Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Mkuu, kuusu kuzurika ilo siliofii sana, na sina hofu juu ya hawa mafedhuli kwani nilisharipoti polisi juu ya usalama wa maisha yangu na kadi yao nilishawarudishia na wanajua mimi ni adui yao na kwaatakayetaka kunifuatilia zaidi asisumbuke kunitafuta kwani mimi ni Mgonbea udiwani mwaka 2010 Arusha kata ya Elerai kwa tiketi ya ccm nilieshindwa katika uchaguzi huo na Bayo aliekuwa mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema Ambae baadae chama kiliwafukuza uanachama na wakapoteza udiwani wao yeye na wenzakae watatu.

Siogopi na wakinizuru najua watakuwa wamezidi kujipalia makaa, kwani hili swala Mbunge wangu G.Lema analijua na nguvu ya uma ipo na itafanya kazi.

...songa mbele Kamanda!!!!
 
[h=2] Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...[/h]
(mfahamu ben vizuri hapa)

Kama vijana tunaweza tukainuka na kuanza kuporomosha mashtaka na kutaja majina ya watu bila hata facts, basi kazi ipo ndugu zangu.

Ufahamu wangu ni kuwa ili tufanikiwe kuwaondoa CCM madarakani lazima tufanye kazi hiyo kama timu moja, mawazo yangu ni kuwa hatutaweza kufikia hatua yoyote ikiwa tutakuwa na vijana wa namna hii.

Vijana wa aina ya Ben Saanane wanaoweza kukaa, kutengeneza mgogoro, kubuni njia za kuuendesha mgogoro, kutafuta suluhu na hatimaye kwenda kuuza huo mgogoro kwa viongozi wengine huku akiamini kuwa anakinusuru chama hakika anakosea sana.

Vijana wa aina ya Saanane ambao kazi yao nikutumia muda na akili zao nyingi kuwarubuni na kuwagombanisha vijana wa chama na viongozi wa chama ni hatari pengine kuliko ukoma.

Kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akinitaja kwenye mijadala yake yote. Bila hata kuangalia namna ninavyohusika, na kwa kuwa na leo hii ameamua kunitaja na kunihusisha moja kwa moja, na kwa kuwa viongozi, vijana na wanachama wengi wa chadema wamekuwa wakinihusisha mimi kuwa karibu sana na zitto kabwe. leo nitasema kitu kwenye hili.

1. Naomba niweke wazi hapa leo, kuwa sikuwahi kumfahamu mtu anayeitwa Ben Saa nane kabla mwezi wa nne 2011.
sijawahi kumsikia jina wala kumuona sura yake.(hawezi kubisha kwenye hili)

2. Ben ndiye alikuwa wa kwanza kunipigia simu, kati kati ya kipindi cha kampeni za uchaguzi wa BAVICHA - 2011 mimi nikiwa nagombea uenyekiti na yeye akiwa ni mgombea wa kimkakati(alitumwa na baadhi ya viongozi kuja kuuvuruga uchaguzi-uthibitisho upo) ambapo aliponipigia simu na kunieleza kuwa tuna haja ya kukaa kama wagombea na kuangalia namna tunaweza shiriki salama kwenye huo uchaguzi kwa madai kuwa amepata tetesi makao makuu wanamgombea wao na wanajiandaa kukata majina ya watu, jina lake na langu yakikiwemo. Nilimsikiliza na kumpuuza.

3. Baada ya hapo sijawahi kuwasiliana nae tena ben saa nane, mpaka usiku wa siku jina langu limekatwa na kamati kuu ya chama, tena aliwasiliana na mimi kupitia grayson nyakarungu, aliyekuwa swahiba wake…cha kusikitisha ni kuwa mwana mkakati ben aliwashauri mwampamba, nyakarungu na kisandu kuungana, akanishirikisha na mimi. Huku nikijua dhamira yake kuwa ni unafiki. Nikamsikiliza kwa kuwa sikuwa tena na cha kupoteza (nimeshaenguliwa tayari).

