Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Kwa mujibu wa utafiti watanzania wengi Wana matatizo ya akili 🚶🚶🚶🚶
 
Kwahyo kwenda kanisani ni jambo la kulazimishana?
Kwa kuwa unalelewa basi ni shuruti sio ombi.

Huyo ni mzazi hawezi kukuacha pale anapoona unapotea nafsi yake haiwezi kukubali. Ni bora upotee wakati hakuoni. siku moja utatubia hayo unayomtendea mama yako wakati huu
 
Binti nenda kanisani tafadhali

Hiyo akili unamiliki mama anaijua kuliko hata sisi
Kwani ni lazima? Hata nikienda kumfurahisha anione nimeenda.
Je vipi kiimani? Mungu anaonaje?
Maana naenda tu kuchati huku moyo ukisononeka muda wangu unavyopotea
 
Binti unataka upotee njia uku mama anashuhudia...haiwezekani alooh nenda kanisani
 
Kiufupi ni kua hauna adabu. Unapokua chini ya nyumba ya mtu unatakiwa ufuate kile alichokipanga na kukiweka basi, Tofauti na hivo ni utovu wa nidhamu.

Utafanya chchte utakacho ukiwa ndani ya nyumba yako umekaa kweny sofa lako tofauti na hapo ww unatakiwa uchwapwe na uburuzwe mno.
 
Kwa kuwa unalelewa basi ni shuruti sio ombi.

Huyo ni mzazi hawezi kukuacha pale anapoona unapotea nafsi yake haiwezi kukubali. Ni bora upotee wakati hakuoni. siku moja utatubia hayo unayomtendea mama yako wakati huu
Okay yeye anaona napotea, ila mimi sipotei.
Kwasababu nawajua wengi huko kanisani wahuni kuliko hata mimi nisiyeenda.

Au Kupotea una maana gani? Maana kitabia mimi ni mtulivu na wala sina uhuni wowote.

Na hata nikisema niende kumfurahisha, kiimani imekaaje? Maana siamini huko nakoenda.
 
Kwani ni lazima? Hata nikienda kumfurahisha anione nimeenda.
Je vipi kiimani? Mungu anaonaje?
Maana naenda tu kuchati huku moyo ukisononeka muda wangu unavyopotea

Kwahiyo huna imani yoyote Ile?
 
Ni halali yake kukushinikiza uende kusali atakako.
Unaishi kwake Kwa nini usifuate Sheria zake?
 
Kwakuwa ni mama itabidi uende mara moja moja kumridhisha, angekuwa mtu mwingine ungepiga chini
Duh, sasa yeye hata hiyo mara moja moja hataki, yani anataka kila j2. Na hilo kanisa wana ibaada ndefu saa 2 hadi saa 8 huko.

Sawa mkuu...Mimi ntaenda kumfurahisha yeye mzazi. ila bado naona kabisa hili jambo si sawa.
 
We share the same case study asie mimi sikuta ujinga nilikata utumwa wa fikra na maendeleo yangu ni mazuri kuliko awali.
uko sahihi kikubwa ni kuwa na amani ya moyo inner peace,mimi nawaambiaga kwa mifano mbona mababu zetu hawakuwa na dini na waliishi vizuri na kuwa na maadili ya juu kuliko zama hizi za dini na maadili mabovu.
 
Mwenyezi Mungu akujalie akili ya kuona mbali. Kwa aina ya maisha unayotaka kuishi, utakuwa ni mwanamke wa hovyo kupindukia.

Maana sifa mojawapo ya mke mwema, ni ucha Mungu wake. Sasa sijui mwenzetu utakuwa binti maisha yako yote!

Vipi na wewe siku ukiwa mama? Utawahamasisha watoto wako kusali, au mtashinda wote nyumbani mkichati na ma boyfrend wenu?
 
As long as unaishi kwake akiwa amekufuga inatakiwa ufuate anachokuamuru,Kama unataka Uhuru kapange🥺
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…