Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Unaona sasa kwa kusema hii sio facebook ni jf ina maana unafahamu facebook ipo vipi, inaonekana vipi n.k, kwa wewe kusema hauamini kama Mungu yupo/hayupo ina maana itakua unafahamu Mungu jinsi anapaswa awe, kama Mungu angekuepo dunia ingekua hivi ama vile in short utapinga/huamini/kukosa kuamini katika uwepo wake kwa sababu kwa namna ama nyingine utakua unafahamu concept za Mungu... Itakua unafahamu ilipaswa iwe namna fulani ili uwe na imani juu ya uwepo wake..

Sasa hebu nieleze, kitu kipi kinakufanya ukose imani ya uwepo wa Mungu, na mambo yapi ambayo yangetokea ama kutendeka yangekupa imani juu ya uwepo wake kwa maana kwa kupinga tayari unafahamu nini maana ya uwepo wake?
 
Mimi sijui Kama Mungu yupo au hayupo...siajema yupo au hayupo.

Nachosema ni kuwa hawa Mungu (Allah & yahweh) wanaoelezewa kwenye vitabu vya dini ya kikristo/uislam hawapo.
Hakuna ushahidi kama wapo.
Kama unao uweke hapa.

Ni sawa na mimi nikuambie kuwa kuna binadamu mwenye mabawa.
Sasa wewe tayari unajua binadamu yukoje na mabawa yakoje kwhayo kupiga picha binadamu mwenye mabawa sio shida...Shida itakuja kwenye kuniamini mimi kuwa huyo binadamu yupo.
Sio jukumu lako kutoa ushahidi kuwa huyo binadamu hayupo.
Bali ni jukumu langu mimi niliyekuambia kuwa yupo binadamu wa hivyo kukupa ushahidi usio na shaka.

Nikishindwa kukupa huo ushahidi, madai yangu unapaswa uyapuuze lakini hautasema kuwa binadamu wa hivyo hayupo, lakini utasema "Sina ushahidi kuwa binadamu wa hivyo yupo, kwa hiyo siamini yupo...Siku nikipata ushahidi nitaamini yupo"

Ndoivyo sasa kwa Mungu...Kwa hizi dini mbili hawa Mungu wao (Allah au Jehova) anatakiwa awe Na uwezo wote, ujuzi wote na awepo kila mahali.
Sasa bado sijapata ushahidi wa uwepo wake.
 
Ndio maana nasema uliposikia Mungu yupo, unasema huamini kama yupo ama hayupo, swali langu kutakua na sababu na hoja ya msingi kwa nini huamini yupo ama hayupo, je ulitaka umuone kwa macho, je ulitaka aje kwako akuambie nipo? je ulitaka iweje? thats my qn...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwann mwamposa sio sawa? Ila TAG iwe sawa?
Kwa imani yangu hata watoto wangu nimepiga marufuku kupelekwa kanisani na wife ninawafundisha good manners za life sio kuwatishia kuna Mungu ambae alimtoa mwanae wa pekee ili atusamehe zambi zetu na sio kulitoa roho shetani ili tusamehewe dhambi zetu na tupumue
 
Ndio maana nasema uliposikia Mungu yupo, unasema huamini kama yupo ama hayupo, swali langu kutakua na sababu na hoja ya msingi kwa nini huamini yupo ama hayupo, je ulitaka umuone kwa macho, je ulitaka aje kwako akuambie nipo? je ulitaka iweje? thats my qn...
Ndiomaana nikajibu siamini kuwa hayupo, ila sijapata ushahidi wa uhakika wa kuamini kuwa yupo.

Sasa huo ushahidi wa uhakika unaweza kuwa kwa njia yoyote ile.. ila tu iwe ya uhakika.
Uwanja ni mpana.
Wewe hata ukiniambia twende Bunju saa saba usiku tutamuona anashuka ...ni sawa.

Ushahidi wa uhakika na siyo maneno matupu kama yaliyojaa kwenye vitabu vya dini. Sijui nani aliambiwa na nani akamuambie nani.
 
Kwa imani yangu hata watoto wangu nimepiga marufuku kupelekwa kanisani na wife ninawafundisha good manners za life sio kuwatishia kuna Mungu ambae alimtoa mwanae wa pekee ili atusamehe zambi zetu na sio kulitoa roho shetani ili tusamehewe dhambi zetu na tupumue
You're not wrong.
 
You're not wrong.
  • MAMA yako mzazi yuko sahihi na ataendelea kuwa shihi kwa kile anacho amini.
  • Nawe kwa upande wako uko sahihi.

Je nini kifanyike?
- Toka hapo nyumbani, nenda kajitegemee, uwe huru kufanya kile kilicho sahihi kwako. ILA kuendelea kukaa kwa mama na kukaidi anachokueleza, busara ya kawaida inasema sio vyema, hauko sahihi na unakosea sana!.
 
  • MAMA yako mzazi yuko sahihi na ataendelea kuwa shihi kwa kile anacho amini.
  • Nawe kwa upande wako uko sahihi.

Je nini kifanyike?
- Toka hapo nyumbani, nenda kajitegemee, uwe huru kufanya kile kilicho sahihi kwako. ILA kuendelea kukaa kwa mama na kukaidi anachokueleza, busara ya kawaida inasema sio vyema, hauko sahihi na unakosea.
Nimekuelewa.
 
Ndiomaana nikajibu siamini kuwa hayupo, ila sijapata ushahidi wa uhakika wa kuamini kuwa yupo.