Masikini ya mungu BEN akawahadaa vijana wa watu (Mwampamba na Nyakarungu) wakaenguliwa huku yeye akiwa ni wa kwanza kukiri kuwa wameamua kuongeza nguvu.

4. Unafiki wa Saanane uliendelea siku ya tatu baada ya kuisha kwa uchaguzi wa BAVICHA maana baada ya kukatwa jina langu, wanafiki wengi walifikiri ningetoa tamko la kukipinga chama ama kuhama chama, sikufanya hivyo, kwangu mimi uchaguzi ule haukuwa ligi, ilikuwa ni mechi tu ya kirafiki. Hapo mwenyekiti wa chadema wilaya ya Kibaha akaomba kukutana namimi, nikakubali, nikakutana nae ubungo plaza, tukiwa hapo tulikuwa na mwampamba na nyakarungu, aliposimuliwa saa nane kuwa tunaenda kukutana ubungo Plaza, akaandika humu jamii forums kwa kutumia ID fake yake kuwa tumekutana na mimi nina mpango wa kuhama chama.

Nlimwambia Mwampamba kuwa saa nane ana kazi maalum, mwampamba hakunielewa, akanipinga sana sana sana, naamini leo atanielewa vizuri sasa.

5. Kwa kipindi chote hicho saa nane alikuwa anaitisha vikao vya kila aina, saa nane anatukana na kutoa kejeli za kila aina kwa viongozi wa kuu hasa katibu mkuu na mwenyekiti (lengo ni kutaka kluthibitisha kuwa kuna vijana wanawapinga viongozi hawa). Ninataja maeneo machache ambayo saa nane alipenda kuitishia vikao vyake, KWA JOHN FEDHA-KINONDONI, BLUE PEARL HOTEL-UBUNGO PLAZA na LUCH TIME HOTEL-UBUNGO EXTERNAL….naomba nikiri hadharani hapa, si mimi, mwampamba wala Juliana anayemsema aliyewahi kwenda kukutana na saa nane akajinunulia kinywaji wala chakula…kwa saa nane huwa tukifika tunakula, tunakunywa mpaka tunapochoka saa nane yeye hulipia-tukambatiza jina tukamwita manji. (lakini siku zote nimekuwa nikiwaambia wenzangu kuwa kaeni chonjo na huyu jamaa ana kazi maalum---leo wamejionea)

6. kati kati mwaka jana 2011 mwenyekiti wetu wa taifa freeman mbowe alikamatwa kwa kilichodaiwa kutokutii amri ya mahakama hapa napo saa nane akafanya vitu vyake, kama kawaida yake, akawakusanya vijana wake wote ambao yupo nao kwa kazi maalum akaanza kuwajaza ujinga…naomba nikiri tena hapa kuwa usipokuwa makini ni rahisi sana kuingia kwenye kumi na nane za huyu jamaa. Ni lalzima uwe makini kama mchange kumshinda na ndio maana ananichukia sana sana.

Mimi nimefundishwa kuwafahamu wanafiki. Hasa ninapokuwa naongea nao uso kwa macho saa nane kwangu alikuwa mnafiki kwa hiyo sikumpa nafasi hata chembe.

7. katika kipindi chote hiko sijawahi kumsikia mwana mkakati saa nane akiwasema vizuri viongozi wa chadema. Mtu pekee aliyekuwa anamsifia alikuwa ni zitto.

SAA NANE NA ZITTO
Nimeshtushwa sana na maandishi aliyoyaandika Saanane leo, hii inatokana na ama kuchanganyikiwa au kujihami kutokana na kushushuliwa na kuonekana mwongo. Naomba nieleze vizuri hapa.

1. Ben Saanane ndiye alikuwa muitishaji mkuu wa vikao vya hotelini(makutano) akiwa na saa yake ya kurekodi aliyonunuliwa na kiongozi mmoja wa chama kwa kinachoitwa kazi ya ushushu. Yeye ndiy aliyekuwa mwenyekiti wa vikao na mwandishi wa kila kinachosemwa.

2. Ni BEN SAANANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7.(V4C-VOICE FOR VOICELESS) Akashawishi kikundi hicho kizunguke nchi nzima kuhamasisha viongozi wa huko kufanya mageuzi ndani ya chama. Saa nane unafiki utakupeleka pabaya.

