Mwigulu: Tunawindwa kwenye suala la dini, mtego wake hauna mshindi

Mwigulu: Tunawindwa kwenye suala la dini, mtego wake hauna mshindi

Kwa nini hakuwakemea BAKWATA waliojikita kuishambulia TEC??
 
Nchi haina dini wauaji wasijifiche katika kivuli cha udini.

Tarehe 29 risasi zilifyatuliwa kwa watu kiholela na hakukua na maswali wewe ni dini gani ndio upigwe risasi.

Hakuna hadithi wala chochote watafanya kujisaficha katika mauaji yale.
 
Hakuna udini, tunawapinga nyie mnaowatendea ukatili Watanganyika bila kujali dini zao
Mliuwa watu wa dini zote,
Maji wanakosa watu wa dini zote
Ajira wanakosa vijana wa dini zote
Wanatekwa watu wa dini zote
Kura mnaiba za watu wa dini zote
Umesema ukweli kabisa! Wewe sio mnafiki kabisa.
 
Hao mashehe mnawaacha kwa sababu wapo upande wenu halafu mnasema huwa mnawekewa mtego!!😀

Mtu kahamasisha mchana kweupe ukataji vichwa baadae msingizie mnawindwa?

Wale wa JUMIKI/UAMSHO wangechekewa hali ingekuwa mbaya huko visiwani wa Mombasa Kenyatta aliwafyeka wote. Rogo, Makuburi etc
 
Nchemba amesema kuwa mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakitegewa mitego katika vipindi vya uchaguzi kwa kuchochewa ukabila na udini, akieleza kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka mtego wa ukabila lakini sasa inakabiliwa na hatari ya mtego wa udini.
Ndugu Nchemba mngetenda haki.
Uchaguzi huru, hakuna faulo wala wizi wa kura.
Hakuna pingamizi za kihuni wala mtego wa fomu ya maadili ya ujanjajanja, nani angepata nafasi ya kutumia udini kuwagawa watu?
Mnatengeneza tatizo mnatafuta mtu wa kumrushia lawama ambaye hausiki!
Wasingetekwa watu, zingefuatwa sheria taratibu na kanuni halali za kupitisha wagombea nafasi mbalimbali za uongozi kusingekuwa na mtu wa kuwagawa kidini wala kikabila.
Udini unaletwa na walibananga haki.
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amewaonya Watanzania dhidi ya kuingia kwenye kile alichokitaja kuwa ni mtego wa migogoro ya kidini, akisisitiza kuwa migogoro inayogusa imani za watu haina mshindi na inaweza kulivuruga taifa zima endapo haitakwepwa mapema.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Desemba 29, 2025, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko na kituo cha mabasi Bunju, Wilaya ya Kinondoni, Dkt. Nchemba amesema kuwa mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakitegewa mitego katika vipindi vya uchaguzi kwa kuchochewa ukabila na udini, akieleza kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka mtego wa ukabila lakini sasa inakabiliwa na hatari ya mtego wa udini.

Amesema Tanzania imejengwa juu ya misingi ya kuvumiliana kidini, ambapo serikali haina dini na kila mwananchi ana uhuru wa kuabudu dini anayoamini bila vikwazo, hali iliyowezesha hata familia zenye waumini wa dini tofauti kuishi kwa amani.

“Ukigusa imani ya mtu, hapo hakuna mshindi. Ukishaingia kwenye mtego huu hauna kutoka,” amesema Dkt. Nchemba, akionya kuwa migogoro ya kidini ikianza huwakumba wote bila kujali nani alichochea au nani alikaa kimya.

Waziri Mkuu amewahimiza viongozi wa dini, viongozi wa siasa pamoja na wananchi wa kawaida kutumia njia sahihi za mazungumzo na ushauri pale wanapokuwa na hoja au malalamiko, akisisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka wazi milango ya mazungumzo na yuko tayari kupokea mawazo, ushauri na hoja kutoka kwa wadau mbalimbali.

Ameonya dhidi ya tabia ya kushambuliana hadharani katika masuala ya imani, akieleza kuwa kiongozi wa dini anaposhambuliwa, waumini wake humtazama kama baba au kiongozi wa kiroho, jambo linaloweza kuchochea hasira na migawanyiko mikubwa katika jamii.
Amwambie boss wake ndiye amesnzisha huu upuuzi wa kubagua na kutweza dini za watu, hivi asiyejua kuwa wale masheHE waliomshambukia Makamu wa Rais Emanuel Nchimbi kuwa anatumiwa na TEC wametumwa Samia mwenyewe.
 
Sawa. Tatizo linakuja pale ... wale wanaozungumzia haki wanadakwa chapuchspu na kupotezwa lakini hao kenge wanaachiwa tu kuelendea na uhuni wao.

Hivi haobwanaodai kuchinja watu vichwa na Gwajima kati yao ni nani hatari kwa nchi!?
Hao masheikh uchwara ni hatar zaidi
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amewaonya Watanzania dhidi ya kuingia kwenye kile alichokitaja kuwa ni mtego wa migogoro ya kidini, akisisitiza kuwa migogoro inayogusa imani za watu haina mshindi na inaweza kulivuruga taifa zima endapo haitakwepwa mapema.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam leo Desemba 29, 2025, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko na kituo cha mabasi Bunju, Wilaya ya Kinondoni, Dkt. Nchemba amesema kuwa mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakitegewa mitego katika vipindi vya uchaguzi kwa kuchochewa ukabila na udini, akieleza kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka mtego wa ukabila lakini sasa inakabiliwa na hatari ya mtego wa udini.

Amesema Tanzania imejengwa juu ya misingi ya kuvumiliana kidini, ambapo serikali haina dini na kila mwananchi ana uhuru wa kuabudu dini anayoamini bila vikwazo, hali iliyowezesha hata familia zenye waumini wa dini tofauti kuishi kwa amani.

“Ukigusa imani ya mtu, hapo hakuna mshindi. Ukishaingia kwenye mtego huu hauna kutoka,” amesema Dkt. Nchemba, akionya kuwa migogoro ya kidini ikianza huwakumba wote bila kujali nani alichochea au nani alikaa kimya.

Waziri Mkuu amewahimiza viongozi wa dini, viongozi wa siasa pamoja na wananchi wa kawaida kutumia njia sahihi za mazungumzo na ushauri pale wanapokuwa na hoja au malalamiko, akisisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka wazi milango ya mazungumzo na yuko tayari kupokea mawazo, ushauri na hoja kutoka kwa wadau mbalimbali.

Ameonya dhidi ya tabia ya kushambuliana hadharani katika masuala ya imani, akieleza kuwa kiongozi wa dini anaposhambuliwa, waumini wake humtazama kama baba au kiongozi wa kiroho, jambo linaloweza kuchochea hasira na migawanyiko mikubwa katika jamii.
Hii inaitwa, " tengeneza tatizo Kisha ujifanye mtatuzi".
Mwenye agenda ya udini ni ccm na leo wanajifanya hawahusiki. Hizi aibu nyingine ni za kujitakia.
Ccm mkijua kulikoroga mjiandae kulinywa. Endeleeni na mwamposa na mashehe wenu na ipo siku mtajikuta mnaomboleza ujuha wenu kwa jinsi mnavyolamba makobasi ya waarabu. Mtajuta na tamaa zenu. Mwarabu siyo mtu akiingia anga zako lazima akumalize. Waulize waamerika wanaujua mziki wa mwarabu.
 
Hajamaliza ya wasanii kasharukia ya dini.Full kuhangaika.
 
Back
Top Bottom