Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

😂,Sijui tukusaidie vipi🙆‍♀️,inakaa kama mamako ni mkristo mwenye itikadi kali,, hao huwa hawaelewi kitu, hata umweleweshe vipi,, anza kwenda kanisani au uondoke ukapange chumba kwingine
 

Unajua kuwa Dini ndio Utamaduni wenyewe unazungumzia mambo ya taboos?
 
Usipomuabudu Mungu
Utapata miungu ya kuabudu
Dah, kwani binadamu hawezi kuishi bila kuabudu??

Mbona mnamshisha binadamu na kumfanya kama kiumbe dhaifu kuliko nyani?

Nyani hawaabudu, mbona wanaishi? Wanapata mahitaji yao na maisha yanaenda.
Inamaana binadamu ndio kiumbe hafifu lazima atafute likitu la kuabudu sio?
 
Kanisa ni kituo cha kulelea maadili.

Sijasema Kanisa ni baya.
ila ukishakuwa mkubwa na maadili yako halina maana tena.
Yani ushanufaika na neno la Mungu na kanisa afu ukubwani unalikana
Unapomkana Mungu/imani yako umekana na Kanisa/watumishi wa Mungu
Usipeleke mtoto huko mfundishe Sayansi Mama Mungu si hayupo?
Malezi ya kumjua Mungu ya nini na ushaona hayupo?


Sema tu ur bored na routine ya kanisani
Ama km umemkataa Mungu mkatae na kila kitu chake uvuguvugu wa nini?

Unajicontradict
 
Reactions: Cyb
Kama sasa Ibada yako ni upingaji wa uwepo wa Mungu
 
Mimi kusema Mungu hayupo haimaanishi dini haina umuhimu.
Dina ina mapungufu yake mengi na ina faida zake chache.

Naweza kuwapeleka ili wafunzwe uoga utotoni (uoga wa kutenda dhambi) lakini Nitajitahidi sana wanangu wasiliwe ubongo na dini na kugeuka misukule kama ya kwa mwamposa.

Maana ukishaliwa ubongo huko kutoka ni ngumu.

Wachache tulioweza kutoka tunashukuru.

So kuwapeleka wakiwa wadogo ni nzuri ila wakishafika miaka 12 kuendelea nawaachisha.
 
nakazia hapa
 
Kama sasa Ibada yako ni upingaji wa uwepo wa Mungu
Kwani mtu akipinga uwepo wa mungu,, huyo mungu atapata athari gani?,,
Maandiko yanasema, binadamu alipewa utashi wa kuamua mwenyewe na sio kushurutishwa,,
Kuabudu hakumuongezei kitu mungu,, wahindi wanaabudu ng'ombe, sanamu, etc wachina wanaabudi budha, na maisha yanakwenda.
Binaadamu yuko huru
 
Hakuna siku ya mwisho, siku yako ndio mwisho ila kwa wengine bado wataendelea kuishi, na hukumu pia hakuna hukumu hiyo, malipo ni hapa hapa ukiiba kabla hujaondoka ulimwengu huu lazima ulipe malipo ya uwizi
 
Unajua kuwa Dini ndio Utamaduni wenyewe unazungumzia mambo ya taboos?
Ni kweli dini ni utamaduni...Lakini utamaduni sio dini.
Dini ni subpart ndogo ya utamaduni.

Utamaduni una mambo mengi, Taboos zipo ndani ya utamaduni. Na zingine ndani ya dini.

Mfano kuna kabila mwanamke hatakiwi kula map*mbu ya ng'ombe au mbuzi...Hiyo ni Taboo lakini haihusiani na dini yoyote.

So kitu kuwa Taboo usiforce kinahusiana na dini automatically.
Hata babu zetu hawakuoana wao kwa wao kabla ya dini kufika na mashua.
 
Dhambi ni misimamo/sheria za Mungu
Atheists mnaamini Mungu hayupo so kwenu hamna dhambi

Woga wa dhambi wa nini Mama na Mungu hayupo?
We staki nataka wa Mungu
 
Hakuna athari
Kwani Mungu yupo?
Heri we umemkana full
Kuliko mwenzio anasema Mungu hayupo ila watoto atawapeleka kanisani😅
 
Dhambi ni misimamo/sheria za Mungu
Atheists mnaamini Mungu hayupo so kwenu hamna dhambi

Woga wa dhambi wa nini Mama na Mungu hayupo?
We staki nataka wa Mungu
Actually natumia lugha yako ili unielewe kirahisi.
Nimesema dhambi kwa context ya kanisani, lakini mimi naangalia Morality in generall, kujua mema na mabaya.

Kuiba, kuzini, kuua, kudanganya nk. Nk.
Ni vitu vya morality, Visingefundishwa kanisani nisingepeleka watoto kanisani...

Na hata mm nkiwa na muda wa kukaa kuwafundisha hivi vitu sitowapeleka.
Ikitokea organization ya kufundisha morality kwa watoto bila dini ntawapeleka huko.

Morality ya kufundishwa in form of stories na vitisho...kama wanavyofanya kanisani.
 

Taboo lazima ihusiane na Dini,
Taboo inahusiana na miungu na ukishasema miungu moja Kwa moja unataja Dini.
Taboo ni miiko. Na miiko inahusianishwa na Imani Fulani Kwa miungu.

Embu nitajie Taboo yoyote unayoijua ambayo haiendani na Dini?
Vinginevyo hujui maana ya DINI
T
 
😂,Sijui tukusaidie vipi🙆‍♀️,inakaa kama mamako ni mkristo mwenye itikadi kali,, hao huwa hawaelewi kitu, hata umweleweshe vipi,, anza kwenda kanisani au uondoke ukapange chumba kwingine
Dah, kazi ninayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…