Mwl. Mwakasege: Nilienda Mbinguni nikaongea na Yesu na Musa

Mwl. Mwakasege: Nilienda Mbinguni nikaongea na Yesu na Musa

Maisha ya Kikristo ni rahisi semaa mtoa mada unayatia ugumu...

naamini mafundisho ya mwakasege yanakugusa that why ukaamua kuangalia.
Sikiliza mafundisho chukua yale yanayokufaa kwenye safari yako ya mbinguni yatendee kazi...

siwezi kuamini kwamba hujawai pata kitu cha kukufaa kutoka kwa huyu mwalimu.. haya mengine ni ngumu kumeza kwako yaache tuu
Kusema cha ukweli, nilikua namfuatilia sana huyu jamaa kwasababu ya Dada yangu mkubwa, ..anamkubali sana.

Niliwahi pia kuhudhuria semina zake pale Arusha uwanja wa pale kwenye reli.

Kiukweli , mafundisho yake...ngumu sana kumeza,...kwasisi ambao tumejikita katika kumeditate , kusali, kufunga na kuomba.

I mean, ..unapokula chakula chake..kisha ukarudi home..ukakicheua na kuanza kukimeng'enya UPYA ili ukimeze mazima..unajikuta unakitapika tu.

Kiufupi, Mimi huwa nawasikiliza wahubiri wote...lakini issue huwa inakuja pale kwenye kusinkisha madini yao ndani ya tumbo langu. Maana , kiukweli ninapokulaga chakula cha kweli, mwili wangu huwa unasisimka sana, unastawi na kunawili sana...nakua mtu mwenye Amani without doubts...na nakua namfurahia huyo mtu aliyenipa hicho chakula.

Mimi sio sampuli za wale waumini ambao wanapokua kwenye mafundisho ..huandika notes ..na baadae wakifika home wanazidamp kusubiri mkutano mwingine .... Mimi huwa lazima nianze kufuatilia UPYA kile nilichokisikia ( outer voice) , ni oanishe na sauti ya ndani ( inner voice). Naikubali sana sauti ya ndani
 
Hakuna aliyeonana na Mungu Baba akabaki salama...



Ila Yesu mbona hujifunua kwa watu Sana... Maana hata kwa Saulul alijitokeza wazi wazi...



Wewe kama kiroho upo chini usitegemee Miujiza hii na bado utaona waliomwona yesu wapigaji



kiroho kila jambo linawezekana



akili za kuambiwa changanya na zako... Zumarid anajiita mungu.. Mwakasege anahubiri habari za Mungu huoni hawa ni watu wawili tofauti kiroho
Hizi ni porojo wewe kondoo wa Mwakasege
 
Kusema cha ukweli, nilikua namfuatilia sana huyu jamaa kwasababu ya Dada yangu mkubwa, ..anamkubali sana.

Niliwahi pia kuhudhuria semina zake pale Arusha uwanja wa pale kwenye reli.

Kiukweli , mafundisho yake...ngumu sana kumeza,...kwasisi ambao tumejikita katika kumeditate , kusali na kuomba.

I mean, ..unapokula chakula chake..kisha ukarudi home..ukakicheua na kuanza kukimeng'enya UPYA ili ukimeze mazima..unajikuta unakitapika tu.

Kiufupi, Mimi huwa nawasikiliza wahubiri wote...lakini issue huwa inakuja pale kwenye kusinkisha madini yao ndani ya tumbo langu. Maana , kiukweli ninapokulaga chakula cha kweli, mwili wangu huwa unasisimka sana, unastawi na kunawili sana...nakua mtu mwenye Amani without doubts...na nakua namfurahia huyo mtu
Bora umekubali tuu
 
Kimsingi hakuna platform ya hovyo humu duniani kama JF, ni mtandao ambao umejaa wachawi na mawakala wa shetami na ndio maana kikiandikwa kitu chochote kimuhusucho Mungu, yatatokea mashambulizi na kashfa nzito sana za kila namna ila kwa umri na muda niliomtumikia Mungu nafahamu Mungu anajifunua kwa watu wengi yeyr binafsi na pia kuwafunulia kuhusu mbingu. Binafsi, nashuhudia kumuona mwenye haki Yesu Kristo si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo. Pia nashuhudia, Mungu kunifunulia na kuiona mbingu.