3. Ni BEN SAANANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE (kwa kuwa nilikuwa naijua dhamira yake niliendelea kumkeli)

4. Ni BEN SAANANE ndiye aliyeshauri namna ya kuhakikisha kikundi hicho kinapata pesa, wakati mimi nilimpinga ku anzia kuanzisha hiko kikundi mpaka namna ya kukusanya kwake pesa..wakati yeye alikuwa anasisitiza kwenye njia ya kukusanya michango, tena tuwachangishe viongozi wa chama na watu wengine maarufu.

5. Akiwa mkweli atakumbuka na kukiri kuwa nilimwambia kuanzisha kikundi hicho ni sawa na kuanzisha chama ndani ya chama, aliumizwa na misimamo yangu sana.

6. Ni BEN SAANANE ndiy aliyekuwa anasisitiza tuombe kukutana na zitto kabwe ili tumuombe ufadhili wa kufadhili kikundi chetu kilichoasisiwa na SAANANE na akanipa jukumu la kuhakikisha ninamwambia na kumshawishi zitto tukutane nae tufanye nae kikao, sababu yake kubwa ni kwamba Zitto ni rafiki yangu sana na itakuwa rahisi kumpata. Hapa tulirumbana sana, mimi nilielewa dhamira yake na nikiri leo hadharani kuwa nilimshauri zitto asikubali kukutana na kikundi hiki, na niukamwambia kabisa kuwa lengo la kikundi hiki ni kuthibitisha makundi ndani ya chama.-leo yametimia.

7. Ni SAANANE aliyewaapia kujito a kwenye kikundi alichokianzisha mwenyewe kwa sababu ya kutokumpata zitto kwenye kikao, siku ambayo saa nane alipendekeza zitto tukutane naye zitto alikwenda marekani kuzindua tawi la chadema, ni saa nane ndiye aliyenilaumu sana kuwa kwa nini sikumuarifu kuwa zitto hatokuwepo, nilimjibu sio wajibu wangu kuwaambia watu kuwa zitto yupo ama hayupo.

8. Ni Saanane huyu huyu mnafiki tuliyerumbana naye hasa mimi nay eye juu ya namna ya kumshirikisha zitto kwenye michango ya kikundi chake cha PM7. Naomba ninukuu mabishano yetu..mimi ‘’ kama swala ni kukusanya pesa, kwanini tumfuate Zitto kwanza na sio mtu mwengine yeyote’’?...saa nane..’’kwa sababu zitto ni kijana na ana mitazamo chanya kwa vijana wenzie na pia tunafanana nayo mitazamo hiyo sio kamakina mnyika wao status quo’’…mimi..’’kama Zitto tumemwomba tuonane naye na amesafiri bila kutujibu hauoni kuwa anatuudharau, kwanini tujipeleke kwa zitto tunayemnung’unikia kila leo?’’..saa nane.. ’’ hapana ni lazima atusaidie, zitto kwa vyovyote lazima agombee uenyekiti, na hatuwezi fanya hii kazi tukamfungulia milango bila nay eye kutoka jasho lake, ni lazima atupe pesa’’….mimi sasa kwanini tunakataa wenzetu kutumiwa halafu na sisi tunajitumikisha wenyewe kwa zitto?’’…saa nane..’’Mchange, hakuna jinsi tunaweza acha mshirikisha zitto, mwisho wa siku zitto atakuwa beneficiary kwenye huu mpango’’… …………………ukifuatilia kwa makini mazungumzo yetu ambayo kwa bahati nzuri nimeyarekodi kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho utaweza kumuelewa SAANANE kuwa alikuwa na kazi maalum.

Niseme hapa kuwa wote kwa pamoja, saa nane na zitto kila mmoja ameniambia kwa mdomo wake kuwa hawajawahi kuonana uso kwa macho, zitto yeye anasema kuwa anaweza akakutana leo na saa nane barabarani na akapishana nae bila kumfahamu.

