Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Wanawake wengi sana ambao ni wahudhuriaji na waumini wazuri wa kanisa uasherati(mapenzi kabla ya kufunga ndoa)
Siku hizi wengine wanafunga ndoa wakiwa wajawazito kabisa.
Wengine ni wakwepa kodi, michepuko, watesaji wa mabinti wa kazi,waongo n.k
Mwenyezi Mungu akujalie akili ya kuona mbali. Kwa aina ya maisha unayotaka kuishi, utakuwa ni mwanamke wa hovyo kupindukia.

Maana sifa mojawapo ya mke mwema, ni ucha Mungu wake. Sasa sijui mwenzetu utakuwa binti maisha yako yote!

Vipi na wewe siku ukiwa mama? Utawahamasisha watoto wako kusali, au mtashinda wote nyumbani mkichati na ma boyfrend wenu?
 
Mambo vipi wakuu,
Nimemaliza chuo mwaka jana, I am 24. nipo nakaa hapa nyumbani ila kuna tatizo la kiimani.

Mom analazimisha kila jumapili niende kanisani.
Kiuhalisia mimi saivi sina imani kabisa na kanisa au maswala ya Mungu naona kama ni utapeli na mambo ambayo binadamu walitengeneza tu hayana ukweli wowote.

Sasa nikaanza kamgomo kangu baridi ka kutoenda, kila ikifika j'pili nakuwa na kisingizio tofauti, mara naumwa, sijiskiii etc.

Sasa imeenda hivyo mwishowe mama akaamua anifungukie kuwa as long as bado naishi chini ya paa lake, kwenda kanisani ni lazima. Akajaribu kunidadisi kwanini sipendi kwenda, Mimi nkaona kabisa nikimwambia siamini tena maswala ya dini atapata presha bure.

Nkawa namuambia kuwa siamini katika kusali kanisani maana Mungu yupo moyoni na naweza kumuomba siku yoyote iwe juma3 au juma4, na nkamuambia kama biblia nnayo kwenye simu naisoma kila siku na nasali kila siku.
ila akawa haelewi anasema biblia inasema "wakutanapo wawili kuna Mungu...bla bla bla"

Sasa mimi nkamuambia "Nikuambie tu sasa ukweli, Mimi naona ibada ni kati yangu na Mungu wangu wala sio kati yangu mimi na wewe na mungu. Kwahyo kama unanilazimisha kwenda kanisani, ntaenda ili nikufurahihishe tu, ntakuwepo kimwili kanisani ila kiroho na kiakili sitakuwepo kanisani"
Akaanza kusema niende kwa ajili yangu sio kwa ajili yake
Nkamuambia "sasa mimi sijawiwa kwenda, ila wewe ndo umenlazimisha nifanyeje?"

Akakaa kimya. ila siku hiyo alikasirika siku nzima na ilikuwa jumapili akaanza mpaka kusema "Mimi ningekuwa na nyumba nyingine ningeenda kuishi nikawaacha maana haina maana kukaa na watu hamnitii"

Mimi nikamuambia "Lakini mama, Swala la kanisani sio la utii kwako, ni la kwangu na Mungu na wala hutakiwi kunilazimisha"

Akasema "Sisi ndivyo tulivyolelewa, na watoto wangu wote nimewakuza hivyo mpaka leo wanasali, wewe ndio unataka kupinga siwezi kukubali. Subiri ujitegemee ndiyo ukaidi, ila as long as bado upo chini yangu kanisani ni lazima"

Nikaendelea kutokwenda kibishi kibishi tu.

Lakini housegirl ndio siku moja akaja akayatibua tena..Tumemaliza kula usiku mara akaanza kusema kabla hatujalala ana jambo la kuniambia pale sebuleni.

