ndg wana jf salaam. Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa
1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa. Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu. Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues. Ben, look at you?
Hapo kwenye Red mbona unaendeleza mambo yako ya kutishia watu?
Mkuu Nchemba kwa post yako hii unafikiri umejitetea na kueleweka, hakika hutaweza kutubu kwa kunyamaza kimya ni lazima ukiri ili usamehewe. Naomba ujuu watanzania wa leo sio wale wa miaka ya 1961 kipindi Inaitwa Tanganyika, na nani asiejua ukaribu wako wewe na Nchimbi? Ila kwa sasa endeleeni na ukaribu wenu kwani hamna tena chemistry maana mkuu wa kaya keshamweka benchi. Ila nakusii my brother Nchemba usije ukaendelea na michezo yako michafu uliokuwa ukiicheza kipindi cha Nchimbi kwani sasa Mkuu wa Kaya ameamua kufanya substustision katika wizara ya mambo ya ndani kwakuwa hajapendezwa na mlichokifanya Olasiti na Soweto Arusha, Ulimboka, Mwangosya.
Pia unakumbuka kipindi cha kampeni za udiwani Arusha? Ulipokuja wewe na wenzako mkafanya kikao mlichozani ni chasiri katika chuo kiitwacho Help To Self Help Project kilichopo Sakina kuelekea Ollmatejoo. Ambacho kikao kilianza saa moja (07:00) jioni mpaka saa saba na robo (01:15) usiku, uku mkiwa umeweka ulinzi mkubwa kuzunguka chuo chote na kukataza watu kutumia barabara za karibu na chuo hicho.
Najua unashangaa kuipata hiii habari kwani mlikuwa mnaamini ilikuwa ni siri ila sio siri tena nikufaamishe. Kama kuna nilichokupakazia au kupotosha sema ili nilete ushaidi kamili.