Wote kwa pamoja wameniambia kuwa mawasiliano yao huwa ni kwa simu hasa SMS na mara chache kwa emails.

Na moja kati ya malalamiko aliyokuwa ananipa saa nane nimpe zitto ni kuwa..
1.kwa nini hapokei simu za wapiganaji wake akiwemo yeye?...
2..kwanini anakuwa na mpiganaji kama saa nane na hataki kuonna nae….
3…kwanini hataki kukifadhili kikundi cha PM7. a.K.a V4C(VOICE FOR VOICELESS)?

Kwa mtiririko wa matukio ulivyo, na kwa jinsi SAA NANE alivyoandika mashtaka yake dhidi ya zitto huku akizani anamchafua, hakika amejidharirisha sana.

Mtu mmoja mpinzani mkubwa sana wa zitto amenitumia sms kwenye facebook, ananiambia JF vipi maana COMPUTER YANGU HAIFUNGUI..huyu nae ni mjinga sababu anashabikia ujinga.

Kumshambulia zitto kwa mashtaka ya uwongo namna hii kuna mfanya zitto awe na nafasi ya kuonekana anasingiziwa mamba mengi sana hasa ndani ya chama.

Kwa mimi ninayemfahamu Saanane nje na ndani, na ninayefahamiana na kufanya kazi na Zitto, kwa mashtaka haya ya uwongo, basi hakika nitazidi kumuamini Zitto.

Nitazidi kuamini kuwa Zitto amesingiziwa mambo mengi sana ndani na nje ya chama, ninazidi kumuamini na kumtia moyo kwamba hizi ni hatua za mwisho za watu wanaokupinga, wakishindwa kukupinga kwa facts, watakupinga kwa uwongo…saa nane amekubali kutumika vibaya kwa kisingizio cha kuwa anakilinda chama na viongozi wake.

Napata mashaka kama anakielewa anachokisema, huwezi kumtenganisha zitto na uongozi wa chama. Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama, hivyo sio rahisi kumchafua zitto ukaacha kukichafua chama.

Nimemwona saa nane anajitetea kutishiwa kuuawa, saa nane, ZITTO akiwa na mimi amenusurika kuuawa kwa ajali ya gari hivi karibuni tukitokea morogoro kwenda iringa(siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu nyerere) baada ya wapinzani wake ndani ya chama kwenda kufungua nati za tairi la nyuma ili afe, kweli zitto ameaga kwao, kweli zitto hataweza kufa kwa mipango ya mungu, hatukufika mbali tuliushtukia mchezo tukarudi morogoro mjini na zitto akaendelea na retreat yao mpaka kesho yake tukarudi dar wala hakuitangaza hii sababu aliwadharau na mbinu dhaifu.

Sio rahisi kuitoa roho ya mwanadamu mwenzio, sio rahisi kumuua zitto kama mlivyojaribu mara kadhaa na timu yenu ..

Nasikitika sana kama vijana sasa tunaeza kusimama kidete na kuandika uwongo na kuutetea bila hata woga kama ndugu yangu Saanane.

Hasira yako ya mimi kukushtukia na kuwaambia kina Mwampamba na Juliana kuwa wewe kila siku una warekodi na kwenda kuuza habari kwa kiongozi mmoja wa juu ambaye humtumia HAWARA WAKE kutuma SMS za matusi kwa watu, isiwe sababu ya kuanza kuwachafua watu ndugu yangu.

Mchafue Zitto kama unahisi una sababu ya kufanya hivyo kwa mambo ambayo una ushahidi nayo.

SAANANE acha tabia ya KUBUNI MGOGORO, KUUANZISHA, KUUENDELEZA, NA KISHA KUUTUMIA KAMA CHANZO CHAKO CHA KUPATA PESA.

SAA NANE, Waislam wanasema sifa za mnafiki tatu (ayatul munafiq thalasa).
1. akiongea huongea uwongo..
2..akiaminiwa hajiaminishi/hudhiaki..na ..
3..akiahidi hatimizi..​

Ipo siku huyu saa 8 atakimbia kivuli chake.
 
