Mwisho wa Tanzania Pride: JWTZ wadhalilishwa kusubirishwa mpakani huko Rwanda

M23 na Rwanda ni pande mbili za shillingi (two faces of the same coin) hata ripoti za UN zimethibitisha hilo.

Jwtz wapo kulinda amani.
Wanalinda amani kwa kutumia kanga au wana silaha? Wamefanikiwa katika zoezi lao la kulinda amani au wamefeli?
 
Kwa hiyo wajeda wetu walienda kucheza madogoli? Wangelinda vipi amani wakati hata kujilinda wao wenyewe wameshindwa mpaka to the extent ya kukusanywa kama kuku wenye mdondo? Warudi tu waendelee na kazi wanayoiweza ya uchawa kwa Chura Kiziwi.
 
Kwasasa tuna Jeshi la Makada wa CCM, hakuna Jeshi la Wananchi pale.
 
Kwani JWTZ hatuna Chopa za kivita for evacuation.
Chopa ya kivita si inadunguliwa mazee itatua wapi wakati maeneo yote M 23 wameyazingira na kumbuka hata jeshi la DRC wamejiunga M 23 na polisi wao kwa kuhahidiwa mshahara mkubwa kuliko wa Serikali ambao ni mdogo na walikua hawapewi kwa wakati..
 
Kids of these days, you're so brainwashed. Tafuta wenyeji wa maeneo yaliyovamiwa na Idd Amin wakupe firsthand information na si habari za kusimuliwa na walimu wako wa madrasa, kwanza huu uzi hauhusu dini bali unahusu udhifu/umahiri wa jeshi letu na kilichotupeka DRC.
Tuliotembelea vijiji vilivyokuwa vimevamiwa(enzi hizo) tunajua udhalimu uliofanywa na wavamizi, tuliongea na victims ambao ni relatives na si habari zilizochujwa kwa malengo ya propaganda.
 
Hayo majibu waliyopewa ni ya kweli.
Ukiwa kwenye mkataba wa ulinzi wa amani, silaha na vifaa vya kijeshi hulipiwa na UN.
Halafu mikataba ya kiulinzi ya UN hauruhusiwi kurusha risasi hata uchokozwe.
Si bora hata kuweka masanamu basi au waende wamevaa madera badala ya full combats kama mfumo ndiyo huo wa ukupigwa kibao shavu la kulia mpe na la kushoto akutandike kibao kingine.
Peace keepers who can't keep peace hata kwao wenyewe, total rubbish.
 
Habari ni ya kweli yenye lengo maalumu. Kwanza, aliyeleta ni ''jirani'' yetu
Pili, kama mnakumbuka JokaKuu aliweka habari ya misiba na vilio Kigali.

Tatu, inatangazwa Askari wamepanda ndege Rwanda ili kuonyesha kwamba Rwanda haina tatizo na DRC

Nne, Askari walikabidihiwa na M23 kwa Rwanda bila kuwadhuru kwa maana ni majeruhi, inaonyesha ''coordination' kati ya M23 na Kigali, kwamba , M23 hawana tatizo na mataifa mengine ni watu ''wema''

Tano, tangu kikao cha Dar kilichoagiza Wakuu wa Majeshi wa Nchi 5 wakutane hakuna taarifa zaidi.

Sita, M23 wanazidi kusonga mbele bila kujua hiyo ni mbinu ya ''ku stretch'

Subirini mtasikia
 
Akili za kijinga na kujipa umuhimu msiokuwa nao, lini mateka anakamatwa na kuachiwa silaha yake? M23 wanaonekana wana ubinadamu kuwaachia mateka na kuwaruhusu kurudi Kwao bila condition yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…