Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu Nchemba: Wafanyabiashara msiogope kuweka fedha benki hazitachukuliwa

Mwigulu asiseme kwamba pesa kwenye ma bank hazitachukuliwa sababu hii itakua imekaa kisiasa zaidi ya kiutendaji..... Bali aseme ni pesa gani ambazo hazitachukuliwa ili kuwasaidia watanzania kuwa makini na pesa zinazopita kwenye mikono yao

Nchi hii inaendeshwa kwa sheria na taratibu, pesa kama zile bilion4 kasoro za TPA zitatafutwa popote zilipo na kurudishwa mikononi mwa serikali

Pesa kama zilizosemekana kukwapuliwa BOT kama ni kweli zitatafutwa kwenye accounts zozote na zitachukuliwa
Walio kwapua TPA sio ngumbaru
 
Unawajua na kuyajua mambo yao
Ukweli ndio huo, mengine tusiumize sana vichwa. Kikubwa hapo seriakili kuziba huo mwanya kwa kubadili sheria na sera za mambo ya pesa yawe yenye uwazi. Sio watu wawili au watatu wanakuwa wana hozi mabilioni ya watanzania.. kiasi kwamba yanawapa mwanya wa kuyakwapua
 
Utawala wowote wa ccm hakuna siku utafaa katika nchi hii, wao ndio mchawi anayekuloga kisha tena kujifanya kukuagua.

Sio Samia wala Mwigulu aliyelaumu dhuluma ambayo dikteta Magufuli alikuwa akiwatendea watanzania na wenyewe walikuwa ni sahemu ya hiyo dhuluma. Leo amekufa Magufuli ndio wanajifanya kuongea huo unafiki.

Naona hata huu utawala wa sasa utafeli tu kwa sababu umezidi unafiki. Wawarudishie watu waliodhulumiwa mali zao na Magufuli kama akina mama Antonia Zakaria, Tundu Lissu, Mbowe, Kabendera, Ruge, Singa Singa nk na wajue wakiendeleza dhuluma kazi itarudiwa tena na wale wanaowakejeli kila siku kwa kuwaita mabeberu. Mzungu hashindwi kitu.
 
Mwigulu Nchemba huyu huy ndio kabadilika tena, si ndio alisema mazingira ya biasashara ni mazuri sana Tanzania? kwahio nini msimamo wa Mwigulu kwa sasa?
Amethibitisha kwa kinywa chake walikuwa wanachukua pesa za watu
Ushahidi mahakamani ...
kaanza vibaya atamaliza alivyoanza
 
Yaani hawa wote walikuwepo na bado wapo serikalini na wanajua uhalisia wa kilichokuwa kinafanywa Leo waonekane wapya kwa mfanyabiashara.

Kwa walioathirika nifunzo tosha. Tra wanasema sheria inawaruhusu kukukagua a/c miaka mitano nyuma kujiridhisha na uwiano wa kodi uliyokuwa ukilipa. Inaweza kuwa sio Utawala huu ila ujao ikaathiri.
 
Ongea na TRA vizuri Juzi nimeenda kufanyiwa makadirio km mjasiriamali mdogo,nikianza mwakajana laki moja juI naenda wananiambia Tsh 320000. Hebu imagine kutoka 100000 mwaka 2020 Hadi 320000 mwaka 2021. BAADA ya kuhoji wakasema ni maelekezo kutoka juu.
Tutatoroka wengi Sana kodi na kufunga biashara kwa mtindo huu.
 
Kumbe zilikuwa zinachukuliwa? Ni nan huyo alikuwa Ana chukua na kwa amri ya nani?unaanzaje kwenda kuchukua pesa ya mtu kwenye account yake.
 
serikali walikosea kitu kimoja, walipokua wanachukua hela kibabe kwenye account, wangehakikisha pia mtaani kuna ujambazi wa maana.

Ukiweka hela bank zinakombwa, ukiweka home, majambaka.
Tunahifadhi darini, ukiwa na shida unapanda ngazi. Tena tunaweka in USA $ na £ Sterling.
 
Back
Top Bottom