Housegirl: "She, leo nikuambie tu mbele ya mama hapa, hili swala linaniumiza mno. mkubwa anakuambia kitu halafu unakaidi. Sio vizuri na leo imenifika shingoni lazima nikuambie. Sio vizuri unapomkaidi mama yako na kupinga kwenda kanisani au kwenda kwa kuchelewa sana.Huyu ni mkubwa na mkubwa akisema kitu wewe mtoto unatakiwa ufuate. Mungu anakupima, huenda ukimtii na ukaenda kanisani utafunguliwa hata mambo yako mengi kama kupata ajira"

Ukawa mjadala mrefu sana pale wakisapotiana na mama.

Sasa mimi nikaona hii ishakuwa kesi, ila nikaona usiwe ubishi usio na faida pale sebuleni, maana hata niseme kwa lugha ipi, hata niongee kigiriki na kiyunani. Hawa watu hawawezi kunielewa. Ni kwamba wako brainwashed na dini ya mzungu mpaka stage kwamba mimi ndio wataniona punguani.

Sasa nkamuangalia mama nkaona kama anaumia moyo sana kwa ajili yangu na kisa ni kwenda kanisani tu.
Isiwe kesi sana

Ikabidi sasa nitumie hekima tu niwajibu "Nimewasikia, Mungu hutumia watu wake kufikisha ujumbe, na leo amewatumia nyie kufikisha ujumbe kwangu. Kwahyo nimesikia na kwa utiifu kuanzia sasa nitaanza kwenda kanisani Amina"

Lakini kanisani naenda na simu, nakaa nyuma nachati ibaada nzima hadi muda wa kuondoka hata ukiniuliza muhubiri alikuwa jinsia gani au alikuwa amevaa nguo gani au amehubiri nini wala sijui.
Yani sipendi kabisa naona kama napoteza tu muda wangu huko.
Ikifika jumapili nakosa raha kabisa kwasababu hiyo.

Sasa wakuu, naombeni ushauri wenu, Nipo sahihi? Au nisimamie msimamo wa kutoenda? Au niendelee kwenda kwa kuwafurahisha tu? Au niwaambie nimeasi kabisa?

Nani yuko sahihi hapa, kati yangu na mama?
kuna idea mbili tofauti hapa kwanza bado upo kwenu kwahiyo kibongo bongo lazima ufuate kanuni za hapo kwenu pili mara nyingi wazazi wengi wakiafrica huwa wanategemea hata kama mtoto ni mtu mzima ufuate yeye anachofikiria ni bora kwake hata kama wewe unaona hakina logic mfano kuna kipindi nilikua nimemaliza chuo na sikua na kazi ya kueleweka ambayo mzazi kwenye fikira zake aliona inafaa kulingana na elimu aiyoniseomesha lakini akawa haelewi kwamba ajira ni ngumu kwahiyo nikawa napiga vibarua hapa na pale siku moja kanifuata huko nilikokua nimepanga kaniambia twende kwa mganga akanifanyie zindiko eti nimerogwa niikataa na nikamsihi asiniambie kitu kama hicho tena. Kiukweli aliongea na kulalamika sana na kusema watoto hatusikiizi wazazi. Lakini point sio heshima ni kuangalia kama mtu mzima kipi unaona kinakufaa na kipi hakikufai.

Tatu naona watu humu wanatoa uhusiano wa kuharibikiwa na kwenda kanisani ni mawazo yakushangaza maana kuharibikiwa ni tabia ya mtu na maamauzi na hapa hakuna mungu wala shetani anaweza kubadili tabia ya mtu ndio maana leo hii dini kila kona ila mambo maovu yanaendelea sadly wengine wafanyao ni hawa hawa wanaoshinda kanisani.

Ushauri kwenda kanisani sio jambo baya we nenda imani ya mtu ipo moyoni mwa mtu fanya kama mambo yoote tuliyofanya utotoni ili kumfurahisha mzazi mfano kupretend kupenda taarifa ya habari na huku unamiaka 6 hujui hata kinachoongelewa ni nini, au kujifanya unasoma masaa sita huku uwezo wako ni masaa mawil ili tu mzazi aone unasoma kwa usongo kila mtu humu jukwaani kapretend. Sio idea mbaya just do it wont hurt.
 