Sasa ndg yangu Mkuu ya Kaya! unavielelezo vyote khs huyo Jamaa! na mpaka umepoteza mtoto! kwanza pole kwa yt lkn bado huoni 7bu yakuanika kila kitu unachokijua Unasubiri hadi aifute ARUSHA yote kwa milipuko! Ili ubaki ww uanze kusimulia wapi vikao vilikuwa vinafanyika hujui km utakuwa umechelewa sana! Plz km kuna chochote khs mipango OVU ya Ndg NCHEMBA hebu 2pia hapa jukwaani Ukisubiri hadi akanushe huenda naww hatutakusoma tena hapa JF!


Mkuu subira huvuta heri, ila ukisubiri kwa mtu kama Mwigulu atatumaliza.
Ni hivi hii mambo ndio ipo kwenye atua za mwisho kwenda mahakamani, wakili wangu ameshakamilisha kila kitu na nina tegemea tarehe 27/12/2013 mambo yaanze.
Nilivumilia sana ila nilipoiona post ya Mwigulu subira iliniisha na nikaamua kufunguka. Ila ningependa kufunguka zaidi kwa kuleta ushaiidi lakini mwanasheria wangu amenizuiya.
 
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.

Hivi Mwigulu anaamni uwepo wa Mungu kweli..?
 
Aisee huyu jamaa ana habari nzuri kwa maslahi ya taifa, jumlisha na yule aliyepelekwa na Lema bungeni..
Tafadhari, toeni taarifa hapa au kwingineko kwa maslahi mapana ya taifa.. weka habari hapa ili kesho kila mtanzania aisome magazetini..

....breaking news...lumumba mtafutano!!!!
 
Mwigulu wewe ni mtu mwenye nyadhifa na fedha katika nchi hii na ndio hata baada ya kumpoteza mwanangu nimeshindwa kujitokeza hadharani na kwenda kukushitaki kwani ninajua nikijaribu na mimi pia nitapoteza maisha yangu. Mipango yako dhidi ya mauaji ya soweto (bomu la soweto)ninajua fika hukulifanya kibinafsi kwani ulikuwa na maslai ya chama chako na msukumo wa nguvu kutoka kwa baadhi ya watu ambao sio waaminifu serekalini.

Ila elewa nguvu uliyokuwa nayo iko siku utaikosa na upande wa pili utakuwa na nguvu na hapo ndio itakuwa muda muafaka kwangu kulipiza kisasi.

Namuomba Mungu atupe maisha marefu ili nchi hii ije kushuuudia ukilipa uliyoyafanya.

mkuu kabla mwigulu hajachukua maisha ya mtoto wetu ulishirikiana nae kuua wa2 wangapi
2)kwanini usianzishe uzi wenye ushaidi hapa?au unamuogopa?

Kuusema ukwel ni moja wapo ya njia za kumuenzi mtoto we2
 
chadema wao wangetengeneza gongo tu kwa sasa yawezekana ikawalipa vizuri siasa imewashinda kabisa.

Ndugu unajua lkn km Serikali yako imepandisha bei ya UMEME? au wenzetu nyie ndo wale tangu mnazaliwa hadi mnazeeka hamjui hata karatasi ya BILI inakuwaje!
 
Mwigulu wewe ni mtu mwenye nyadhifa na fedha katika nchi hii na ndio hata baada ya kumpoteza mwanangu nimeshindwa kujitokeza hadharani na kwenda kukushitaki kwani ninajua nikijaribu na mimi pia nitapoteza maisha yangu. Mipango yako dhidi ya mauaji ya soweto (bomu la soweto)ninajua fika hukulifanya kibinafsi kwani ulikuwa na maslai ya chama chako na msukumo wa nguvu kutoka kwa baadhi ya watu ambao sio waaminifu serekalini.

Ila elewa nguvu uliyokuwa nayo iko siku utaikosa na upande wa pili utakuwa na nguvu na hapo ndio itakuwa muda muafaka kwangu kulipiza kisasi.

Namuomba Mungu atupe maisha marefu ili nchi hii ije kushuuudia ukilipa uliyoyafanya.

Maneno yako yanatia uchungu mkuu...Pole sana..
 
