TANZIA Mwl. Samson Kibaso, mtunzi wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Afariki Dunia

TANZIA Mwl. Samson Kibaso, mtunzi wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Afariki Dunia

😆😆😆! Mtumishi iko siku nakunywesha mi "image" wewe😛!
Mara moja moja ijumaa na j'mosi navinywa hivyo vidude, japo sukari yake iko juu sana, vitanishinda.. ilà upatapo wasaa ukuje tuvinywe wote, it'll be memorable hakyanani!!
 
Mara moja moja ijumaa na j'mosi navinywa hivyo vidude, japo sukari yake iko juu sana, vitanishinda.. ilà upatapo wasaa ukuje tuvinywe wote, it'll be memorable hakyanani!!


Mwinjilisti unayumbaaaa🤸🤸🤸🔥🙃
 
Ni nani mtunzi wa wimbo wa EAC?

View attachment 1494332
PICHANI: Mwl. Samson Kibaso enzi za uhai wake.

Kuanzia 1999 hadi 2010 EAC ilikua ikitafuta wimbo rasmi wa Jumuiya hiyo. Aliyekua Katibu mkuu, Balozi Juma Mwapachu alikiita kipindi hicho "a decade-long search for a song that East Africans would call their own". Yani muongo mmoja mrefu wa kutafuta wimbo rasmi wa EAC. Watunzi zaidi ya 1,000 walipeleka nyimbo lakini hazikukidhi vigezo.

Kuna Mwalimu maharufu sana kwenye ufundishaji wa nyimbo za injiri anayetoka kanisa la waadvetista Wasabato anajulikana kama Mwalimu Kibaso, majina yake kamili ni Samson Kibaso mnamo mwaka 2010 alipeleka wimbo wake ambapo baada ya kupitiwa na jopo la wataalamu, ukaonekana unafaa.

Baadaye mapendekezo yakawasilishwa kwenye mkutano wa 12 wa wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki ulioketi tarehe 03/12/2010 na wimbo huo ulipitishwa na kukubarika.

Kwa wale wadau wa njimbo za injili wa makanisa ya KKKT, Angrikan nk wanamfaham gwiji huyu katika ufundishaji wake, lakini hakuna mahali popote huyu Mwl. Kibaso anapokumbukwa kwa kazi hii kubwa, ukifuatilia hata serikali yetu ya Tanzania nadhani wamesahau au labda hawajui hili.

Kwenye website ya Jumuliya ya afrika Mashariki imeelezea historia ya wimbo huu lakini hawajataja mtunzi wa wimbo huo na haifahamiki ni kwa makusudi au bahati mbaya lakini wabunge wetu wa EALA walitakiwa wahoji na kutoa ufumbuzi.

Pamoja na yote gwiji huyu Mwalimu Samson Kibaso amefariki dunia wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na jana amezikwa huko kwao Rorya Tarime mkoa Mara na serikali imeshindwa hata kutoa pole kwa familia.

Najaribu kuwaza angekua Mkenya ingekuaje? Nina uhakika serikali ingeubeba msiba wake na ingekua habari kubwa sana Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta angeshiriki na viongozi wengine wa EAC wangeungana nae. Main stream media zingeifanya habari hiyo kuwa "lead story" na ingezaa "developing stories" nyingi. Zingeandaliwa makala kuhusu EAC kukosa wimbo na jinsi Kibaso alivyookoa jahazi baada ya miaka 10.

Lakini sisi tumechukulia kirahisi na kuona ni jambo la kawaida tu, serikali imeshindwa kumtambua late Mwl. Samson kibaso akiwa hai na bado imekataa kumtambua akiwa maiti, Eeh Mungu utusamehe kwaheri Mwalimu Kibaso, asante kwa utumishi wako kupitia uimbaji na umeacha alama isiyofutika!.



Appr: Mwl/Pr. Ezra Juma.
Credit to Malisa GJ
 
Ameumaliza mwendo, mtaalamu na mtunzi mbobevu wa nyimbo Samson Kibaso. Pole kwa familia, kanisa la Waadventista wa Sabato kwa ujumla na kwaya ya Kurasini
Nilijua umeongozana na ndg, jamaa na marafiki kumsindikiza!.
 
Ee Mungu twaomba uilende, Jumuiya Afrika Mashariki...

Nakumbuka nikiwa chuo ilikua ndo wimbo wetu, maana tulikua mataifa mengi. Sikuwahi kuusikia kabla, ila sasa ni uko moyoni.

Subuhanallah! "ila sasa ni uko moyoni"


Ndugu yangu Muislamu, unapotea,,,,achana na hayo manyimbo yasio na faida yoyote,,soma Qur'an ndio kila kitu.
 
Ee Mungu twaomba uilende, Jumuiya Afrika Mashariki...

Nakumbuka nikiwa chuo ilikua ndo wimbo wetu, maana tulikua mataifa mengi. Sikuwahi kuusikia kabla, ila sasa ni uko moyoni.

Subuhanallah! "ila sasa ni uko moyoni"


Ndugu yangu Muislamu, unapotea,,,,achana na hayo manyimbo yasio na faida yoyote,,soma Qur'an ndio kila kitu.
 
Oooh! pole sana wanafamilia, pole ya kupoteza, pumzika kwa raha na amani ya Milele Mwl. Kibaso!
 
Msiwe mnakurupuka,mazishi yake yamehudhuriwa na Mkuu wa mkkoa wa simiyu,na naibu waziri mwita waitara
 
Back
Top Bottom