Mwongozo wa Serikali: Kipimo cha Corona ni Dola za Kimarekani 100 kwa anayesafiri nje ya Nchi

Mwongozo wa Serikali: Kipimo cha Corona ni Dola za Kimarekani 100 kwa anayesafiri nje ya Nchi

Sisi hatuna corona kwa mujibu wa serikali ilitakiwa watanzania wapewe hivyo vyeti maana sote hatuna corona halafu watalii ndiyo wapimwe maana kuwapima watanzania ni kana kwamba taarifa ya kuwa hakuna corona itakuwa siyo sahihi
Hakika ni kuwaonea wataanza na hili ni wivu wa mabeberu
 
Duu!! Aisee!!! hivi kama kupima covid 19 ndy dola 100 $ hivi hiyo chanjo ikija si ndy tutachanja kwa dola 1000 $ kabisa?..
Mtanzania wa kawaida anaenda Belgium, Canada au USA kutafuta nini
 
Umeelewa?, Ukitaka kwenda nje ya nchi, sasa unaongelea mambo ya mtz wa kawaida, ataenda huko kufanya nn?
Duu!! Aisee!!! hivi kama kupima covid 19 ndy dola 100 $ hivi hiyo chanjo ikija si ndy tutachanja kwa dola 1000 $ kabisa?....
 
Hii ni kituko cha Karne. Na hali kuwa mbaya, huduma ambayo inatolewa bure duniani kote, hadi kwenye airport za nchi mbalimbali bure, kwa masikini wa Tanzania, ni kukamuliwa. Taarifa toka wizara ya Afya, inaelekeza kwamba kila anayetaka kusafiri, kupima Covid-19 lazima alipe $100

D O L A 100....... ay hefdha za kitanzania Laki 239,000. Hii ni Zimbabwe inatunyemelea au kuna tatizo gani?
wasafiri wa nje ya nchi hawana njaa kiasi hicho,labda kama wanaenda kuomb omba nje huko.
 
Kiasi kilichotajwa na serikali ni rahisi kulingana na clinic binafsi zilizopewa ruhusa ya kufanya test ya corona Nchini Uingereza.
Serikali ya Uingereza inawafanyia bure wananchi wote waliopo uingereza lkn imepiga marufuku kutumia majibu wanayokupa kwa ajili ya kusafiria.

Clinic binafsi zinatoza kuanzia pounds 100-300 kutegemea na uhitaji wako wa haraka. Nchi nyingi ambazo zina makampuni makampuni makubwa ya ndege waliamua kutumia mtindo huu ktk kipindi hiki cha majira ya baridi baada ya kuona maambukizo yanazidi kushamiri.

Mi nimeingia na KLM jana kutoka UK...kabla ya ku check in inatakiwa uoneshe majibu ya test yaliyofanya kwa kipimo cha PCR na pia kuna fomu wanakupa uijaze taharifa za wapi ulipofanyia hiyo test.

Na muda wote ukiwa kwenye ndege hutakiwi kuvua barakoa. Watoto wenye umri mpk miaka 12 ndio wamepata msamaha wa kufanya hii test.
 
Umeelewa?, Ukitaka kwenda nje ya nchi, sasa unaongelea mambo ya mtz wa kawaida, ataenda huko kufanya nn?
Je,akikutwa na Corona itasemwa?Je,hizo nchi zitaamini certificates za Tz? Maana tunasema Tanzania hakuna Corona, sasa wataamini kweli kama tumepima majibu ni sahihi?

Tuache kutumia matatizo kama magonjwa kuwakandamiza watu wetu!Yaani kisa unajua mtu anayesafiri atakuwa na uwezo basi unampa gharama zisizo akisi uhalisia na ni za Tanzania pekee!Shame!
 
Kiasi kilichotajwa na serikali ni rahisi kulingana na clinic binafsi zilizopewa ruhusa ya kufanya test ya corona Nchini Uingereza....
Sahihi kabisa,watu wanalaumu bila kujua gharama za nchi zingine zikoje,hiyo ndio gharama yake huku na tunalipa coz hakuna jinsi.
 
Back
Top Bottom