Mwisho wa Kariakoo huu hapa: Serikali yapitisha gulio la Wachina Kurasini

Siyo ujinga. Monopoly ni mbaya kwa mteja na competition ni nzuri.

Kama Wachina watauza kwa bei ya chini bidhaa zile zile ni heri kwa mteja. Na hilo ni jambo jema...

Turuhusu competition ya watoa huduma na makampuni. Ndivyo mambo yalivyo huko nchi za wenzetu. Monopoly ni adui!
 
Nadhani Kurasini kutakuwa na mfumo ambao upo based zaidi katika wholesale, na TRA, watakuwa sambamba sioni shida, itasaidia kukusanya mapato vizuri zaidi katika mlango mmoja, kariakoo ujanja ujanja mwingi mno, masoko ya namna hii huwa na GATE moja kubwa ambapo nyote ni lazima mpite hapo! Na kukaguliwa.

HONGERA HONGERA.
Hoja ya Kariakoo kufa haipo, Mbona kiatu karume ni 3000/- kwa Jumla na ukikiosha vizuri unakiuza mtaa wa pili kwa 10000 /-
 
Usikute hii hasara ya nchi ni katika lile dili la kumuokoa Ridhiwani asinyongwe China pale alipokamatwa na makontena ya madawa ya kulevya. Sitoshangai kama Kikwete alihusika hapa, Ridhiwani kalitia hili taifa hasara sana eti leo kawa naibu waziri?
 
Wamepitisha lini wakati Serikali ilisema imeachana na huo mpango wa Kurasini ili kuondoa msongamano?
 
Ndiyo hatari ya mikopo hiyo. Mikopo inakuelemea hadi unaanza kukubali vitu visivyo na faida kwako. Mwigulu anapiga kelele kuwa wawekezaji wanakuja kuleta ajira, ukweli ni kuwa wanakuja kupora ajira.

Bahati mbaya Serikali ina njaa sana ya pesa yoyote ili iservice madeni. Kama hadi biashara za rejareja nchini mwako zikianza kushikwa na wageni jua kuwa umekwisha. Tuendako ni kubaya sana.
 
Inaweza kuwa ni mawazo mazuri! Ila waliopitisha Wana waza sawa na wewe? Labda wawe wanapita hapa na kuchukulia maelezo Yako kuwa ni hoja Yao.
 
Si mnataka vitu vishushwe bei au?
 
Sijajua kwanini watanganyika tunaogopa sana ugeni. Wachina wakija na bidhaa zikawa bei nafuu wateja hawatakuja kutoka mikoani tu, hata nchi jirani wanaweza kuja kwa wingi. Mikoani pia biashara zitachangamka.

Cha msingi soko liwe na ukuta, kuingia bure ukitoka na mzigo clearance ifanyike serikali ipate. Huduma ziwe ni kwa jumla, serikali ya soko iwe na database ya maduka yote humo ndani na bidhaa inazouza.
 
Wachina unawajua au wawasikia?
Wale wanatakiwa waje Tanzania kujenga viwanda na si vinginevyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…