Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Mwl Mwakasege: Niliwahi kutoka nje ya mwili wangu nikaenda Mbinguni na kukutana na Nabii mkubwa, nikamtambua

Endelea kukaa gizani ukimtumainia mganga na visomo vya majini ,mwisho wa hayo ni kuzimu.
Hivi Kwa akili yako unaamini kwamba nabii Mussa na huyo anayejiita nabii uchwala wanajuwana?
 
kuna peponi na motoni tu.elewa wewe chizi
Mahali pema peponi Yesu aliingia hapo,

Baada ya kufufuka Kwa Yesu aliondoka na WATAKATIFU wote na kwenda nao Mbinguni,

Baada ya kufufuka Yesu hata sasa, hakuna tena kusubiri Mahali pema peponi.

Uwe unaelewa.
 
Mahali pema peponi Yesu aliingia hapo,

Baada ya kufufuka Kwa Yesu aliondoka na WATAKATIFU wote na kwenda nao Mbinguni,

Baada ya kufufuka Yesu hata sasa, hakuna tena kusubiri Mahali pema peponi.

Uwe unaelewa.
unaropoka kama chizi flani hivi
 
I think nilishachangia huko nyuma ni ya zamani!
Halafu ku-deal na watu wasioelewa mambo ya kiroho ni kazi sn

Bible ipo wazi hakuna jipya alilolisema mwalimu hapo japo kachukua kipande angeweka SoMo zima watu waelewe
Pili,sitaki unajisi mkuu
Nimekuelewa vzr sanq, Mtumishi
 
Sijui kama humu watakuelewa! Wataona una matatizo ya Afya ya akili.
Mungu anamtafuta mtu mmoja tu katika Uzi huu,

Na ndio Nia ya Mchungaji kuacha kondoo 99 na kumfuata kondoo mmoja aliyepotea.

Na mtu huyo mmoja anayetafutwa atapatikana Kwa uweza wa Mungu, na mtu huyo ni asomaye na kusikia sauti ya Mungu.
 
Tumia akili roho ni spirit kwa kiswahili ni ROHO kwa kidini ni SPIRIT kwa kisayansi ni ENERGY....usichanganye mambo NASFI ni ufahamu wa kujitambua ndiyo nafsi ....mara nyingi watu wanachanganya roho na nafsi ...bitu vyote ni roho hata mungu ni roho na ufalme wake wote ni roho ...ufalme wa mungu ni ni vitu vyote ni uwezo wote ni nguvu xote ni uzima wote nk...hiyo neno SPIRIT NDIYO KILA KITU HAKUNA KISICHUKUWA SPIRIT YAANI ENERGY
Kwa hiyo hapa unajibu sayansi au unajibu theology mbona hueleweki.

Mimi nimetumia maandiko kukwambia kuwa nafsi ni muunganiko wa mwili la roho then wewe unakuja na pumba pumba zako hapa mara kingereza ni spirit mara kiswahili ni roho mara kisayansi ni energy ndiyo nini.

Hapa discussion ni theology toa majibu ya ki-theology siyo kubwajaja mara kidini mara kisayansi mara kingereza.
 
Sasa Mbinguni ndipo tulipotokea kabla ya kuvaa miili hii ya nyama na Kuzaliwa,

Kuongelea habari za Mbinguni ambako ndio nyumbani kwetu,

Si kutafuta headlines,

Ni kukumbushana kuwa duniani ni pa kupita tu.

Weka picha kuthibitisha.
 
Siri za Mungu kupitia neno lake hazifunuliwi kupitia common sense!
Still more this is a free forum for whoever wants to participate na hizo "siri za Mungu" ndiyo ujinga gani? Mungu anaogopa kitu gani kuweka mambo yake bayana mpaka yawe siri, huu ubishani wa kipuuzi usingekuwepo japo hata achomoze kichwa kutoka kwenye mawingu atusemeshe kuondoa utata ili shetani awe ameishindwa jumla? Kwani akijificha na wengi kwa kutokumuamini wakaenda jahanam(motoni🥺🥺) anapata faida gani?
 
Salaam, Shalom!!

Akifundisha katika semina jijini Mbeya Jana tarehe 26 January,Mwalimu Christopher Mwakasege amerudia kauli aliyowahi kuitoa kabla.

Amesema, asubuhi, walipokuwa katika bible study ya familia asubuhi ya jumapili hiyo, Mkewe alimuuliza swali kuwa ikitokea ametokewa na YESU atamtambuaje?

Mwalimu Christopher Mwakasege akamjibu Kwa kumkumbusha juu ya siku aliyotoka ndani ya MWILI wake na kwenda Mbinguni, alipofika Mbinguni, alikutana na Nabii Musa yule Nabii wa kale, na alimtambua, akaongeza kusema, Ukiwa katika mwili wa kiroho, huhitaji kutambulishwa sababu Roho inajua yote na kutambua yote yajayo na yaliyokwisha pita.