Kuhusumbingu, nakumbuka ilikuwa 2016. Siku hiyo niliamka kama kawaida saa 9 alfajiri na kusali. Ilipofika saa 11:45 nikasema nilale ili nikiamka niende kazini. Nilipolala kama saa 12 alfajiri niksona Malaika ananiambia nimetumwa nikufuate. Akanishika mkono, nikaoba natoka kwenye mwili upande wenye moyo. Nikapita kwenye bati la nyumba bila kizuizi. Safari ya kupanda juu ikaanza kwa speed ya ajabu. Nikaangalia chini na kuona mwili wangu, mke na mtoto wangu wamelala kitandani. Unaona nyumba na miti ya duniani, unaona kadunia kalivyo kadogo then unafika katika nchi ile ambayo "watu" wanaimba na kuabudu na tuliimba "Bwana Mungu nashangaa kabisa"

Sijui nielezeje muonekano wake nchi ile ila ni nzuri na ya meta meta. Hali ya hewa na mazingira ni tofauti na huku duniani. Nchi ile ni kweli na mji ule ni kweli. Jitahidi usikose kuingia mji ule.

Baadaye nikaambiwa turudi na kwa speed ya ajabu, najikuta naingia mwilini mwangu upande wa kushoto kwenye moyo, mwili ukawa kama umepigwa "shot" nikashtuka.
Mmmh
Screenshot_2023-04-19-22-47-59-366_com.whatsapp.w4b.jpg
 
Hata Mimi nimemsikia.tena anasema alikuwa anaumwa wakati huo kalala kitandani
Sasa mbona kuna kondoo wake hawataki kukubali alitamka habari hizo za yeye kwenda Mbinguni?
 
Acheni pigo hizi. Na usinichukulie poa kabisa bob! Mimi ni level zingine kabisa. Na kiufupi , nilishawahi kutokewa na Yesu nikiwa kwenye ndoto....na aliniokoa kutoka kwà watu wa giza.

Alikua akisema nami kwà lugha ya ishara tu. Vazi lake lilikua jeupe sana linawaka kama taa!

Kama Yesu asingenitokea kwenye msitu ule wenye giza totoro...wale watu waliokua wananikimbiza gizani na nikawa nakimbilia nisikukujua...wangenikamata sidhani kama ningekua hai mpaka sasa.

Lakini aliweza kuniokoa pale tu walipotaka kunikamata.

Kesho yake nilivyostuka usingizini.....Nikajikuta safari yangu inakua nyepesi sana kwani nilikua stranded katikati ya maadui ( BhokoHaram) huko nchini Cameroon. ( enzi hizo Hao jamaa walikua wameisha penetrate mpaka Cameroon)
Daaah! Nilihisi nimeshasikia yote kumbe ndio kwanza kunakucha
 
Hiyo ndio Demokrasia ya kufunguliwa kwa nchi,sasa manabii ruksa wanaenda hadi mbinguni na kurudi,nani kama mama!
 
Daaah! Nilihisi nimeshasikia yote kumbe ndio kwanza kunakucha
Confidence = training + experience.

"Mimi sitishwagi, Wala sitingishikagi" in Magufuli's voice.

Nimeona mengi sana katika maisha yangu. Na nimepata bahati ya kumeet na wachungaji wakubwa sana hapa duniani...

Nilikua kama zombie kuwafuatilia hao watu lakini nilipoanza kujisimamia...kujipa likizo ya kutowasikiliza kwà muda , huku nikijikita katika kuisoma Biblia na kutafsiriwa via my inner voice....,

Nilipomaliza likizo na kuanza kuwasikiliza tena...ikawa ngumu sana kumeza madesa yao. #Most of them , they do preach sugarcoated teachings kwà ajili ya kushibisha matumbo yao + kutafuta umaarufu + kick ( kwamba wakisema wameenda mbinguni ndo eti waonekane wanaupako sana....lakini wanachokifanya..ni zero , miujiza ya kulazimisha watu kutembea)
 
Kwahiyo zumaridi yuko sahihi?
What a nice question.

Ujue watu wanafikiri mbinguni ni pa mchezo mchezo tu. Yani roho Yako iende kule afu irudi huku then ubaki kuwa ordinary tu...

Aah..huo ni uongo bhana! Uongo huo bhana!!! Mimi sitaki bhana huo uongo wenu bhana!
 
Sasa mbona kuna kondoo wake hawataki kukubali alitamka habari hizo za yeye kwenda Mbinguni?
Kukubali au kukataa NI suala la mtu binafsi.Huwezi kumlazimisha mtu aamini kile unachokisema.Mimi nimemuamini kwa SABABU alikuwa mgonjwa Yuko kitandani Ina maana alikuwa hoi
 
Kwahiyo zumaridi yuko sahihi?
Siwezi kuzungumzia usahihi wa Zumaridi kwakuwa simuamini, kwa sababu kadha wa kadha,hata hilo la kusema kaenda huko alichanganya mambo mengi mara kutaka kuolewa na Paulo,mara kuna nyimbo za msanii Fulani zinapigwa huko,wote tunajua Yesu alishasema mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.

Nilichosema ni kwamba kwenda mbinguni kwa mtu mwenye Ushirika na Mungu inawezekana,Sasa inategemea aliyeenda unamuamini vipi na alichosema kinaendana na maandiko au La.
 
Back
Top Bottom