Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Watanzania wana kiwango kikubwa sana cha uelewa kiasi kwamba wanaweza kupambanua kati ya uongo na kweli. Mwigulu na wenzako mambo mnayotenda dhidi ya binadamu yamevuka kiwango cha uovu nadhani shetani pia anawashangaa.
 
Ben sio mara yangu ya kwanza kufafanua hili. Siku nilipoiona tu niliandika humu na fb kuwa hiyo sio e mail yangu na wala sijawahi kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa e mail. Hapa nimeongelea ya kuwa umeitwa polisi of which nisingeongea kabla hujaitwa. Hizo siasa za kiwango cha chini mno.

Ukinitajia kuwa sijui hizo ni siasa za nini sijui huwa unaniudhi sana. Wewe ni mtu wa aina gani? Huu uliohusishwa nao ni uhalifu na ukihusisha mauaji halafu wewe unajieleza kama vile ni jambo dogo sana! Mbona unaonyesha maisha ya watu wengine hata hayakushtui yakipotea? Au kwako ni kafara?
Mwigulu, mtu mcha MUNGU na mkweli katika jamii yeyote kwanza habari hii ilipotoka tuu na kuonyesha kuhusisha maisha ya watu kupotea lazima ingemnyima raha na hata utetezi wake ungeonyesha jinsi gani kaumizwa na walao kutajwa tuu. Lakini sio wewe! Wewe ni kama vile umshtaki fisi kala mbuzi wako, utetezi wake utaonyesha kuwa hajala wako ila kula mbuzi sio issue kwake.
Hao Polisi watamuulizaje Ben kaingiliaje mawasiliano yenu bila kuwasiliana na nyinyi wenye hayo mawasiliano? Au wewe unaposema kahojiwa kwa kutengeneza e mail bandia jee hao Polisi walijuaje ni bandia bila kuwasiliana nanyi?
Kama kweli mlipanga hayo mambo, nakuhakikishia utakuwa na mwisho mbaya kisiasa na kimaisha ila KAMA yote yasemwayo unasingiziwa MUNGU atakupaisha na kuwa juu siku zote za maisha yako.
 
Mh. Mwigulu Nchemba
Ben Saanane achana naye tuachie sisi anachotafuta ni umaarufu ili ajipenyeze Bavicha; huna sababu hata moja kujibishana na mzuzuraji ambaye hana tija yoyote katika jamii; siku zote anatafuta watu wenye majina ili ajijenge Bavicha; anajua fika kiatu hicho saizi yake ikiwa kimeshinda mabwana zake wanamtumia atakiweza yeye? huyo ni mganga njaa tu hana hata kimoja cha kukubaisha unajua hawa kauzu wa Bavicha wanachotafuta ni jela ili wajipe sifa ya uhanga hiyo ndiyo njia pekee wanayoijua; kama unavyojua tangu alipokosa ajira mambo ya nje amegeuka mchungu sana na serikali ya CCM; yaani tumlipie shule kazi tusimpe? Anashindwa kuelewa tabia zake alizofanya India ndio zilizomnyima kazi; wizara inataka watu wenye maadili ambao wakipelekwa nje wanatoa sifa bora kwa bora kwa taifa. Hata hapo Bavicha hawamtaki kwa tabia zake za kinafiki ni nani anaweza kukaa karibu na nyoka wa aina yake? Mh. achana na hwa kauzu wa Bavicha wanaotafuta umaarufu kwa nguvu; mtu mwenyewe hana maana hata moja wa nini kujibizana naye?

Kheeh! Leo nimegeuka kuwa mchungu kwa Serikali na CCM kwa kuwa walinisomesha nje wakaninyima nafasi ya ajira Mambo ya nje?

Sio lazima niajiriwe serikalini?Kuitumikia nchi sio lazima niajiriwe mambo ya nje.By the way,Serikali iliyonisomesha huko ilitumia kodi ya watanzania na sio kodi ya pango ya CCM iliyohodhi mali za umma.Naomba tuheshimiane na iwe mwisho kutoa kauli za kipuuzi kama hizi

Na kama mnadhani mnakomoa vijana kwa njia hii basi subirini mwisho wenu na chama chenu katika ramani ya siasa.Kitu ambacho hamtaweza kutunyang'anya ni elimu.Hamuwezi kuhujumu taaluma ambayo ipo kichwani.Mnashangaza!
 
ukisikia Nchemba amepewa uwaziri utajisikieje?

