Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Wanawake wengi sana ambao ni wahudhuriaji na waumini wazuri wa kanisa uasherati(mapenzi kabla ya kufunga ndoa)
Siku hizi wengine wanafunga ndoa wakiwa wajawazito kabisa.
Wengine ni wakwepa kodi, michepuko, watesaji wa mabinti wa kazi,waongo n.k
 
kuna idea mbili tofauti hapa kwanza bado upo kwenu kwahiyo kibongo bongo lazima ufuate kanuni za hapo kwenu pili mara nyingi wazazi wengi wakiafrica huwa wanategemea hata kama mtoto ni mtu mzima ufuate yeye anachofikiria ni bora kwake hata kama wewe unaona hakina logic mfano kuna kipindi nilikua nimemaliza chuo na sikua na kazi ya kueleweka ambayo mzazi kwenye fikira zake aliona inafaa kulingana na elimu aiyoniseomesha lakini akawa haelewi kwamba ajira ni ngumu kwahiyo nikawa napiga vibarua hapa na pale siku moja kanifuata huko nilikokua nimepanga kaniambia twende kwa mganga akanifanyie zindiko eti nimerogwa niikataa na nikamsihi asiniambie kitu kama hicho tena. Kiukweli aliongea na kulalamika sana na kusema watoto hatusikiizi wazazi. Lakini point sio heshima ni kuangalia kama mtu mzima kipi unaona kinakufaa na kipi hakikufai.

Tatu naona watu humu wanatoa uhusiano wa kuharibikiwa na kwenda kanisani ni mawazo yakushangaza maana kuharibikiwa ni tabia ya mtu na maamauzi na hapa hakuna mungu wala shetani anaweza kubadili tabia ya mtu ndio maana leo hii dini kila kona ila mambo maovu yanaendelea sadly wengine wafanyao ni hawa hawa wanaoshinda kanisani.

Ushauri kwenda kanisani sio jambo baya we nenda imani ya mtu ipo moyoni mwa mtu fanya kama mambo yoote tuliyofanya utotoni ili kumfurahisha mzazi mfano kupretend kupenda taarifa ya habari na huku unamiaka 6 hujui hata kinachoongelewa ni nini, au kujifanya unasoma masaa sita huku uwezo wako ni masaa mawil ili tu mzazi aone unasoma kwa usongo kila mtu humu jukwaani kapretend. Sio idea mbaya just do it wont hurt.
 
Vipi kama angebadili dini na kuwa Muislamu akawa anaenda Msikitini Ijumaa badala ya kanisani Jumapili??

Halafu kwa nini Housegirl anabaki nyumbani wengine wakiwa Kanisani? Huo sio ubaguzi??
 
Sawa sasa kwanini haniachi?
Mtu mzima aliyezidi 18 ni wa kulazimisha dini kweli?
Mara useme wewe kwake ni mtoto, hapa tena unasema we ni mtu mzima uliezidi 18 yrs.
Ama kweli muwamba ngoma huvutia kwake.

Hilo jambo lako kama jamii haijakifunza basi huwa tunasoma life skills pale form 1 , ukikikosa hicho kipindi basi utasoma parsonal hygiene and good manners hapo hapo form one.

Kama unaona maza anakosea hama hapo ukakae kwake, wewe ukiwa kwako utakaa nyumba moja na mchawi??
Watu wanaosali ni ngumu sana kukaa na wasiosali kabisa na wasiomuamini Mungu kama wewe!!

Kama upo kwake fuata sheria zake la sivyo utamfanya akuchukie na kukuona wewe kama kikwazo kwenye familia.
Tatizo watoto wa kike mnapenda sana battle, yani unabattle na mzazi wako eti nani yuko sahihi, so ukiambiwa wewe ndo uko sahihi utaenda kumuonesha huu uzi ama??

Ajabu sasa ukiolewa na mume mwenye mawazo kama ya mama yako na ww utaanza kusali.
 
Angekuwa kwenye nyumba ya Answar Sunni halafu akageuka kuwa Mkristo ila akalazimishwa kujifunika ushungi ingekuwa sahihi kutii??
 
Hoja yako imejaa hisia au mhemko mkubwa
 
Sipo 50 by 50....soma vizuri post zangu utanielewa.
Mungu huyu wa hizi dini mbili hayupo kwa asilimia 100%
Mungu halisi anaweza kuwepo na sina uhakika kama yupo, ila ushahidi uliopo/ambao haupo nampa asilimia 0.000000001% ya kuwepo.
 
Mada yako umeileta ya nini ikiwa unakataa ushauri unaopewa na wengi? Tatizo ni kwamba unajiona una uelewa sana kuliko Hawa wote wanaokushauri,...



Nje ya mada kidogo,
Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anaweza kuoa mke wa namna kama yako
 
Kuna sehemu nimesema ukristo haufai?? Ukristo unafaa.
 
Kwahyo kabla ya wazungu waafrka tulisali rozali ya bikra maria na kumsifu yesu kristo?
 
Sawa
 
Ni sawa,kwa sababu ana wajibu wa kulea,mbona huulizi uhalali wa mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda shule ,kunywa dawa akiumwa,kula anapokataa kula?
Hayo yote yanafanywa kwa watoto
 
Im sorry.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…