Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mkuu She nafikiri uko sahihi kuwaambia ukweli kuwa huamini tena. Ila mzazi anapoudhika kwa swala la kiimani huwa ni hatari.

Kwa sisi Waislam huwa tunaambiwa tuwatii wazazi wetu kwenye kila lililo jema, ila watakapotuamrisha maovu basi kwa adabu tuyakatae.

Uko sahihi kuwa suala la imani ni kati yako na Muumba wala mama halimhusu kwakuwa ushakuwa mtu mzima sasa.

Lakini kwakuwa uko chini ya paa lake sioni kama una chaguo, Ushauri wangu ni kuwa endelea kwenda Kanisani wakati huohuo jaribu kutumia njia nzuri kumuelewesha mama ni nini unafikiri kuhusu Dini na Mungu, tena mueleze kwa upole na adabu zote nina amini utaipata njia sahihi.

‘By the way i have been there’
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Afadhali wewe umekuwa muwazi .
Huo ndio umuhimu mkubwa wa dini kwa Africa hasa usipokuwa tajiri. Mahusiano ya kijamii.Ndoa, kusaidiwa katika shida kubwa na kuzikana.
Ni aina fulani ya uoga wa maisha pia.
 
Mungu hajawahi shindwa kwa mwanadamu kuna sehemu atakubana, maisha yatakubana, kila mlango wa mafanikio utakuwa umebana hapo sasa utakuwa huna kimbilio zaidi ya kwenda church mwenyewe bila kulazimishwa niliwahi kuwa kama wewe way back ila kuna mahali nilibanwa sikuwa na namna na sasa nafurahia uamuzi wangu wa kumfuata Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu..
 
Mmh hongera sana.
Ni wanadini wachache wenye mawazo huru kama wewe.

So far kwenye huu uzi, watu wasio na dini ndio nimeona wako open minded (pamoja na kuwa wengi wao wamesema sipo sahihi, ila wametoa sababu zinazo make sense) ila wanadini wao wapo kulazimisha wanachoamini wao tu.
Ukizingatia sijaomba ushauri kuhusu kuamini Mungu au La, ilikuwa mjadala kuhusu swala la uhuru wa kiimani.

Kama imani inalazimishwa basi haina maana tena, maana imani ni kuamini, na huwezi kulazimisha mtu aamini unachotaka.

Wewe kwa mindset yako utafika mbinguni (kama ipo) kuliko hao mashehe wanaoshinda msikitini.
 

Wajibu wa mzazi Ni kumlea, kumuongoza Na kumsimamia Mtoto wake.

Wajibu wa Mtoto Ni kumtii mzazi Na kufuata maelekezo ya mzazi ili akabidhiwe kwenye "dunia" iliyo Salama kwake.

Kumbuka asiyefunzwa Na mamaye hufunzwa Na ulimwengu, Na kamwe hapaswi kuja kumlalamikia mzazi wake yakimkuta: kumbuka 'asiyesikia LA MKUU huvunjika guu'.

Mama yako ana nia mzuri sana Na we we, Na Kwa vile umemaliza chuo karibuni, yawezekana umesoma zaidi Yake.

Anachokuzidi Ni kwamba yeye Ni Mzazi, ambaye amepewa kibali Na Mungu kukulea Na kukusimamia akikuongoza katika mema anayoyajua.

Tafakari haya kabla ya kufikiri umkubalie au umkatalie "maelekezo" Yake, ukikumbuka ombi LA Mkubwa Ni amri..
 

Okay nmekupata, ila kwa umri wa wazazi sitajaribu kuwaelewesha..maana ni umri unaoaminika wa kumrudia muumba.
Kwahyo haitakuwa na maana wataona kama najaribu kuwapotosha niwanyime raha za mbinguni.

How did you solve your case?
 
Usidhani maisha yako yanareflect maisha ya kila mtu...Kuna nchi hata haziamini Mungu na wananchi wanaendelea kufanikiwa na kututawala eg. China
 
Kwa nini kusema kuwa ana degree imekuuma sana??! Inferiority complex inakusumbua.
Tafuta degree na wewe kama huna ili mtu akisema ana degree usiumie.
 
Hata ungekuwa umelelewa kwenye dini 20, una uwezo finyu sana wa kufikiri nje ya chungu cha dini, wewe ni mlevi wa dini.
 
Kwa nini kusema kuwa ana degree imekuuma sana??! Inferiority complex inakusumbua.
Tafuta degree na wewe kama huna ili mtu akisema ana degree usiumie.
Yaan namshangaa sanaaa huyu Taikon, nilikua namuona akili kubwa, ila ktk huu uzi ndo kajivua nguo zaid
 
Mifano yako ni pointless
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…