Sitoshangaa mana sijui uwaziri watu wanapewa vigezo gani mfano Ngeleja is good katika Law ila alipewa wizara ya Madini na nadhani wakaona is under performance na ndo mana wamemuweka Muhongo who is good katika hiyo Wizara so silaumu wala sipendekezi nani apewe uwaziri na nani aachwe ila nnachoomba mpe mtu kutokana na uwezo wake katika kuongoza na pia katika hiyo wizara au ni sawa kumpa mtoto mdogo jembe akalime wakati hata kulishika ni tabu ila itabd azuge kua anaweza kubeba ili watu wamsifie kua ni Jembe au atakuja kua na nguvu baadae while he is nothing.So tunamuomba Raisi katika kuteua mtu awe anaangalia uwezo wa wa mtu katika kuongoza na hata Fani kama ni yake au lah mana Magufuli anafanikiwa kujua wakandarasi wabaya kutokana na kua na timu ambayo haiwezi kumdanganya maana anajua hayo mambo na ndo watu tunaowahitaji taifa hili sio wau wenye elimu ya kufoji

Ni ushauri tu
 
Nimeona bora niweke wazi baazi ya mipango iliyofanyika katika chuo cha Help to Self Help Project Arusha iliyosimamiwa kwa karibu kabisa na Nd. Mwigulu Nchemba. TAREHE 13/05/2013

mpango no.1
ni kuakikisha tunazuiya wanachama NA WAPENZI WA CHADEMA kutokuuzuria Mikutano ya kampeni inayofanywa na lema.
Mpango mwingine ilikuwa ni kuwaimiza ndugu na rafiki wa karibu wasiudhurie mkutato wa kuitimisha kampeni za Chadema . Na tulijariribu kuoji kwanini na yeye akasema neno moja tu "Hatari kubwa itatokea"

Tulikuwa wajumbe zaidi ya 27. Ila sipendi kuweka list ya majina yao lakini kama Mwigulu atabisha basi Nitaorodhesha baazi ya wajumbe ninaowakumbuka kwa majina na no. yangu ya sim nitatoa pia ili kuzibitisha ninachokiandika ni ukweli mtupu.

....Mkuu Usiogope Mungu yupo pamoja nawe... yaweke kwa maanufa ya vizazi vyetu vijavyo!!!

.....Leo hachomoki mtu hapa...tumechoka!!!!
 
Mods tunaomba muweke hapo juu majibu ya Kamanda Ben Saanane.

Pia Mwigulu Nchemba nakuomba umrudie Mungu hii dec kabla hujaingia mwaka mpya, Pia jitahidi uwasiliane na watumishi wa Mungu wakupe msaada wa kiroho zaid na upate na ubatizo wa maji mengi.

Cc😡Invisible
 
Last edited by a moderator:
mwigulu mwaka huu kabla haujaisha unapaswa kuokoka ,aya maisha ya duniani ni ya muda tu na ni ya kupita, laana za damu ya watu hazitakutesa wewe tu bali fikiri juu ya watoto wako kwa baadae,kaini alipo laaniwa, mpaka wajuukuu waliishi na hiyo laana,badilika mungu ni mwema ukitubu kwa kumaanisha anasamehe,usisubili mwaka huu uishe kabala ya kuchukua maamuzi magumu ya kuokoka ,vyeo vitapita ,pesa itapita ,umaarufu utapita,ila neno halitapita ,usimfurahishe mwanadamu wa kufa kesho mfurahishe mungu asiyekufa,maandiko yanasema na alaaniwe amtegemeaye mwanadamu,ivi oporesheni kama tokomeza damu za watu mnaweza kuzikimbia nyinyi viongozi na watoto wenu?
 
hata kipofu huona watu ni vipofu isipokuwa yeye wakati yeye ndo kipofu mwigulu ni mnafiki mkubwa wewe mipango yako hatafanikiwa kamwe shetani mkubwa weweee
 
Chemba ,unaonekana unakipenda sana chama kuliko Watanzania hii inapunguza heshima yako mbele ya uma.Chama kinaweza kufa,lakini nchi ikaendelea kuwepo.Unaweza kuwa maarufu bila hata ya kuwa kasuku wa chama,na maelfu ya watu wakakukumbuka kwa mema iliyoitendea nchi yako.Kuhusishwa na njama chafu kama hizi kunahalibu future yako ya siasa.Maelezo kwenye utetezi wako bado yanaleta utata.
 
Guys msihangaike kujibizana na majina haya coz hizi ni fake ID za nchemba mwenyewe mshenzi ni hatari sana huyu anajidai anajua kucheza na mtandao kumbe. Hana lolote....

* mwa 4
* stroke
* mwekundu

Na hilo jina lake mwenyewe analojidai kujibu kwa uadilifu kumbe ni muuaji. Mwigulu hufai duniani wala kuzimu..

ID ya Tawsira na Hamy D zipo reserve..
 
nilijua hutakubali. hivi kati yako na nchimbi nani kati yenu ni kiongozi hadi mpakwe matope?. hii thread haiwezi kukuondolea shutuma.
 
Kifo hicho cha Mvungi mimi nilikuwa bado kwenye dimbwi la mawazo bila kupata mwangaza, sasa kumbe nuru imeshaanza kupenyeza na pia nilikuwa sijavipatia vizuri vipengere kadhaa katika ile hacked email, sasa naona kunapambazuka na mwanga kwa mbali unajitokeza alfajiri mapema kabla ya jua kuchomoza.

Ukiwa kama kijana unaejitambua na ulienda shule ni vyema kuhakikisha elimu uliyoipata inakunufaisha mwenyewe, familia yako na jamii kwa ujumla wake. Hakuna chochote katika hili kinachothibitisha uhusika wao lakini pia hatuwezi kusema moja kwa moja hawahusiki. Kinachoniuma sana ni kuandika kuwa fulani kahusika na kuuwawa kwa flani tena kwa njia za kidanganyifu kama hii ya email. Hao watu wanakutana kila mara na wajua wazi hatari ya mitandao swali kwanini wasiyazungumze haya walipokutana mpaka ati watumiane emails kupongezana? Tizama kwenye email kuna sehemu inasema tutakutana palepale pa siku ile kweli huu si utoto wawazi kabisa? Uweze kuandika jinsi ulivyoshiriki kuua na kuhujumu upinzani ushindwe kutaja wapi mtaenda kutana na mhujumu mwenzenu ambaye mmemtaja katika mawasiliano yenu? Jamani mbona twajidhalilisha kiasi na kushusha dhamani ya elimu yetu katika kiwango kikubwa hivi? Hii ni propaganda ya kitoto au iliyntengenezwa kitoto mno pamoja na kwamba siwakatilii kuwa Mvungi ameuwawa kutoka na kazi yake aliyokuwa aifanya. Hata hivyo sishangai katika siasa ya bongo inawezekana tu. Kama mtu ajitangaza yeye ni mtoto wa Nyerere na kumkana baba mzazi mhaya kweli itashindikana kutafuta mtoka kupitia wanasiasa walio na majina?
 
ndg wana jf salaam. Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa 1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe. 2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari 3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu. 4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini. Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taif.we kwa jinsi ulivyo na roho ya kishetani hata ungejitetea vipi mbele ya uma hakuna wa kukuamini.we mchawi tu
 
ndg wana jf salaam. Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa

1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa. Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu. Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues. Ben, look at you?

Dongo Chakani,UKISIKIA AAAIIIIIII ujue limempata!!!
 
Ulijibu kwenye thread ipi hapa JF?

Pia nilipoanzisha Thread hukutoa majibu kwenye ike thread au kuanzisha nyingine kama hii kutoa ufafanuzi

Wewe kila kitu unafikiria kisiasa siasa tu hata kwenye jambo linalohusisha maisha na damu ya watu kaka.Kama hizo fikra zinakupeleka huko ni bora uache siasa

-Kwanza tangu jana nilipoulizwa kuhusu maswala ya password na hacking nimekua nikifikiria sana maana hata wewe ulishawahi kuniuliza kwa kuniandikia Inbox kama ni mimi niliye-hack account yako.Nilikujibu na kutoa ufafanuzi haraka.

