Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

Mwigulu: Sijawahi kuwasiliana na Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa e-mail tangu nizaliwe

pole sana,ndio siasa zilivyo tena siasa za Kiafrika,watu wapo radhi hata kukuwekea meno ya tembo mlangoni,ilimradi tu upatikane na hatia.
kwa technolojia ya sasa,swala la kutengeneza email na mambo mengine ni jambo rahisi sana,cha msingi ni viongozi kuwa makini.
Haya yote yanamwisho wake,tusubiri tuone mwisho wa siku polisi watatueleza nini juu ya uchunguzi wao

Mtolera.....naona una sympathise na huyu jamaa.
Tena unaongelea uchunguzi wa polisi. Kweli??! Hata wewe?

Kuna mambo ya msingi sana ningependa kuona polisi wakimaliza uchunguzi.
1) mabomu ya Olasiti na Soweto Arusha.
2) Mauaji ya watu uchaguzi wa Igunga na Arumeru mashariki
3) mauaji ya raia Arusha na mauaji ya Mwangosi.
4) Kesi za ugaidi za Lwakatare na Kileo and Co.
5) mauaji ya Dr. Msangi,
6) Kipigo cha Dr. Ulimboka

The list goes on and on......huu ijinga wa kupotezea watu musa kwa uchunguzi wa kipuuzi hautusaidii kitu.
 
Hata sisi wote ilituwia vigumu kuamini lakini baada ya Nchimbi kwenda kumshitaki Ben polisi kuwa ame hack email akaunti zao na polisi kumhoji Ben alitoa wapi Password, kwa nini tusiondoe shaka kwamba wahusika wana mikono yao kwenye mawasiliano hayo!??

Nataka kukuambia hakuna kitu!!! Upuuzi tu wa watu hapa eti na mtu na akili zake analeta sms kwenye thread anasema uthibitisho. Hivi wabongo tumerogwa? kwa nini tunajifanya tunajua kila kitu hali tukiwa wengine hatujui kila kitu? Nasema hivi hakuna kitu,evidence zenu mnazoweka kwenye hizi thread zinazohusiana na electronic correspondences hazina chepe ya kukubalika mahakamani au as cyber evidence. Ni kwamba mnajitungia upuuI wenu, mnajifurahisha wenyewe!
 
mnapenda sana kesi,hizo gharama za kesi si bola ukachimbie kisima kuliko kuzitumia kumpeleka mtu mahakamani?

Tell that to your comrade zana za kilimo who want to start a marathon to the court even before his issues are handled as per his party's organs.
 
Watu waovu mara nyingi wanapenda sana kutumia viapo kama sehemu yao ya kujitetea. Nchemba alishawahi kutamka bungeni kuwa ushahidi wake atautolea mbinguni, leo anasema hajawahi kuwasiliana na Nchimbi tangu azaliwe. Hii ni aina gani ya utetezi, hata mtoto mdogo hawezi kutumia utetezi dhaifu kama huo katika kujenga hoja. Ipo siku utaikana hata familia kwa mambo ya kijinga na kutoweka sawa kumbukumbu za mambo unayotenda yawe mema ama mabaya.

Mara zote ccm na watawala wake wanajiaminisha kuwa Watanzania ni wajinga na katika kila jambo kwalo ni upepo tu na watalisahau. Hata hivyo siku watakapobaini kuwa kila jambo linawekwa kwenye kumbukumbu sijui watajitetea vipi

Wewe acha kuchanganya mambo. Hayo ya kutoa ushahidi hata mbinguni kwenye kesi ya Lwakatare yana uhusiano gani na hizi Email za kubuni zilizotengenezwa na Ben Saanane?
 
Mtolera.....naona una sympathise na huyu jamaa.
Tena unaongelea uchunguzi wa polisi. Kweli??! Hata wewe?

Kuna mambo ya msingi sana ningependa kuona polisi wakimaliza uchunguzi.
1) mabomu ya Olasiti na Soweto Arusha.
2) Mauaji ya watu uchaguzi wa Igunga na Arumeru mashariki
3) mauaji ya raia Arusha na mauaji ya Mwangosi.
4) Kesi za ugaidi za Lwakatare na Kileo and Co.
5) mauaji ya Dr. Msangi,
6) Kipigo cha Dr. Ulimboka

The list goes on and on......huu ijinga wa kupotezea watu musa kwa uchunguzi wa kipuuzi hautusaidii kitu.

Mkuu Birigita:
Hapo kwenye Red Nafikiri ulikuwa unamaanisha Dr. Mvungi. Ubarikiwe
 
Mwigulu, Mwigulu duh,Mwigulu! Atakuwa anadanganya, ni miongoni mwa watu wasioaminika. Huu uzi wake utakuwa wa kilaghai
 
Mkuu Tedo wakipigika kabisa huwa wanalike na kukimbia kama alivyofanya ZeMarcopolo

Tatizo lenu nyie dunia yenu iko Jamiiforums. Watu wako out of town wakila maisha, nyinyi mmekusanyika hapa kuanzia asubuhi mpaka jioni mkiandika utumbo tu.
 
Mkuu Birigita:
Hapo kwenye Red Nafikiri ulikuwa unamaanisha Dr. Mvungi. Ubarikiwe

Upo sahihi......samahani kwa kosa la uandishi mkuu.

Wakina msangi ni mapolisi tu...tehe tehe teheee
 
Mwigulu ungekuwa mtu wa ajabu sana kama ungekiri kuwa umeshawahi kuwasiliana na Nchimbi katika hili. Mwisho wa kunuku!
 
hivi ukitazama yale ya oparation tokomeza, kwa nini usiamini haya ya Mwigulu na Chimbi?
 
mauaji yote yenyeutata na utekaji watu mwingulu amekuwa akishukiwa, sasa kwanini police hawamhoji??
 
ndg wana jf salaam. Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa

1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa. Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu. Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues. Ben, look at you?

MAJIBU ya BEN SAANANE

Mh. Mwigulu, supervisor haina double p, uwe makini mkuu unatafuta PhD, siyo kura!
 
Mwigulu is working for TISS kitambo tunajua hilo. Alishawahi kuchelewesha vpnd vya physics a'level Mazengo high school. Alitumwa na wanausalama kuiba computer ya mwl wetu frm USA wakihofia kuwa alikuwa leak inteligency info to the CIA.
Ndiyo maana hawezi kuhojiwa na Polccm.
 
Mh. Mwigulu, supervisor haina double p, uwe makini mkuu unatafuta PhD, siyo kura!

teh teh teh teh! umeliweza hili jitu, eti lisomi la phd.. au masomo yake ni kwa lugha ya kiswahili? mi lilivyoandika 'supp' nikajua linamaanisha supplementary (japo pia haikuwa na maana) kumbe lilitaka kumaanisha supervisor.. duh!

Ila yote yapo sawa, si unalijua na jenzake li'dkt imani tv.. limesomea czech (tamka chek) kwa kiarabu.. hapa sjui linajiita li'zee nini sjui..
 
Back
Top Bottom