Benn mwigulu hana hoja ya msingi hapo kwan yeye alikuwa wapi mpaka leo anataka kutulaghai kipumbavu namna hyo,aende akaandae buku7 za watu xmass imefka.
 
Wana JF nina hasira sana dhidi ya Mwigulu Nchemba na CCM
1:nipoteza nyumba yangu kipindi cha kampeni za kugombania Udiwani pale nilipokopa pesa ili niweze kutembea na gari aina ya Toyota Surf kipindi chote cha kampeni (siku 30) na nilipokosa udiwani nyumba iliuzwa kufidia deni na ccm ilinitelekeza

2:Nilisiriki kikao cha kuihujumu Chadema mpango ukuiwa umetoka makao makuuu ya chama ukiratibiwa na Mwigulu Nchemba na matokeo yake nikapoteza mwanangu.

Nasema hizo ni sababu tosha za mimi kupigana vita zidi ya Mwigulu na ccm yake.

Wana Jf nitakuwa nikiwapa habari kila hatua nitakayoipitia katika hii vita kwani nikienda kimya kimya watanichakachua.
 
Mbona vidhibitisho vyenu vya kusikitisha sana? Mbona hata hamjui namna ya kuonyesha email inatoka kwa account gani? Kwa nini mnajifanya wataalamu wa kila kitu? Ben Saanane i can assure it is only ICT illiteracy person that will believe those correspondences are genuine. anyway ngoja niache wajinga wawasiliane na wajinga wenzao. Poor evidence poor poor...
 
Last edited by a moderator:
Wewe Mwigulu,yatakuja yakutokee puani.Unatumia dola kufanya unayoyataka as if wewe ndio nani sijui,siamini haya yote uliyoyasema,iweje ukae muda wote huo kwa tuhuma hizi nzito? Sasa ulijuaje kama mawasiliano yameingiliwa kama huna e-mail ya aina hiyo? Hizi ni tuhuma nzito,unasubiri nini kwenda mahakamani ili ukweli ujulikane? Umekaa kujitetea Jf hii ndio mahakama?
Vp ule ushahidi wa mbinguni na duniani umefikia wap?
 
Wana JF nina hasira sana dhidi ya Mwigulu Nchemba na CCM
1:nipoteza nyumba yangu kipindi cha kampeni za kugombania Udiwani pale nilipokopa pesa ili niweze kutembea na gari aina ya Toyota Surf kipindi chote cha kampeni (siku 30) na nilipokosa udiwani nyumba iliuzwa kufidia deni na ccm ilinitelekeza

2:Nilisiriki kikao cha kuihujumu Chadema mpango ukuiwa umetoka makao makuuu ya chama ukiratibiwa na Mwigulu Nchemba na matokeo yake nikapoteza mwanangu.

Nasema hizo ni sababu tosha za mimi kupigana vita zidi ya Mwigulu na ccm yake.

Wana Jf nitakuwa nikiwapa habari kila hatua nitakayoipitia katika hii vita kwani nikienda kimya kimya watanichakachua.

Si umesema wakili amekuzuia kusema haya kwa ajili ya kesi unayotaraji kuifungua? Au amekuruhusu tena?
 
Huna lolote wewe gaidi,kila kitu HUKANA!PHD sii ujipe tuu kama shoga yako Nchimbi!
 
Wana JF nina hasira sana dhidi ya Mwigulu Nchemba na CCM
1:nipoteza nyumba yangu kipindi cha kampeni za kugombania Udiwani pale nilipokopa pesa ili niweze kutembea na gari aina ya Toyota Surf kipindi chote cha kampeni (siku 30) na nilipokosa udiwani nyumba iliuzwa kufidia deni na ccm ilinitelekeza

2:Nilisiriki kikao cha kuihujumu Chadema mpango ukuiwa umetoka makao makuuu ya chama ukiratibiwa na Mwigulu Nchemba na matokeo yake nikapoteza mwanangu.

Nasema hizo ni sababu tosha za mimi kupigana vita zidi ya Mwigulu na ccm yake.