Message yako ipo.Nilipoulizwa swala la hacking nikajua ndio mentality ile ile


Tuwasaidie Polisi katika upelelezi wa hili tuache siasa chafu.Tuwe wakweli na tuache kuingiza siasa kwa jambo linalohusisha maisha ya watu kwanza maana hata hilo la kuwaweka lockup vijana wa CHADEMA halijaanza leo na hili lilizidi kutusukuma wengi wetu kutaka ufafanuzi.

Narudia SMS hii nilikutumia hapa chini kuhusu thread:

"Hon'ble Nchimbi,

Mawasiliano ya Barua pepe yanayoonyesha kati ya jina la Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba kama yanavyosambaa JamiiForums na Mitandao mingine ya kijamii yanayoainisha njama ovu dhidi ya CHADEMA ni za kweli?Muda wote wahusika mmekaa kimya bila ufafanuzi sasa nimeanzisha thread ili mtoe ufafanuzi.Vinginevyo tutaendelea kuamini ni ukweli.

Mh.Mwigulu nawe umekua kimya pamoja na kuwa member wa JF na Facebook.Ben Saanane

CC:Mwigulu "

-Hatuwezi kuona vitu kama hivi vinazunguka na vyombo vya dola vikihusishwa bila majibu ya kutosha kutoka kwa wahusika halafu tukakaa kimya.Amani ya nchi inawekwa rehani

Ndio maana Polisi waliponiuliza jana kwamba huoni kuanzisha thread ike unaweza kufunguliwa kesi ya uchochezi?Niliwajibu kuwa nilichofanya ni kuzuia uchochezi maana majina ya watu waliohusishwa wangetoa ufafanuzi kama.nilivyoomba ili kuweka kumbukumbu sawa ingekua njia salama zaidi ya kuzuia uchochezi kwa nguvu na gharama ndogo zaidi.Walipooendelea kukaa kimya na kuja kutaka uchunguzi juu ya aliyevujisha au mtu aliyeweka kwenye mitandao mawasiliano hayo ni Uchochezi maana maudhui ya mawasiliano hayo yataendelea kusambaa na kuaminika zaidi maana kwa mfano hadi sasa ni mwezi mmoja umepita.


Mkuu Ben, Hakuna marefu yasiokuwa na ncha.
Ngoja tusubiri uteuzi wa mkuuu wa nchi katika wizara ya mambo ya ndani itakuwaje. Na kama atatuwekea mtu sahiii basi tutatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kukamatwa kwa watu walio husika katika mauuaji ya mabomu na utekaji ambayo mpaka sasa hatujapewa jawabu.

Nina uchungu sana kwani nimepoteza mtoto wangu katika bomu la soweto na mpaka sasa nina ushaidi usiopungua 80% Mwigulu kuhusika na kifo cha mwanangu.
 
ndg wana jf salaam. Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa

1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa. Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu. Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues. Ben, look at you?

Hv ikithibitika kuwa ni email halisi na imetoka kwako ebu tuambie.adhabu itayokufaa...ict sio mchezo
 
Kheeh! Leo nimegeuka kuwa mchungu kwa Serikali na CCM kwa kuwa walinisomesha nje wakaninyima nafasi ya ajira Mambo ya nje?

Sio lazima niajiriwe serikalini?Kuitumikia nchi sio lazima niajiriwe mambo ya nje.By the way,Serikali iliyonisomesha huko ilitumia kodi ya watanzania na sio kodi ya pango ya CCM iliyohodhi mali za umma.Naomba tuheshimiane na iwe mwisho kutoa kauli za kipuuzi kama hizi

Na kama mnadhani mnakomoa vijana kwa njia hii basi subirini mwisho wenu na chama chenu katika ramani ya siasa.Kitu ambacho hamtaweza kutunyang'anya ni elimu.Hamuwezi kuhujumu taaluma ambayo ipo kichwani.Mnashangaza!

....Mkuu Ben huyo zuzu weka pending!!!

Leo kazi moja tu kusafisha bendera ya Taifa letu....
 
Back
Top Bottom