TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Pichani ni kijana aitwaye Aziz Alumini Njombi wa huko wilaya Nanyumbu.
Huyu kijana hajihusishi na siasa wala mambo ya uanaharakati na kazi yake ni afisa usafirishaji a.k.a bodaboda.
Mnamo tarehe ya jana yaani 19/9/2024 alitekwa na mtu aliyembeba kama abilia ila inasemekana hakuwa abilia bali mtekaji.
Baadaye usiku wa kuamkia leo watekaji walipiga simu kwa mke wake wakitaka password ya simu ya mumewe.
Ila baadaye hao watekaji walimuua na leo maiti yake imeokotwa.
NB. Jeshi la polisi nchini, kutokana na kadhia hii ya utekaji raia ovyo hata vibaka, majambazi, wezi na kila muarifu wanatumia mbinu ya kuteja na kuua.
Kwa sababu inaonekana tayari ni njia iliyohararishwa wkt si kweli, ikiwa nyie ndiyo wenye jukumu la kuwalinda raia kisheria basi tunaomba ulinzi.
Vinginevyo mruhusu sasa raia wajilinde katika hali yoyote.
CC. Nawasilisha.