanyaniashara kinguvu. Sasa madhara hake ndio hayo hata kupata kodi stahiki itakua ngumu sana
 
Nyooo ili mkanikate kodi sizileti ng'ooo tena sahiv nimebuni mbinu mpya nimetengeneza fire break point kwenye sehemu nilipozihifadhi ili zisiungue
 
Mwigulu anasema watu waweke fedha bank hazitachukuliwa tena. Nani anamuamini Mwigulu? Ikumbukwe yeye ni mtuhumiwa pia kwenye utawala ule dhalimu. VP wa sasa ndio alikuwa waziri wa fedha wakati pesa zinaporwa, hapo unategemea nani awe na imani na serikali ya majizi?
 
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Lameck Nchemba akiongoza kikao kazi cha kuchakata maagizo ya Rais Samia kwa Wizara hiyo.

Waziri amewaambia Wafanyabiashara nchini kote na Watanzania kwa ujumla wasiogope kuweka fedha zao Benki kwani zitakuwa salama na hazitachukuliwa.

Dkt. Mwigulu ameteuliwa hivi karibuni na Mhesh Rais Samia kuongoza Wizara ya Fedha akitokea Wizara ya Sheria na Katiba.

Hapa kazi tu & Zege halilali

MCL

=============

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha tabia hiyo kwa maelezo kuwa fedha zao haziwezi kuchukuliwa.

Dk Mwigulu ameeleza hayo leo Jumamosi Aprili 3, 2021 katika kikao na watendaji wa wizara hiyo na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hazina (TR).

“Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”

“Kodi itatozwa tu kwa sehemu ya fedha inayotakiwa kukusanywa na sisi tujenge utaratibu wa kutii sheria kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa nchi yetu.” Amesema Mwigulu.
Wizara zote Mama kapatia ila hapa tumepigwa
 
Kumbe ni kweli walinyan'ganya watu fedha zao!
Watawarudishia?
 
Back
Top Bottom