MzeeKipusa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 2,705
- 4,967
- Thread starter
- #281
Kusema cha ukweli, nilikua namfuatilia sana huyu jamaa kwasababu ya Dada yangu mkubwa, ..anamkubali sana.Maisha ya Kikristo ni rahisi semaa mtoa mada unayatia ugumu...
naamini mafundisho ya mwakasege yanakugusa that why ukaamua kuangalia.
Sikiliza mafundisho chukua yale yanayokufaa kwenye safari yako ya mbinguni yatendee kazi...
siwezi kuamini kwamba hujawai pata kitu cha kukufaa kutoka kwa huyu mwalimu.. haya mengine ni ngumu kumeza kwako yaache tuu
Niliwahi pia kuhudhuria semina zake pale Arusha uwanja wa pale kwenye reli.
Kiukweli , mafundisho yake...ngumu sana kumeza,...kwasisi ambao tumejikita katika kumeditate , kusali, kufunga na kuomba.
I mean, ..unapokula chakula chake..kisha ukarudi home..ukakicheua na kuanza kukimeng'enya UPYA ili ukimeze mazima..unajikuta unakitapika tu.
Kiufupi, Mimi huwa nawasikiliza wahubiri wote...lakini issue huwa inakuja pale kwenye kusinkisha madini yao ndani ya tumbo langu. Maana , kiukweli ninapokulaga chakula cha kweli, mwili wangu huwa unasisimka sana, unastawi na kunawili sana...nakua mtu mwenye Amani without doubts...na nakua namfurahia huyo mtu aliyenipa hicho chakula.
Mimi sio sampuli za wale waumini ambao wanapokua kwenye mafundisho ..huandika notes ..na baadae wakifika home wanazidamp kusubiri mkutano mwingine .... Mimi huwa lazima nianze kufuatilia UPYA kile nilichokisikia ( outer voice) , ni oanishe na sauti ya ndani ( inner voice). Naikubali sana sauti ya ndani