Vipi kama angebadili dini na kuwa Muislamu akawa anaenda Msikitini Ijumaa badala ya kanisani Jumapili??

Halafu kwa nini Housegirl anabaki nyumbani wengine wakiwa Kanisani? Huo sio ubaguzi??
Mleta mada hujitambui, yawezekena unatumia ngada au unasumbuliwa na ujuaji wa kijinga au usomi uchwara. Wewe mtu mzima gani unaishi kwenu, alafu unaambiwa na mzazi wako ufuate taratibu za mji wake unashupaza shingo. Au unataka wakati wanapoenda kanisani ubaki unamtafuna housegirl. Hapo Mzee akitangulia mbele za haki na wewe utatanguliza tumbo lako kudai urithi wakati sasa hivi unasema wewe ni mtu mzima hupangiwi Wala kulazimishwa. Kuwa na adabu kwa baba yako, na wewe utafanyiwa upuuzi km huu na watoto wako. Wazazi wako ni Mungu wa pili wanakuongoza kwa mema. Acha ujuaji na usera wa kijinga. Umeniudhi sana km Mzazi.
 
Sawa sasa kwanini haniachi?
Mtu mzima aliyezidi 18 ni wa kulazimisha dini kweli?
Mara useme wewe kwake ni mtoto, hapa tena unasema we ni mtu mzima uliezidi 18 yrs.
Ama kweli muwamba ngoma huvutia kwake.

Hilo jambo lako kama jamii haijakifunza basi huwa tunasoma life skills pale form 1 , ukikikosa hicho kipindi basi utasoma parsonal hygiene and good manners hapo hapo form one.

Kama unaona maza anakosea hama hapo ukakae kwake, wewe ukiwa kwako utakaa nyumba moja na mchawi??
Watu wanaosali ni ngumu sana kukaa na wasiosali kabisa na wasiomuamini Mungu kama wewe!!

Kama upo kwake fuata sheria zake la sivyo utamfanya akuchukie na kukuona wewe kama kikwazo kwenye familia.
Tatizo watoto wa kike mnapenda sana battle, yani unabattle na mzazi wako eti nani yuko sahihi, so ukiambiwa wewe ndo uko sahihi utaenda kumuonesha huu uzi ama??

Ajabu sasa ukiolewa na mume mwenye mawazo kama ya mama yako na ww utaanza kusali.
 
Angekuwa kwenye nyumba ya Answar Sunni halafu akageuka kuwa Mkristo ila akalazimishwa kujifunika ushungi ingekuwa sahihi kutii??
Huwezi weka philosophical au theological zako kwenye nyumba za watu. Ungekuwa mtu mzima na unaelimu kama usemayo usingeishi kwenu

Utu uzima sio umri pekee Bali ni majukumu pia.

Hata angekuwa anaabudu mashetani anamamlaka ya kukuambia uabudu hayo mashetani na ukafanya
 
Hoja yako imejaa hisia au mhemko mkubwa
Mkuu nakushauri uhame tu hapo home ukajitegemee ili uishi upendavyo. Kuna wenzio hawana hata mama wa kuwakumbusha kwenda kanisani,wewe unae unamfanyia dharau na bado ati unaenda kanisani na kuchat ibada nzima mkuu laana nyingine ni za kujitakia. Punguza dharau na ujuaji.

Jishushe,mpe thamani sahihi mzazi wako.
 
