Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kwa ukumbusho,Subuhanallah! "ila sasa ni uko moyoni"
Ndugu yangu Muislamu, unapotea,,,,achana na hayo manyimbo yasio na faida yoyote,,soma Qur'an ndio kila kitu.
mnagongaMwinjilisti unayumbaaaa🤸🤸🤸🔥🙃
Yes...wasabato mnagonga divai kiaina eeh hatari sana
mnagonga
ha ha angalia wasikufute ushirika ila rudi nyumbani sasaYes...
Nimezaliwa huko nikaja angukia rc!ha ha angalia wasikufute ushirika ila rudi nyumbani sasa
Mimi pia nimezaliwa humo na still nipo humo,dada yangu ameenda timna nae kama ww ha haNimezaliwa huko nikaja angukia rc!
Narudi...nishaanza safari ya kurudi!..Mimi pia nimezaliwa humo na still nipo humo,dada yangu ameenda timna nae kama ww ha ha
Tunakuombea urudi nyumbani hasa kwenye makambi ya mwaka huuNarudi...nishaanza safari ya kurudi!..
Comment zako kwa cc tuliosoma falsafa tunazielewa Sana.Nashanga mzalendo kama wewe humjui. Tanzania mshazoea kuwasikia Mondi, Harmonize.
Nashangaa mpk muda huu viongozi kimya na hutawaona msibani cc:msiba wa meneja fulani
Ova
Pole mamaYaani nimelia mimi nimelia sana sijui nisemeje kuhusu Kibaso! Rip Kibaso!
The power of love hiyo, haha!!Narudi...nishaanza safari ya kurudi!..
Hasa waimbaji wa nyimbo za Noten R.I.P Mwendo umeumaliza kampumzike salamaNi nani mtunzi wa wimbo wa EAC?
Kuanzia 1999 hadi 2010 EAC ilikua ikitafuta wimbo rasmi wa Jumuiya hiyo. Aliyekua Katibu mkuu, Balozi Juma Mwapachu alikiita kipindi hicho "a decade-long search for a song that East Africans would call their own". Yani muongo mmoja mrefu wa kutafuta wimbo rasmi wa EAC. Watunzi zaidi ya 1,000 walipeleka nyimbo lakini hazikukidhi vigezo.
Kuna Mwalimu maharufu sana kwenye ufundishaji wa nyimbo za injiri anayetoka kanisa la waadvetista Wasabato anajulikana kama Mwalimu Kibaso, majina yake kamili ni Samson Kibaso mnamo mwaka 2010 alipeleka wimbo wake ambapo baada ya kupitiwa na jopo la wataalamu, ukaonekana unafaa.
Baadaye mapendekezo yakawasilishwa kwenye mkutano wa 12 wa wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki ulioketi tarehe 03/12/2010 na wimbo huo ulipitishwa na kukubarika.
Kwa wale wadau wa njimbo za injili wa makanisa ya KKKT, Angrikan nk wanamfaham gwiji huyu katika ufundishaji wake, lakini hakuna mahali popote huyu Mwl. Kibaso anapokumbukwa kwa kazi hii kubwa, ukifuatilia hata serikali yetu ya Tanzania nadhani wamesahau au labda hawajui hili.
Kwenye website ya Jumuliya ya afrika Mashariki imeelezea historia ya wimbo huu lakini hawajataja mtunzi wa wimbo huo na haifahamiki ni kwa makusudi au bahati mbaya lakini wabunge wetu wa EALA walitakiwa wahoji na kutoa ufumbuzi.
Pamoja na yote gwiji huyu Mwalimu Samson Kibaso amefariki dunia wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na jana amezikwa huko kwao Rorya Tarime mkoa Mara na serikali imeshindwa hata kutoa pole kwa familia.
Najaribu kuwaza angekua Mkenya ingekuaje? Nina uhakika serikali ingeubeba msiba wake na ingekua habari kubwa sana Afrika Mashariki.
Rais Kenyatta angeshiriki na viongozi wengine wa EAC wangeungana nae. Main stream media zingeifanya habari hiyo kuwa "lead story" na ingezaa "developing stories" nyingi. Zingeandaliwa makala kuhusu EAC kukosa wimbo na jinsi Kibaso alivyookoa jahazi baada ya miaka 10.
Lakini sisi tumechukulia kirahisi na kuona ni jambo la kawaida tu, serikali imeshindwa kumtambua late Mwl. Samson kibaso akiwa hai na bado imekataa kumtambua akiwa maiti, Eeh Mungu utusamehe kwaheri Mwalimu Kibaso, asante kwa utumishi wako kupitia uimbaji na umeacha alama isiyofutika!.
Appr: Mwl/Pr. Ezra Juma.
----
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mwalimu na mwimbaji wa kwaya ya SDA Kurasini mwalimu Samson Kibaso kabla ya mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Ingrichini Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara.
Mzalendo wapi huyu njaa kali wazalendo wapo wamekaa kimya wanawatizama huku wanatikisa miguuNashanga mzalendo kama wewe humjui. Tanzania mshazoea kuwasikia Mondi, Harmonize.
Nashangaa mpk muda huu viongozi kimya na hutawaona msibani cc:msiba wa meneja fulani
Ova
Ongeza na Zitto.Tangu mwaka 2015 adui wa Tanzania ni
1.Chadema
2.Ujinga
3.Maradhi
4.Umasikini
Nimecheka sanaMzalendo wapi huyu njaa kali wazalendo wapo wamekaa kimya wanawatizama huku wanatikisa miguu
Asante kwa ukumbusho,
Lakini nna moja la kushangaa. Huu muda ulopita kufungua, ukasoma huu uzi ungekua umehifadhi aya ngapi ama umeleta stighfaar mara ngapi.
Tujue kuwa na kiasi, usikurupuke katika kila jambo.