My Tribute to Samia Suluhu Hassan! Kenya inaisifu Tanzania!

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
28,259
Reaction score
41,416
Nimejionea hii taarifa nikasukumwa kuandika huu uzi kuhusu serikali ya Tanzania ya sasa!

Kwa muda mrefu nimekua mkosoaji nguli wa serikali za CCM kuanzia kwa JK hadi kwa Samia!
Kwa hivi karibuni trend ya uchumi wa Tanzania, mapambano dhidi ya Rushwa, harakati za matumizi ya nishati safi, ujenzi wa miundombinu na maboresho makubwa katika utumishi wa umma huyu mama Samia anastahili pongezi za pekee!

Kikubwa kilichonifurahisha na kunisukuma kuandika huu uzi ni juu ya usafi katika mwenendo mzima wa usajili na uwazi wa matumizi ya madeni ya nchi. Mkaguzi mkuu wa Hesabu za kenya anasema wanapaswa kujifunza na kuiga huu mfumo bora kabisa toka Tanzania.

Hii video hapo chini ni kutoka nchi ya Kenya tunayoamini na kuisifu ipo mbali sana kuliko Tanzania katika katiba na mengine mengi wanakiri kuja kujifunza Tanzania juu ya uwazi katika fedha!! Rais Ruto alikiri Tanzania inaizidi Kenya kwa exports!!
Hakika mwanamke anaweza na anaweza tena!

Huu uzi umenifanya niwakumbuke akin mama shupavu sana akina Benazir Buto, Angela Markel, Margaret Thatcher na Her majesty the Queen Elizabeth II wa Uingereza!!

My Tribute to Samia Suluhu Hassan! Hongera Samia hongereni wanawake Mnaweza!
 
Attachments

  • v09044g40000cv3b97fog65nj0ml7sug.mp4
    77 MB

Unaifananisha Kenya na Tanzania kwa kutumia specific to general approach. Actually Kenya ipo juu kiuchumi kulikon Tanzania, kawaida ni kwamba tajiri hujifunza hata njia za utafutaji za masikini, ili azidi kuwa tajiri.
 
Wakenya na Watanzania wana wivu wa jadi.

Wakenya wanatamani mambo ya Tanzania, wakati Watanzania wanatamani mambo ya Kenya.

Watanzania wengi wanatamani katiba mpya ya Kenya na mambo kama uraia pacha na jamii inayoruhusu uwazi zaidi.

Wakenya wengi wanatamani nchi isiyo ma ukabila sana, isiyo na rushwa sana, iliyo na ardhi sana, isiyo na matabaka ya dhahiri sana.

Wakenya wanatamani viongozi wa Tanzania kama Magufuli na Samia. Wakati hawawaelewi vizuri.

Watanzania wengi wanatamani mtu kama Magufuli angejikita katika siasa za kimataifa kukabiliana na ubeberu kiukweli, kama de-dollarization of African economies, hoja aliyoishikilia sana William Ruto.
 
Kenya kaja kujifunza namna ya kuweka kumbukumbu za madeni. Wewe unasema huo utaratibu sifa apewe Samia lakini huo utaratibu umekuwepo toka Nyerere, wa kujua nani katukopesha ila wewe unasema sifa apewe Samia, hapo ndio shida ya uchawa inapokuja.

Huu utaratibu wa kuweka rekodi sahihi za madeni tunao miaka yote, na miaka yote watanzania tumekua tukiambiwa deni letu ni kiasi gani. Sasa Samia anaingiaje hapo?

Kama mtu kafanya jambo jema asifiwe ila hii sio hoja kabisa.
 
Nimejionea hii taarifa nikasukumwa kuandika huu uzi kuhusu serikali ya Tanzania ya sasa!

Kwa muda mrefu nimekua mkosoaji nguli wa serikali za CCM kuanzia kwa JK hadi kwa Samia!
Kwa hivi karibuni trend ya uchumi wa Tanzania, mapambano dhidi ya Rushwa, harakati za matumizi ya nishati safi, ujenzi wa miundombinu na maboresho makubwa katika utumishi wa umma huyu mama Samia anastahili pongezi za pekee!

