Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Hahah...yani kila mtu anavutia kwake. Akija muislam anavutia kwake, msabato nawewe unavutia kwako 😂 hizi dini ni vichekesho
 
Mara nyingi hatufanyi vitu kwaajili yetu binafsi bali tunafanya vitu kwaajili ya watu tunaowapenda...ni suala la muda tu, tafakari kwa dhati
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka sana aisee
 

Umeeleza vizuri Sana.

Ikiwa unamarifa haya yote ni kwanini unashindwa kuelewa Sababu za Mama kukulazimisha uende Kanisani tena Kanisa analosali yeye ilihali unaishi kwake?

Kwa sasa ninaamini umejua kuwa ni halali Kwa Mama yako kuingilia Uhuru wako uwapo katika utawala na himaya yake. Si ndio?
 
Sio halali...Lakini kwakuwa yeye anaamini ni halali namimi sitaki kupishana naye nitamfuata kumfurahisha tu.
 
Mungu ana nafasi yake.

Utamtafuta mwenyewe kwa machozi.

Hapo upo kwenye comfort zone.

Ila muavuli wa mama yako ukiondolewa na ukakutana na machungu ya dunia.

Utautafuta huu uzi uufute.

Dunia bila ulinzi wa kiroho ni chungu mno.

Heshimu nafasi ya Mungu.
 
Wewe wasema
 
And you were lucky,ni heri ulifikia kupata neema ya kumgeukia Yesu,maana kama ungepotea kabla ya kuufikia wokovu na kumjua yeye saa hizi ungekuwa unateketea...
 
Fuata kile unachoona sawa, maisha ni yako...
 
Bado unaishi kwa mama?...
 
Sio halali...Lakini kwakuwa yeye anaamini ni halali namimi sitaki kupishana naye nitamfuata kumfurahisha tu.

Wewe unaamini sio halali, Naye anaamini ni halali.
Hivyo ambaye yupo kwenye himaya ya mwenzake ndio afuate sheria za mwenzake.

Na hapo Wewe ndio sio halali Kwa sababu upo kwenye himaya ya Mzazi wako.

Halali na haramu inaletwa na SHERIA.
Sijui mama unalijua Jambo hilo
 
Ukikaa miaka minne kitaa bila ajira, utajua Mungu yupo au hayupo, kusali ni muhimu au siyo muhimu.
 
Sipo 50 by 50....soma vizuri post zangu utanielewa.
Mungu huyu wa hizi dini mbili hayupo kwa asilimia 100%
Mungu halisi anaweza kuwepo na sina uhakika kama yupo, ila ushahidi uliopo/ambao haupo nampa asilimia 0.000000001% ya kuwepo.
Hata hio 0.000000001% tayari kuna imani ndogo juu ya uwepo wake, Yesu alisema imani ndogo mfano wa punje ya haradali unaweza fanya mambo makubwa mno, sasa hio sio completely zero, imani yako ndogo hio imepelekewa na sababu zipi?
 
Zaidi ya 18 ni mtu nzima na katiba inatambua. Unachagua imani yoyote unayotaka. Tena nakupongeza kwa kugundua Ukristu ni uzungu na Uislamu ni Uarabu. Tulipokea hizi imani bila kuhoji, sasa ni wakati wako wa kuhoji. Waambie una imani katika mababu zako waliokufanya uwe duniani, hao ndio kiungo chako na Mungu wa kweli. Ila usibishane nao maana hawatakuelewa.
 
Jehanam ipo kwa ajili ya wanao kaidi, na paradiso ni kwa ajili ya wanao tii UKO HURU KUCHAGUA mahali upapendapo,
 
Kwa kuongezea mimi nadhani inategemea pia na aina ya kanisa, kiukweli kuna makanisa yameibuka yamechangia sana kuchanganya na kuharibu imani za waumini hasa vijana. Imagine unaenda kanisani kama kwa yule sijui Nabii aliyechorwa tattoo na mke wa mtu na kupelekea kuvunja ndoa ya muumini wake hapo unatajia nini? Kumbuka vijana wa sasa ni wa dadisi sanaa... Kuna kijana Wa rafiki yangu kamaliza form 4 mwaka juzi amegoma kuendelea na shule (form 5) au chuo na amehamia kwa mchungaji wa haya makanisa ya mwendokasi eti naye anataka kuwa mchungaji..
 
Kwa mwamposa
Nilitegemea aina hii ya makanisa. Nina swali je umewahi kufikiria kwenda yale makanisa kama ROMA au Lutheran? I mean yale makanisa ya zamani ambayo tulikuwa nayo kabla ya haya ya mwendokasi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…