Sasa huo ushahidi wa uhakika unaweza kuwa kwa njia yoyote ile.. ila tu iwe ya uhakika.
Uwanja ni mpana.
Wewe hata ukiniambia twende Bunju saa saba usiku tutamuona anashuka ...ni sawa.

Ushahidi wa uhakika na siyo maneno matupu kama yaliyojaa kwenye vitabu vya dini. Sijui nani aliambiwa na nani akamuambie nani.
Kama huamini kuwa hayupo ina maana kuna mambo kadhaa yanakufanya usiwe 100% na imani kwamba Mungu hayupo, hebu nielezee mambo yapi yanakufanya uwe na imani kwamba yawezekana Mungu yupo? na mambo yapi yanakufanya uamini yawezekana Mungu hayupo? Ina maana upo 50 by 50,
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
Mama yako ndiye sahihi.
 
Niamini au nisiamini hii haihusiani.
Awepo asiwepo hii haihusiani.

Swala la kujadili hapa je ni sahihi kumlazimisha mtu aamini Mungu yupo?
Si sahihi hata kidogo... lakini je kuna ubaya wowote kujaribu kumconvince mtu aone uwepo wa Mungu??
 
Mzazi yupo sawa sababu we ni mtoto wake hataki uharibikiwe na kingine bado unaishi chini ya wazazi wako unatakiwa ufate kile wanachokwambia

Kijana mdogo ushaona dini uliyozaliwa ndani yake uiamini

Acha kujipa usahihi na mzazi wako mzazi huwa hakosei hata siku moja
Huyu She Quoted you mpaka hapa hajitambui.. Mzazi huwa anapenda mtoto wake awepo popote patakapomjenga mtoto awe na maadili mema. Kanisani ni moja ya sehemu hizo.

By the way, kama anajiona amefika umri wa kujiamulia mambo yake aanzishe kwake..!! Huwezi kuwa huru huku kuna vitu unamtegemea mwingine.
Yaani huyu She Quoted you anaona kishavuka miaka 18 kwenye kuamua au kupambanua, lakini na miaka hiyo hiyo 18 bado yupo kwa mzazi
 
Mimi sijui Kama Mungu yupo au hayupo...siajema yupo au hayupo.

Nachosema ni kuwa hawa Mungu (Allah & yahweh) wanaoelezewa kwenye vitabu vya dini ya kikristo/uislam hawapo.
Hakuna ushahidi kama wapo.
Kama unao uweke hapa.

Ni sawa na mimi nikuambie kuwa kuna binadamu mwenye mabawa.
Sasa wewe tayari unajua binadamu yukoje na mabawa yakoje kwhayo kupiga picha binadamu mwenye mabawa sio shida...Shida itakuja kwenye kuniamini mimi kuwa huyo binadamu yupo.
Sio jukumu lako kutoa ushahidi kuwa huyo binadamu hayupo.
Bali ni jukumu langu mimi niliyekuambia kuwa yupo binadamu wa hivyo kukupa ushahidi usio na shaka.

Nikishindwa kukupa huo ushahidi, madai yangu unapaswa uyapuuze lakini hautasema kuwa binadamu wa hivyo hayupo, lakini utasema "Sina ushahidi kuwa binadamu wa hivyo yupo, kwa hiyo siamini yupo...Siku nikipata ushahidi nitaamini yupo"

Ndoivyo sasa kwa Mungu...Kwa hizi dini mbili hawa Mungu wao (Allah au Jehova) anatakiwa awe Na uwezo wote, ujuzi wote na awepo kila mahali.
Sasa bado sijapata ushahidi wa uwepo wake.
Bible inasema, "Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu" Zaburi 53 :1a
 
Ungekuwa unaishi kwako usingeandika haya pengine ujuaji wa dini nyingine imekuingia unatafuta muumini mwenzako hapa aamini unacho amini lengo lako sio kuandika kuwa hutaki kwenda kanisani lengo ni kuwaambia watu kuwa Ukristo haufai na wanapotea ila ujumbe wako hujaufika vizuri. Usizunguke mbuyu
 
Kama alinizaa hata nizeekeje bado ni mtoto wake.
Suala la dini (Imani) ukisema ni matokeo ya kuwa Brainwashed na wazungu inaakisi namna ambavyo hujui kudadisi mambo.

Kifupi, miaka maelfu wanadamu wamekuwa na ugomvi na concept ya kuabudu. Msingi wa ugomvi ni:-
1. Kuabudu Mungu mmoja ni sahihi ama sio sahihi? Huyu Mungu mmoja ni nani?
2. Kuabudu miungu wengi ni sahihi ama sio sahihi? Hawa miungu wengi ni akina nani?

Kwamba kuna asiyeabudu kabisa? Huyu hayupo. Sana sana utakuta amezama kwenye kundi la kuabudu miungu wengi.

Kundi utakalochagua ni kama bundle la simu hivi (yaani unapata SMS kadhaa, muda wa maongezi dakika kadhaa, GB kadhaa nk). Wewe Tu!

Kuhusu wewe kukosa Imani na kumbishia mzazi wako kuhusu kwenda ibadani pamoja, Mama yako yupo sahihi 100%. Ikiwa yeye akiondoka kwao ili aishi atakavyo, nawe fuata hizo nyayo uishi upendavyo.

Ukiwa kwako hiyo kesi ya twende kanisani itakuwa imekufa kishujaa.
 
Back
Top Bottom