Wana Jf nitakuwa nikiwapa habari kila hatua nitakayoipitia katika hii vita kwani nikienda kimya kimya watanichakachua.

mkuu usituudhi tumekwambia uanzishe uzi/thread ili watanzania tuelewe kinagaubaga kwa mtiririko maalum unachoogopa ni nini?
 
Ukiwa kama kijana unaejitambua na ulienda shule ni vyema kuhakikisha elimu uliyoipata inakunufaisha mwenyewe, familia yako na jamii kwa ujumla wake. Hakuna chochote katika hili kinachothibitisha uhusika wao lakini pia hatuwezi kusema moja kwa moja hawahusiki. Kinachoniuma sana ni kuandika kuwa fulani kahusika na kuuwawa kwa flani tena kwa njia za kidanganyifu kama hii ya email. Hao watu wanakutana kila mara na wajua wazi hatari ya mitandao swali kwanini wasiyazungumze haya walipokutana mpaka ati watumiane emails kupongezana? Tizama kwenye email kuna sehemu inasema tutakutana palepale pa siku ile kweli huu si utoto wawazi kabisa? Uweze kuandika jinsi ulivyoshiriki kuua na kuhujumu upinzani ushindwe kutaja wapi mtaenda kutana na mhujumu mwenzenu ambaye mmemtaja katika mawasiliano yenu? Jamani mbona twajidhalilisha kiasi na kushusha dhamani ya elimu yetu katika kiwango kikubwa hivi? Hii ni propaganda ya kitoto au iliyntengenezwa kitoto mno pamoja na kwamba siwakatilii kuwa Mvungi ameuwawa kutoka na kazi yake aliyokuwa aifanya. Hata hivyo sishangai katika siasa ya bongo inawezekana tu. Kama mtu ajitangaza yeye ni mtoto wa Nyerere na kumkana baba mzazi mhaya kweli itashindikana kutafuta mtoka kupitia wanasiasa walio na majina?
CHAMVIGA
===>Mgosi hawa jamaa unawatetea sana,mbona hawaendi mahakamani?
===>Jamani tuwe makini,kuna leo kuna kesho,kuna kupanda kuna kushuka,kuna kupata kuna kukosa, kama yalivyo maisha ya binadamu kuna kuzaliwa kuna kufa,hivyo hivyo kwenye maisha hasa ya kisiasa leo ccm wako madarakani na kesho wataondoka,nikimaanisha kuwa hawatatawala milele.
===>Wakiondoka madarakani hawataondoka na taarifa zoote kwenye vyombo vya ulinzi na taasisi zake,kutakuja watu wapya wenye mitizamo mipya,kimkakati na kivitendo. Tuombe mungu viongozi wengine watakao ingia madarakani wasiwe wenye visasi, na kama watakuwa wenye visasi hali itakuwa mbaya sana.
===>Kabla hatujafikia huko,nawaomba sana watanzania,kuna maisha baada ya hapa duniani,siasa zetu zisitusababishe tufanye mambo ya hatari ambayo mwisho wa siku yataliweka taifa hili katika hali mbaya.Kila mmojawetu kwa nafasi na uwezo wake ajitahidi sana kuepuka kucheza michezo michafu ya kisiasa, hii ni mibaya sana maana ukishiriki mara moja ni vigumu sana kuacha.
Mungu atupe nguvu na uwezo wa kuyaacha haya mabaya kwa ajili ya maisha bora ya watoto wetu hapo baadae.
 
Last edited by a moderator:
Damu za wote uliyowasababishia mauti ulemavu chini ya ulatibu wako zitakuandama mpaka unaingia kabulini na huna tofauti na kina savimbi, hitra,idd amin. Kwako tofauti ya mitizamo ni uadui sijui ni mwanasiada wa aina gani tz imepata? Unavyo wachukia cdm unatamani ungekuwa na uwezo ungewaangamiza wote kwa mpigo. Ila kaa uelewe fanya ufanyavyo lazma na ww siku moja utawafuata malehemu uliowatanguliza kabla ya muda wao anzia igunga, ndago, moro, iringa nk.
 
Back
Top Bottom