Mzazi alomfikisha Mahakaman Mwl Madrasa Kwa kosa la kuchapa watoto, akemewe popote pale anapoonekana na ikiwezekana Jamii imchukulie hatua

Dah hayajakukuta bado,nyinyi ndio aina ya watu mnaoharibu watoto kwa kigezo cha uhuru na demokrasia mwisho wa siku mtoto akishahama nyumbani kwako anaenda kuwa jambazi au shoga huku mzazi bado unakenua meno tu
Kupiga sana mtoto haimzuii kuwa jambazi au shoga.

Kupiga mtoto ni ufinyu wa kufikiri, na ukosefu wa maarifa ya malezi, kwa kudhani kuwa hakuna namna nyingine ya kumfanya mtoto afuate unachotaka.

Halafu ni muhimu uelewe kuwa mtoto siyo lazima afuate unachotaka.

Unaweza kufuata anachotaka yeye, hapa napo najua utashangaa!
 
dini ya kikatili sana hii aisee, na ina watu kama wewe? kwa taarifa yako, huyo mtoto ukimzaa ni wako kwenye makaratasi tu, ila kiuhalisia sio wako, ni wa serikali au kwa lugha nyingine ni wajamii nzima. ukimdhuru ukavuka mipaka ya sheria za kiserikali, jamhuri inakuchukulia hatua. hata mashuleni, kuchapa watoto viboko kumeruhusiwa ila sio kila mwalimu anachapa na kuna masharti ya kuchapa na hata number za viboko vingapi sheria imeweka.

ukizaa mtoto wako ukamtesa, jamhuri inakuchukulia hatua, usipomtunza jamhuri inakuchukulia hatua, ukimfanyia ukatili wowote ati kwa sababu ni wa kwako jamhuri itakuchukulia hatua. na hata hapo ni hamhuri imemchukulia hatua huyo ustaadhi katili anayeumiza watoto, labda kama katika uislam inaruhusiwa kutesa watoto hivyo ndio mje hapa mseme, ila waislam viongozi wako walishatoa waraka kulaani kile kitendo na wamejivua gwanda wakamwachia huyo mwalimu katili msala.

kumbe vitoto vinavyopitia madrasa vinafuata uislam kwa lazima, vinaumizwa na vimekuwa sugu hadi visura utakuta vimekasirika tu muda wote tunajiuliza ni kwa nini, kumbe vinapitia ukatili kama huo? na wakiwa watu wazima wanakuwa makatili sana hata ukimwambia uwa mtu wanaweza kuua kwa sababu ya makuzi kama hayao. unakutana na kitoto kimekunja sura kama kimtu kizima kumbe kimetoka kuchapwa fimbo.
 
Mshenz sana uyo mzazi
Fimbo za kawaida kabisa zile
 
Sisi ni waafrika mkuu....

Ni mizani gani bora inayotulazimisha tuishi kama waliberali ?!!
 
Nilijua wameacha kuchapa miaka hii hao waalimu kuna mwalimu wa madrasa wa msikiti wa ijumaa Moshi alikuwa anaitwa ustadhi mabawa aisee alikuwa anatuchapa Sana
 
Mtaani kwetu wengi ni waislamu
Watoto wanatoka shule saa 11 au 12 wanakula wanaenda madrasa kurudi saa 4 usiku. Kesho tena wanaamka saa 11 ili saa 12 wawe shule.
matokeo yake wanafeli elimu dunia afu wanasingizia wakristo wanapendelewa marks mitihani, kumbe vitoto havipumziki na hekaheka akili hazipumziki hadi vinachanganyikiwa.
 
Mshenz sana uyo mzazi
Fimbo za kawaida kabisa zile
...mzazi ni mliberali ,watu wanadai anapenda sana muziki na "beats" sasa amempeleka mwanaye madrassah akajue kupiga MADUFU tu ili awe anawaburudisha katika shughuli za maulid ya familia...
 
Nilijua wameacha kuchapa miaka hii hao waalimu kuna mwalimu wa madrasa wa msikiti wa ijumaa Moshi alikuwa anaitwa ustadhi mabawa aisee alikuwa anatuchapa Sana
Si bora kuchapwa hizo fimbo kuliko kuchapwa bakora za maisha haya yaliyo magumu na ya fitina sana....

Mtoto wa kiume na kike anakataa kuchapwa bakora hanzuruni mianzi halafu anakwenda "kuchapwa nao".....
 
Wewe Huwa humchapi mtoto wako ??
 
Wewe Huwa humchapi mtoto wako ??
simchapi kama vile yule mwalimu alivyomchapa. watoto wangu pia wana furaha, hawana woga. mnachapa vitoto hadi vinakua na visura vimekunjamana hasira muda wote utafikiri kametoka afghanistan kupigana, kumbe maskini kametoka kukaririshwa mistari kwa lazima na kamechapwa kikatili. na maisha yao hao ukiwaangalia wana maisha ya kimaskini pengine hata kula hakajala,kamerudi shule hakuna msosi, kubangaiza kakachelewa, kanafika kule kanachapwa, na kesho kanajiandaa kwenda shuel elimu dunia tena. mnatesa watoto.
 
Come and see for your self,we don't have to waffle all day we work
If you like and love israel why don't you go to them and find out how they treat african
Kwahiyo wewe ni muoman au mtanzania/mmatumbi mwenye asili ya oman au mtanzania aishie oman
Nataka nijue kitu kabla sijaendelea
 
Huyo Mwalimu kawachapaje hao watoto na fimbo ngapi?.
 
Vipi kama mtoto alirudi nyumbani akiwa na alama za mchirizi ya fimbo za mwalimu?
 
Wewe ndo huyo mwalimu au Una undugu nae maana umeandika kwa uchungu Sana
 
Sisi ni waafrika mkuu....

Ni mizani gani bora inayotulazimisha tuishi kama waliberali ?!!
Uafrika ni rangi tu mkuu, mifumo ya mwili inafanya kazi sawa tu kwa binadamu wote.

Wewe unadhani ni sababu gani inayotufanya tushindwe kuishi kama waliberali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…