..... Mwisho wa kunukuu....

Naungana na Mwalimu Christopher Mwakasege juu ya UKWELI wa jambo hili, mbingu IPO na ni halisi, Mimi pia nimewahi kwenda Nchi nzuri sana, mfano wa uzuri wa Nchi Ile hauelezeki, mji huo hakuna jua Wala mwezi, IPO Nuru nzuri sana ambayo macho hayachoki kuitazama,

Nimewahi kuandika pia juu kupewa taarifa juu ya ujio wa Yesu kulinyakua Kanisa Kwa kumwona Yesu akiwa na jeshi la Malaika, amepanda farasi mweupe wakienda Kwa Kasi mawinguni.

Ndipo tujue yafuatayo.

1. Mbingu ni halisi Si hadithi.

2. WATAKATIFU wote wapo Mbinguni, wakifa hawakai kaburini.

3. Mungu yupo na ni MMOJA, na Jina la Mungu huyo mmoja tulilopewa WANADAMU liwezalo kuokoa ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH.

Mungu awabariki.
Katika watumishi wa Mungu ambayo nawaelewa kuliko kitu kingine ni Mwakasege... Mungu ampe maisha marefu sana mwambie😊
 
Ni kweli Mungu yupo japo wapumbavu watakaa mimi binafsi nilimuona Mungu akiwa na hasira na akiwa mpole .


1: Siku akiwa kawaka hasira nilikua na lazimisha jambo ambalo halikua langu na alikuja hadi malaika ( sina uhakika kama yule alikua malaika au ni Yesu pekee) na sura haikuonekana ila mwili ulionekana na hakua na rangi tulizo nazo sisi binadamu ila akiwa juu ya farasi mweupe akikinga ukinzani wa hasira iliyokuwa iniwakie mithili ya hadi mimi mwenyewe kuanguka chini ni kiwa na hofu kuu

2: Na siku alokua mpole alikua ananipa majibu ya jambo nililokua nikilazimisha baada ya kuanza kukata tamaa kabisa kiasi cha kutaka kudhihaki. Alinitoa magamba kwenye macho yangu na kunivua ngozi ilokua imenivika nikawa mpya .. kuna vitu sikuviona kwa macho ila nilisikia vikivuliwa kutoa utosi wa kichwa mpaka vikawa vinashuka ardhini na kupotelea huko.


Nb. MUNGU YUPO NA WAAMBIENI PIA NAWAAMBIAGA WATU NINAVYO ONA SASA HIVI SIVYO NILIVYOKUA NA ONA AWALI HAWANIELEWI ILA NDIYO HIVYO
Basi farasi inabidi waheshimiwe kwa kuwa ndiyo usafiri wa mbinguni(peponi), tatizo sisi binadamu tunawachukulia poa.
Farasi weupe 🐎🐎 wapewe status kama wanayopewa malaika.
 
Mungu anaonekana kwa macho yote mkuu, ukitaka kumuona kwa macho ya nyama anakuja na ukitaka kumuona kwa macho ya rohoni anakuja ila kuna namna ya kumuita na umtake asinyamaze, pia ukitaka kuongea nae kirafiki mnaongea kabisa ila kama unajua haupo sawa sawa kuna mawili upigwe au unusurike hakikisha una kinga hata akiwa na hasira Yesu akusaidie kuzuia hiyo hasira tofauti na hapo asee usijaribu
mpumba + vu =?. Jawabu ndo wewe
 
Yuko mfalme mwingine kibiblia anaitwa mfalme wa anga.Ukimwona huyu huwezi kumwona Yesu.Jitahidi uache ganja na kuanza kumtafuta Yesu ni rahisi tu
Hata huyo wa anga sijawahi kumuona
mara nyingi kupitia med ya ganja huwa nikienda mbinguni najikuta nipo na kama pacha wangu yaan najikuta mimi mwenyewe..

kuhusu ganja siwezi acha inanisaidia mambo mengi sana!
 
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuhusu siku ya kiama alisema 👉hata mwana hajui ila baba ....wanafunzi wake wakadhani kasemq yeye ajui siku ya kiama wakaacha kumsumbia kwa kumuuliza uliza kumbe maana ya yale maneno ya Yesu kuwa mwana hajui alimaanisha mwili haujii ila baba ( yaani nafsi inajua) kasome upya injili yote kwa kutumia fafanuzi nilizo kupa utajua ukweli wa haya ninayo kuambia na utajua kuwa injili imenyoka....vizuri sana sema watu mmeshindwa kujua yesu na mungu na roho mtakatifu ni nini?
🙂🙂🙂

Hivi hii biblia inafasiriwa kwa mtazamo wako uonavyo wewe au jinsi theology imemaanisha.

Na yule aliyepaa mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu Baba mwenyezi ni nani
 
Back
Top Bottom