Kama huamini kuwa hayupo ina maana kuna mambo kadhaa yanakufanya usiwe 100% na imani kwamba Mungu hayupo, hebu nielezee mambo yapi yanakufanya uwe na imani kwamba yawezekana Mungu yupo? na mambo yapi yanakufanya uamini yawezekana Mungu hayupo? Ina maana upo 50 by 50,
Sipo 50 by 50....soma vizuri post zangu utanielewa.
Mungu huyu wa hizi dini mbili hayupo kwa asilimia 100%
Mungu halisi anaweza kuwepo na sina uhakika kama yupo, ila ushahidi uliopo/ambao haupo nampa asilimia 0.000000001% ya kuwepo.
 
Mada yako umeileta ya nini ikiwa unakataa ushauri unaopewa na wengi? Tatizo ni kwamba unajiona una uelewa sana kuliko Hawa wote wanaokushauri,...



Nje ya mada kidogo,
Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anaweza kuoa mke wa namna kama yako
 
Ungekuwa unaishi kwako usingeandika haya pengine ujuaji wa dini nyingine imekuingia unatafuta muumini mwenzako hapa aamini unacho amini lengo lako sio kuandika kuwa hutaki kwenda kanisani lengo ni kuwaambia watu kuwa Ukristo haufai na wanapotea ila ujumbe wako hujaufika vizuri. Usizunguke mbuyu
Kuna sehemu nimesema ukristo haufai?? Ukristo unafaa.
 
Suala la dini (Imani) ukisema ni matokeo ya kuwa Brainwashed na wazungu inaakisi namna ambavyo hujui kudadisi mambo.

Kifupi, miaka maelfu wanadamu wamekuwa na ugomvi na concept ya kuabudu. Msingi wa ugomvi ni:-
1. Kuabudu Mungu mmoja ni sahihi ama sio sahihi? Huyu Mungu mmoja ni nani?
2. Kuabudu miungu wengi ni sahihi ama sio sahihi? Hawa miungu wengi ni akina nani?

Kwamba kuna asiyeabudu kabisa? Huyu hayupo. Sana sana utakuta amezama kwenye kundi la kuabudu miungu wengi.

Kundi utakalochagua ni kama bundle la simu hivi (yaani unapata SMS kadhaa, muda wa maongezi dakika kadhaa, GB kadhaa nk). Wewe Tu!

Kuhusu wewe kukosa Imani na kumbishia mzazi wako kuhusu kwenda ibadani pamoja, Mama yako yupo sahihi 100%. Ikiwa yeye akiondoka kwao ili aishi atakavyo, nawe fuata hizo nyayo uishi upendavyo.

Ukiwa kwako hiyo kesi ya twende kanisani itakuwa imekufa kishujaa.
Kwahyo kabla ya wazungu waafrka tulisali rozali ya bikra maria na kumsifu yesu kristo?
 
Neno langu kwako ni hili,wa swahili husema "' Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu"'
kwa upande wangu naona mama yako anakuwazia mema anatamani akufunze njia ipasayo,ila ulimwengu unakutamani ukufundishe ndo maana unaona mtu aliyekubeba miezi tisa na kukutunza hadi leo una akili ya kumkosoa,unamuona anakupoteza.
Nimalizie kwa kusema mkataa pema pabaya panamngoja.
Ninachojua ni kwamba as long as bado unaishi kwake ni vyema ukamtii.
Sawa
 
Ni sawa,kwa sababu ana wajibu wa kulea,mbona huulizi uhalali wa mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda shule ,kunywa dawa akiumwa,kula anapokataa kula?
Hayo yote yanafanywa kwa watoto
 
Kwani wewe ni jinsia gani?
maana kuna imani imeingia isiyohusisha kwenda kanisani wala msikitini
nayo si nyingine bali ni ushoga na usagaji,sasa ni heri umwambie mzazi wako kwamba umejiunga huko
akuondoe hapo nyumbani usiendelee kunajisi nyumba.
Ungekuwa kwangu ningekuwa nimeishakusend hayupo muda mrefu,sema mama yako ni mvumilivu sana.
Im sorry.
 
Back
Top Bottom