View attachment 1479030
Mheshimiwa Mwita Waitara amethibitisha taarifa zilizokuwa zikizunguka mtandaoni kuwa anaumwa, lakini amekanusha kuwa ni ugonjwa wa COVID-19.
Amesema hayo akihojiwa na East Africa Radio asubuhi hii. Mheshimiwa Waitara amenukuliwa akisema "Naumwa na nimelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, kusema naumwa nini sijui kwa sababu sijapata taarifa ya wataalam, kwahiyo aliyeandika mnaweza kumhoji anaweza akawaambia aliongea na mamlaka zipi, lakini mimi taarifa za Corona sina."
"Hali yangu haikuwa nzuri sana ila kuanzia jana nimeanza ku-improve, kabla ya hapo nilikuwa siwezi hata kuongea na simu, nipo Hospitali karibia wiki sasa, naumwa tu kawaida kwani tangu nimekuwa Naibu Waziri nimezunguka sana sijawahi kuchukua likizo"