Kikubwa kilichonifurahisha na kunisukuma kuandika huu uzi ni juu ya usafi katika mwenendo mzima wa usajili na uwazi wa matumizi ya madeni ya nchi. Mkaguzi mkuu wa Hesabu za kenya anasema wanapaswa kujifunza na kuiga huu mfumo bora kabisa toka Tanzania.

Hii video hapo chini ni kutoka nchi ya Kenya tunayoamini na kuisifu ipo mbali sana kuliko Tanzania katika katiba na mengine mengi wanakiri kuja kujifunza Tanzania juu ya uwazi katika fedha!! Rais Ruto alikiri Tanzania inaizidi Kenya kwa exports!!
Hakika mwanamke anaweza na anaweza tena!

Huu uzi umenifanya niwakumbuke akin mama shupavu sana akina Benazir Buto, Angela Markel, Margaret Thatcher na Her majesty the Queen Elizabeth II wa Uingereza!!

My Tribute to Samia Suluhu Hassan! Hongera Samia hongereni wanawake Mnaweza!
Sawa
 
Kwahiyo una maanisha mi 5 tena sivyo?
1000377658.jpg
 
Huyo controller wa Kenya, kwenye hiyo video aliyoweka kwenye mada yake anasema mfumo umewekwa 2017.

Mleta mada kaamua tu kumpa credit Samia.
Poleni sana haters wa mama, mtaumia saaaana yaani. Mama anaupiga mwingi mpaka mwenda zake anatabasamu na kupumzika kwa amani kabisa huko aliko.....hajutiii kabisa kumtaja, mara mbili, awe mgombea mwenza na hatimae makamu wa Raisi.

Mengi yanakuja, haters andaeni ndoo za kutosha za kububujishia machozi yenu.
 
Integrated System imekuwa implemented in 2017, halafu wewe unamsifia Samia.

Ama kweli tenda wema nenda zako, kwenye hii dunia.
Kuna maboresho mengi sana kwa huo mfumo tangu hiyo 2017 mpaka sasa! Namsifu kwa kuusimamia na kuuendeleza pia!! Pia yeye ndiye mkuu wa Nchi hivyo anastahili kubeba sifa pamoja na lawama juu ya mambo yote ya serikali. Ulitaka nimsifu Magufuli wakati hatuko naye?
 
Poleni sana haters wa mama, mtaumia saaaana yaani. Mama anaupiga mwingi mpaka mwenda zake anatabasamu na kupumzika kwa amani kabisa huko aliko.....hajutiii kabisa kumtaja, mara mbili, awe mgombea mwenza na hatimae makamu wa Raisi.

Mengi yanakuja, haters andaeni ndoo za kutosha za kububujishia machozi yenu.
Sasa nibubujikwe na machozi kwanini kwa mfano.

Binadamu tunatofautiana, wengine wana soni ya kuchukua sifa ambazo sio zao. Na wengine wala hawakosi usingizi.

Ni kama juzi alivyokuwa Tanga yaani hana noma kabisa ‘bi tozo’. Maboresho ya bandari ya Tanga kazi inaanza kipindi cha Magufuli dunia nzima inaona, halafu anajidai hela katoa yeye.

Ndio kama huyu mleta mada, video inasema wazi kabisa mfumo umewekwa lini yeye kaamua tu kumpa sifa mtu mwingine.

Si bora angesema Tanzania tu.
 
Kuna maboresho mengi sana kwa huo mfumo tangu hiyo 2017 mpaka sasa! Namsifu kwa kuusimamia na kuuendeleza pia!! Pia yeye ndiye mkuu wa Nchi hivyo anastahili kubeba sifa pamoja na lawama juu ya mambo yote ya serikali. Ulitaka nimsifu Magufuli wakati hatuko naye?
Ungesema Kenya, wamekuja kujifunza kwenye mfumo wetu wa usimamizi wa maswala ya fedha. Hakuna ambae angeona shida.

Tatizo ni kutaka kumpa credit mtu mwingine kama vile yeye ndio main architect, wakati si yeye.
 
Back
Top Bottom