Mwili wa Mtu aliyefungwa kwenye Kiroba wapatikana ukielea kwenye Mtaro Jangwani

Mwili wa Mtu aliyefungwa kwenye Kiroba wapatikana ukielea kwenye Mtaro Jangwani

Aisee! Hii nchi imefika kubaya sana.

Nchi iliyoitwa kisiwa cha amani tulikuwa na matatizo yetu, ila kuanzia 2016/17 tulipoteza direction kabisa ubinadamu unazidi kututoka kadri siku zinavyokwenda.

Bahati mbaya rais atakayefuata naye akikosa chembe ya ubinadamu tuitafute tena 2040 tukiendelea kumalizana kama mazombie ni muda mrefu, tabia hii itaingia kwenye DNA zetu na mbeleni hata nyama za binadamu zitaliwa mezani nchi hii.
Kwahiyo unaamini Rais amehusika?
 
Mama yenu amekuwa kama hayupo! Nchi iko hali jojo! Yamebakiza kumshika kinen... tu!
 
Screenshot_20250827_182457_Instagram.jpg

Mwili wa mtu mmoja umeonekana asubuhi ukielea majini kwenye mtaro uliopo Jangwani, jirani na kilipokuwa kituo cha mabasi ya mwendokasi.

Katika eneo hilo kwa sasa unaendelea ujenzi wa barabara mbadala kabla ya kubomolewa ya awali kupisha ujenzi wa daraja la juu litakalounganishwa eneo la Fire na Magomeni.

Mwili huo wa mtu mzima umeonekana leo Jumatano Agosti 27, 2025, hivyo kuzua taharuki kwa wananchi waliotumia Barabara ya Morogoro lililoko eneo la Jangwani.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (SACF), Peter Mabusi amesema walipata taarifa ya kuwepo kwa mwili huo saa 3:30 asubuhi, hivyo walituma timu kufuatilia.

Amesema timu hiyo ilikuta mwili wa mtu mzima aliyetambuliwa kwa jina la Swalehe Shukurani, ukiwa chini ya daraja lenye maji.

Amesema mwili huo uliopolewa na umekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom